Microsoft wainunua linkedin kwa dola bilioni 26

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
31,340
41,680
kwa wale walioshangaa facebook kutoa dola bilion 18 kununua whatsapp leo microsoft amezidisha zaidi kwa kutoa dola bilioni 26 kununua linkedin kwa haraka haraka ni zaidi ya trilioni 55 za kitanzania (miaka miwili ya bajeti yetu ya nchi nzima)

linkedin imebase sana kwenye makampuni na wafanyabiashara hivyo microsoft ameona itamfaa kwenye office 365 na cloud service yake ya azure

-kwa wasioijua microsoft hii ndio kampuni kubwa ya software duniani na ni maarufu sana kwa operating system yao ya windows inayopatikana kwenye zaidi ya asilimia 90 ya computer zote duniani, pia wana cloud service ya azure, wana microsoft office, wanatengeneza hardware za games (xbox) pamoja na games zenyewe kama vile age of empire na mambo mengi

-kwa wasioijua linkedin hii ni social network ya wafanyabiashara, wafanyakazi na professional mbalimbali huko wanaeka kazi walizozifanya na ujuzi waliokuwa nao. waajiri wengi hupenda kuajiri kwa kutumia linkedin, pia hawa jamaa wanamiliki kampuni ndogo ndogo nyingi kama lynda.com ambayo hufundisha course nyingi online, slideshare ambayo watu hu upload documents online nk
habari zaidi

Microsoft to buy LinkedIn, in $26.2 billion deal [Update]

unafikiri microsoft yupo sahihi?
 
Mmmmmmh bajeti yetu miaka 2.
Ila Microsoft saa zingine wanabugi mno
 
Haaaaa,Jamaa anasema Microsoft wamebug,aisee hawa Jamaa ni makini sana,kumbuka had Google anapeleka kiasi flan cha faida microsoft
 
Safi kabisa, linkedIn ni mtandao muhimu Sana kwa carrier growth, nilishawahi kufungua uzi hapa na kueleza faida zake, thanks Microsoft
 
kwangu mm naona ni good deal,huwa napatwa nawakati mgumu kujua return ya investment kubwa kama hizi faida huwa inaanza kuonekana baada ya miaka mingapi.manake trilioni 55 sio pesa ndogo
 
Back
Top Bottom