Migomo ya walimu ya enzi ya JK imepotelea wapi?

Wamizigo

Member
Sep 8, 2017
52
54
Habari wana JF,

Enzi za JK walimu kupitia viongozi wa CWT walikuwa wakitangaza migomo wakidai haki zao kama vile nyongeza ya mshahara, n.k.

Siku hizi mbona hatusikii viongozi hao wakitangaza hiyo migomo ilihali serikali ya Rais Magufuli haijafanya chochote kwa walimu hao.

Je, hii inamaanisha nini kwa viongozi hawa?
 
Habari wana jf?
Enzi za JK walimu kupitia Viongozi wa CWT walikuwa wakitangaza migomo wakidai haki zao kama vile nyongeza ya mshahara, n.k. siku hizi mbona hatusikii Viongozi hao wakitangaza hiyo migomo ilihali serikali ya JPM haijafanya chochote kwa walimu hao. Je, hii inamaanisha nini kwa Viongozi hawa?
Viongozi wameona hata wakitangaza mgomo,wagomaji ndo hao waliotumbuliwa kwa vyeti feki na wengine bado uhakiki unaendelea.Usije kukuta hao watangaza migomo nao wanapumulia mashine
 
Ajira ndani ya serikali ni sawa na ndoa.

Ndoa inaweza kua mbaya sana lakini bado wanandoa wanakomaa kuinusuru ndoa yao, ndani ya serikali utalalama sana ila kutoka yanabaki maneno.

Na tusiwe wanafiki, asilimia nyingi za wajasiriamali walipata ujasiri wa kujishughulisha kwa kazi zao binafsi binafsi baada ya kujaribu kuingia serikalini mara kadhaa bila mafanikio.
 
Hakuna jambo baya kama kugoma moyoni pasi na kusema mdomoni, kwa wenye watoto shule huko wataelewa ninachomaanisha
 
Habari wana jf?
Enzi za JK walimu kupitia Viongozi wa CWT walikuwa wakitangaza migomo wakidai haki zao kama vile nyongeza ya mshahara, n.k. siku hizi mbona hatusikii Viongozi hao wakitangaza hiyo migomo ilihali serikali ya JPM haijafanya chochote kwa walimu hao. Je, hii inamaanisha nini kwa Viongozi hawa?
Hata maandamano na mikutano ya kisiasa hakuna na watu kimyaaaa, usiwaonee Walimu tu watu wote wamenyweaaa.
 
CWT ni Manyonyaji ya walimu. Viongozi wao wanakata kwa NGUVU walimu 2 asilimia. CWT wanakusanya Bilions za fedha kwa walimu hali walimu wanaishi kwa kukopa kopa. CWT Viongozi wanadanya kuwa kuna Benki imeanzishwa ya walimu kumbe inamilkiwa na vibaraka wengine. Maamuzi ya CWT iwe wilayani, mikoani, Taifa ni ya watu wachache mno na yanafanyika kunufaisha watu hao sio walimu. Kwa mtazamo wa walimu wengi Jinsi CWT ilivyo Nyonyaji kwa Walimu -Ni vema uchunguzi wa fedha za afanyiwe CWT bila mzaha kwani walimu wananyonywa sana na hawa viongozi wao.
 
Sasa hivi ukigoma au kuanzisha mgomo, wewe ni hujipendi na kazi yako pia,
Wasiojulikana......
 
Usiulize migomo tu bali uulize na unafuu wa hali uliokuwepo kwa wananchi kwa ujumla kabla ya mtu asiyejulikana kuja eneo la tukio.
 
Back
Top Bottom