Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Yaah mkuu was a super game na argentina walikuwa kwenye fomu yao
Ila toka pale jahazi la argentina limekumbwa na misukosuko mingi

Na kila world cup huwa wanaenda kama favourites to win lakini safari yao huishia njiani, pengine pia vikosi vyao vya kila world cup husheheni mastaa sana jambo linalopelekea Kocha kushindwa kuwa manage.

World Cup ya 1998, Fundi wa mpira haswa, Fernando Redondo aliachwa kikosini kisa alikataa kunyoa nywele!
 
Nikweli mkuu naikumbuka ile timu ya late maradona world cup ilikuwa na matumaini kibao ila kilichowakuta kwa german wanakijua
 
France 1998,
Niliwashuhudia wakali wa mabao kama Christian Vieri,marcelo salaa,ivan zamorano,davor suker,oliver Bierhoff,Jurgen Klinsman,
Uholanzi ikiongozwa na mtukutu Patrick kluvert na edgar davis,
Watu wangu wa Nguvu Columbia ya akina faustin asprila na Carlos valderama.hakika ilikuwa burudani tosha
 
Kuna Denmark ya akina Michael na Brian Laudrup (The Laudrup brothers)
 
World Cup 1970 uwanja wa Aztec kule Mexico Brazil wakilitwaa kwa mara ya tatu kwa kuichapa Italy 4-1. Pele, Garrincha, Didi, Tostao, Carlos Alberto, Marco Antonio, Jairzinho, Clodoaldo, Gerson, Rivelino, Brazil wakilitwaa kombe la Jules Rimet kimoja.

Kuna beki moja wa Italy aliyepewa jukumu la kumkaba Pele aliitwa Tarcisio Burgnich kabla ya mechi alitamba kwamba huyo Pele ameumbwa tu na nyama na mifupa kama mimi hivyo tutapambana naye lkn baada ya mechi alikiri kuwa jamaa hakuwa binadamu wa kawaida kwani bao la kwanza la Brazil lilifungwa na Pele kwa kichwa.

Wachezaji walikuwa ni hao siku hizi kakuna wachezaji tunafurahisha macho tu kwani ulevi ni ulevi mtu akikosa hela ya bia anaweza kunywa gongo ili mradi tu alewe.
 
Mimi michuano ambayo niliikubali ni ile ya mwaka 1998 Kwanza ilikua na vibe/hamshahamsha za kutosha na wakati huo Ricky Martin katoa wimbo la mashindano linaitwa cup of life(go go aleee aleeee) huu wimbo ukipigwa mpaka sahv lazima uukubali.Kipindi hiki ndio kulikua na miamba,wababe,mafundi,mabeki visiki,watukutu,washambukuaji hatari kila aina ya kipaji nilishudia mashindano haya.Sio sahv Alvaro Morata akiguswa tu anaanguka sidhani kama kipindi hiki angeweza kucheza.Argetina ilikua na Gabriel Omar Batistusta huyu jamaa namkubali sana na nilibahatika kupata watoto mapacha wa kike nimemuita Gabriela na wa kiume Gabriel alinikosha sana.Pia Argentina niliwakubali sana na Ariel Ortega,Juan Veron na Diego Simeoni sasa kocha wa ATM.kwa Brazil nilimkubali Ronaldo maana alikiwasha si kitoto akisaidiana na Rivaldo na Bebeto na Denilson jamaa anapiga chenga hatari bingwa wa kupoteza muda,kulikua na Dunga,Cuf,Roberto Carlos na golini yupo kipa Tafarel.Timu ya Chile kulikuwa na Ivan Zamorano na Marcelo Silas Hawa jamaa walinoges ha sana mashindano haya kwa upachikaji mabao pamoja na Davor Sucker wa Croatia nadhani ndio alingoza magoli na nilifurahi kumuona final ya world cup 2018 nchi yake ilipocheza na ufaransa.Kwa timu ya Ufaransa huo mwaka 1998 kwangu ndio ilikua imekamilika na yenye muunganiko mzuri.waliokiwasha na niliowakubali Zizu,Lilian Thuram,Fabian Bartez,Viera,Lizarazu,Blanc,Henry na Pires.Italy kuna forward inaitwa Vieri ilikua hatari bado wana filipo inZagi na Del piero(huyu jamaa Kofi Olomide anamkubali sana tafuta wimbo wake unaitwa danger de mort humo kavaa jezi nyuma imeandika Del Piero pia ana mtoto Anaitwa Del Pirlo Mourinho).Kwa uholanzi kulikua na miamba kina Van de Sar,Stam,De boer wako wawili(ndugu Frank na Ronald),Seedof,Edgar Davis,Cocu,Zenden,Marc Overmas,Denis Bergkamp na Partick Kluvert.Kwa Africa niliwakubali Cameroon kulikua na Patrick Mboma,Samwel Etoo na Rigober Song na kwa Nigeria kulikua na Celestine Babayaro,Tijani Babangida,Uche Okechukwu,Taribo West,Jay Jay Okocha,Sunday Oliseh,Kanu na Victor Ikpeba.Kwangu Mimi world cup bora 1998,2002,2006 na 2010.
 
