Mkuu kama una uwezo nunua Router nzuri, sio tu itakusaidia kwenye kustream online bali hata offline, kwa maisha ya kisasa router ni must have kuunganisha vifaa vyote nyumbani.
Kuhusu suala la kustream na kukwama halihusiani na router ama simu ama mifi bali aina ya modem iliotumika.
Ili kutake advantage ya mitandao yetu hio router inatakiwa iwe na:
1. Band zote, 800, 1800, 2300 na 2600 mhz, kuna band zinakuwa na speed kuliko nyengine, mfano speed ya tigo band 800 ni ndogo ila band 1800 ni kubwa sana.
2. Iwe na angalau Lte Advance (300mbps kupanda) sababu tayari mitandao yetu baadhi wana hii speed.
3. Iwe na angalau Mimox2 ila Mimox4 recomended, hii huongeza speed sana, hasa kwa Halotel, ni uwezo wa Router kupokea signal kutoka Mnara(antenna) zaidi ya mmoja.