Styvo254
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 246
- 226
Hamjambo WanaJamii
Kero kubwa kwa mkulima hasa pale anapokua akihesabu 'vifaranga', ni wadudu wanaokula mazao yanapohifadhiwa. Swala hili limekera tangu binadamu wa kwanza kugundua kuhifadhi chakula kwa matumizi ya baadae. Ni swala ambalo liko kati kwa kumfilisi au kumhujumu mkulima wa Afrika. Mbinu zinazotumika sasa kupambana na swala hili sana sana ni madawa au sumu za kuwaua wale viumbe. Dawa/Sumu hizi hutumika kwenye mazao na basi ni hatarishi kwa matumizi ya binadamu.
Sasa kuna mbinu mbadala isiyotumia sumu, endelevu na sio hatarishi kwa binadamu. Mbini hii inatumia mifuko aina mbili kwa kuhifadhia mazao. Kuna mifuko MIWILI ya polythene/nailoni ndani ya kiloba/gunia, huja pia na kamba mbili za kufungia ile mifuko ya ndani.
Matumizi sahihi ya mfumo huu ndio siri ya urembo. Unapokua ukiweka mazao, mifuko lazima iwe imesimama wima ili kupata ujazo wote wa mfumo kwa sababu muhimu na ya msingi katika matumizi haya; KUJAZA KABISA MAZAO ILI KUTOA HEWA YOTE MLE!! Hii ndio njia ya kuhakikisha wale wadudu, hapo wakiwa mayai, hawata komaa na kuanzia kula mazao. Kuhakikisha hakuna hewa yeyote itakayo weza kuingia mle, mfumo wa pili pia lazima ufungwe vizuri pale juu, kuufinikia wa kwanza ndani; mwisho kuishona ile gunia na kuhifadhi vizuri.
Njia hii upunguza uharibifu wa wanyama wengine kama panya wanaokua pia wanashambulia mazao. Vipi utauliza? Mnyama yule utegemea harufu au hutumia pua kutafuta chakula, kwa vile mazao haya yamewekwa ndani ya mifuko MIWILI ya nailoni/polythene, hakuna harufu inayotoka na kuwavutia wale wanyama. Ila hakukosi mmoja wawili mtundu anayeangukia, kwa hivyo basi ni muhimi kuwashughulikia wengine kama hawa kwa kuiweka ile mifuko sehemu iliandaliwa vizuri dhiidi yao.
Bila hewa, au mzunguko wake hakuna kiumbe hai chochote kinachoweza kuishi. Mimea pia ni viumbe hai na mazao, ambayo hua ni mbegu au sehemu zingine za mmea - hasaa za uzazi, hayawezi ota yakaendelea na Mzunguko wa Maisha kwa vile hakuna hewa au mvuke/maji mle ya kuotesha. Mazao yale hubaki vile vile kwa mda mrefu - kuna repoti ya kuufungua mfuko baada ya miezi saba na kuyapata mazao safi kabisa. Wale wadudu kwa kuna hata hawakupita ngazi(stage) ya mayai hawatakua issue tena.
Tulivyo ona hapo juu, ni muhimu sana ile mifuko ya polythene iwe MIWILI ili kuzuia kabisa upenyaji wa hewa. Kutotii kwa maagizo ya matumizi kama sala, pia hudhuru utendakazi wa mifuko.
Mifuko hii ilibuniwa na Purdue University ya America.
Sent using Jamii Forums mobile app