Wengi wanasema World Cup ya 1970 ndio bora zaidi kutokea. Je ulitazama michuano hiyo mkuu?
 
Safi kamanda, siku nyingine uweke aya ili tukusome vizuri
 
Wc 2002, ile ilikuwa ni bab kubwa kwangu, brazil ikiongozwa na wachezaji hatar Ronardo de lima, Rivado, Ronadinho Gaucho, denlison. Uturuki ilikuwa na kikosi kizur sana kiasa wasingekutana na mafundi brazil katika hatua ya nusu fainali wangeweza kuchukua ubingwa.
 
Uzi mzuri sana huu!

Kombe la Dunia bora kabisa kulishuhudia ni 1998 pale Ufaransa. Kulikuwa na vipaji maridhawa vya hali ya juu sana. Wachezaji walionyesha ubora wao wa hali ya juu.

Ufaransa katika ardhi ya nyumbani walikuwa na kikosi bora kabisa kilichoongozwa na mchanyato wa waarabu wa Algeria Zidane na Youri Djokaeff, pia akina Vieira, Karembeu, Lizarazu, Desailly na akina Petit.

Pia siwezi kusahau Croatia ya akina Davor Suker, fundi wa mpira Zvonomir Boban walivyopambana mpaka wakatwaa nafasi ya 3.

Kizazi cha dhahabu cha Uholanzi pia kilichagiza michuano ile. Wengi wa wadachi wale wakitokea katika akademi ya Ajax Fc. Moja ya magoli ya kukumbukwa ni Denis Bergkamp alivyoifunga Argentina katika robo fainali bila shaka baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa beki wake, akakontroo, akageuka akaweka kambani. Bao maridadi sana.

Vilevile mechi bora kwa mtazamo wangu ni ile ya nusu fainali ya Brazil Vs Uholanzi, ulipigwa mpira mwingi sana, dakika 120 1-1, Brazil anashinda 4-2 kwa penati. Zamani kulikuwa na ufundi.

Kilichotokea katika mechi ya fainali, Ufaransa Vs Brazil, ni degedege alilopata Ronaldo De Lima mpaka leo hakieleweki ni nini kilimsibu inawezekana ni fitna za Wafaransa.

Mwisho kabisa, michuano hii ilipambwa sana na ule wimbo wa mashindano (go, go, go ale ale ale) ulioimbwa na msanii nguli Ricky Martin. Hakika kwangu mimi ule ni wimbo bora wa Kombe la Dunia wa wakati wote.

Hakika kombe la dunia la 1998 ilikuwa ni michuano ya aina yake.
World cup ya 1998 ilikuwa 🔥
 
Tv zilikuwa zinahesabika hapa Dar es Salaam.

Tulikuwa tunafunga safari kwenda kutazama mpira kwa marehemu Sheikh Yahaya pale Magomeni
Ya 94 tayari tulikuwa tunamiliki tv though ilikuwa black & white, ila ya 90 ndio tulikuwa tunaangalia sehemu ya jumuiya mikanda iliyorekodiwa kwa marehemu sheikh yahya
 
emoji13.png
emoji13.png
emoji13.png
Saudi Arabia wasenge wanapigwaga nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiki kizazi kilikuwa balaa 1998

Zidane
Thiery Henry
Lian Thuram
Marcel Desaily
Davo sucker
Edgar Davids
Roberto Carlos
Dunga
Ronaldo
Michaelowen
Berkam
Amokach
Ja jay Okocha
Rashid Yakin
Ekpeba victor
Kanu
Olisah Sundy
Teribo West
George Fiinidi
Barthez
Samwel Eto
Patrick Mboma
Robert Song
Denis Bekamp
Cluvert Patrick
De boer
Jaap stam
Mark fish

Taja wengine.........
Huyo Robert Song ni Rigobert Song
 
Kama sijakosea Mali walifika robo au nusu fainali kwenye hizi fainali
Hakuna timu kutoka afrika aliyewahi fika nusu fainali WC, Waliofika robo nafikiri ni Cameroon, Ghana na Senegal
 
Kuweka rekodi sawa...

Ozil, Khedira wameanza kucheza timu ya Tiafa ya Ujerumani mwaka 2009 na World Cup yao ya kwanza ni 2010 pale South Africa.

Marchisio 2006 hakuwepo kikosini wakati Italy ikitwaa Ubingwa wa Dunia na Kepteni wa Italy alikuwa Fabio Cannavaro na wala sio Gigi Buffon.

Kwa kuongezea, aliefunga goli la kwanza ni Fabio Grosso ambae pia alifunga penati ya mwisho vs France na sio Iaquinta.
 
Mm naikubali ile ya mwaka 2002 kwani ndio mara yamwanzo kumuona mchezaji ukimchezea fauli anacheka na akipigwa redi card anafurahi kwa vile anavojua kuusanifu mpira na kutia vionjoo na ile frickik aliyo ninginizwa devid siemen haijawahipo kutokea
 
Back
Top Bottom