Ndoa nyingi za wasomi zinavunjika na zingine zipo taabani dhoofu, leo nizungumzie kidogo chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika na kuwa na migogoro isiyo isha,
Nianze na wanawake
Mara nyingi mabinti wengi hushindwa kutofautisha maisha ya ndoa na uchumba wanawake wengi wasomi hupitia mahusiano mbalimbali wakiwa vyuoni wengi huishi pamoja na wenzi wao hupika na kufanya shughuli zote kwa zamu, hivyo mabinti wengi huchukulia kitendo kile kama hali halisi ya maisha na hata wakiolewa hushindwa kubadilika na kutaka kufanyiwa na waume zao kama walivyokuwa wanafanyiwa na wapenzi wao yaani kufanya kazi kwa zamu kitu ambacho wanaume wengi hukataa na kupelekea mwanamke kujenga chui hapendwi na kuleta migogoro ndani ya ndoa.
Sababu ya pili wanawake wasomi huolewa na watu ambao sio chaguo lao wengi huolewa na watu ambao hawawapendi kutoka moyoni ila tu kutokana na msukumuno fulani kama vile kipato cha mwanaume, au kuhofia umri umesonga mara baada ndoa baada ya kile kitu kilicho msukuma kuolewa kuzoeleka migogoro huanza
Sababu ya tatu ni ulimbukeni wa kipato mara nyingi wanawake wa kipato huanza dharau kwa kujiona kuwa wanaweza kuishi bila mwanaume na maisha yakaenda.
Sababu ya 4
Usaliti katika ndoa mara nyingi wanawake wasomi hupenda kupasha viporo na wapenzi wao wa zamani na kusaliti ndoa zao kuliko wanawake ambao hawajasoma sababu inaweza kuwa mazoea amefanya hivyo akiwa chuoni hivyo amechukulia kama jambo la kawaida, lakini vilevile inawezekana mme hamridhishi anakumbuka makoloni yake.
Sababu ya 5
Kubadilika tabia kunakoletwa na makundi pamoja na kuangalia tamthilia wanawake wengi huchukulia maigizo yale kama ukweli na kuyaingiza katika maisha yao mwisho wa siku hubadilisha tabia zao na kuharibu mahusiano yao
Wanaume
Wanaume wengi wanaoa wanawake waliosoma sio kwa sababu wamewapenda ila kutokana na kuvutiwa na kitu fulani kama kipato cha mwanamke mara nyingi utasikia mwanaume anasema nataka kumuoa mwanamke mwenye mshahara tusaidiane maisha, huu ujinga wa hali juu ukimuoa mwanamke sababu ikiwa hiyo ndoa hiyo haitadumu, pesa ya mwanamke haipangiwi bajeti, mwisho wa siku nikuachana baada ya kugundua lengo halitatimia.
Uchepukaji nao ni tatizo kubwa linalopelekea ndoa nyingi kuvunjika utafiti unaonyesha kuwa wanaume wasomi wenye kipato wanachepuka sana kuliko wale wabangaizaji na wanawake wasomi na wenye kipato hushindwa kuvumilia na kuachika.
Suluhisho
1.usioe/olewe kwa sababu ya kipato elimu.
2.siku zote zungumza mwenzi wako.
3.Tumia njia sahihi kutatua migogoro yenu.
4.Tambua kwamba ndoa ni zaidi ya elim/kipato.
5.Mwanaume ni kichwa cha familia tekeleza majukumu yako kama mwanaume ikiwemo kuhudumia familia.
6.mpe uhuru mkeo kutumia pesa nyingi yake.
7.mwanamke tekeleza majukumu yako kama mama wa nyumbani.
8.Tambua uaminifu ni silaha katika ndoa.
9.siku zote mwanamke kuwa mnyenyekevu katika ndoa yako
Mkifanya hivyo ni ndoa yenu itakuwa yenye furaha tele na mtakuwa mfano wa kuigwa.
Alamsiki.