Mastaa watakaokosa World Cup

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,098
12,472
Ikiwa yamebaki masaa machache kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia nchini Qatar baadhi ya wachezaji wataikosa michezo ya fainali hyo kutokana na sababu mbali mbali wengine kwa kupata majeraha na wengine kwa kutoitwa kwenye team zao licha ya kuwa fit na wengine waliamua kustaafu japo kwa sasa wapo katika kiwango bora.

Mastaa hao wanaungana na wakongwe kama kina Eric cantona,Ryan gigs,George weah pamoja na alfred di stefano ambao ni baadhi ya mastaa ambao hawakuwahi kucheza kwenye kombe la dunia licha ya kufanya makubwa kwenye soka na kuacha historia kwa vizazi na vizazi na mwaka huu wanaungana na wafuatao ambao hawatakuwepo nchini Qatar.

ERLING HAALAND NA MARTIN ODEGAARD (NORWAY)
Mchezaji nyota wa Manchester city na team ya taifa ya NORWAY hatukuwepo kwenye fainali hizo baada ya team yake kushindwa kufuzu hivyo ataangalia nyumbani kama tutakavyoangalia sisi pamoja na nyota mwenzake wa club ya arsenal.

MOHAMMED SALAH (EGYPT)
Mchezaji hatari wa liverpool na team ya taifa ya Egypt ataikosa michuano hyo baada ya team yake kutolewa kwenye hatua za kufuzu world cup na Senegal hivyo anaungana na mastaa wengine watakaoikosa michuono hiyo baada ya Egypt kushindwa kufuzu mbele ya Senegal.

ZLATAN IBRAHIMOVIC (SWEDEN)
Mchezaji mkongwe wa team ya taifa ya SWEDEN naye atakuwa miongoni mwa mastaa watakaoikosa michuano hyo baada ya team yake kupoteza kwenye hatua za kufuzu kwa poland na Sweden kufungasha virago kwenye hatua za kufuzu hivyo nyota huyo hatokuwepo nchini Qatar.

JAMES RODRIGUEZ NA LUIS DIAZ (COLOMBIA)
Star wa kombe la dunia 2014 na mfungaji bora wa mwaka huo JAMES RODRIGUEZ atakosa fainali hizo pamoja na nyota wa liverpool baada ya team yao kushindwa kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia hivyo nyota hao hawatakuwepo nchini Qatar.

PIERE AUBAMEYANG (GABON)
Mshambuliaji wa Chelsea na team ya taifa ya Gabon na yeye ni miongoni mwa mastaa watakaokosekana kwenye michuano hiyo baada ya Gabon kushindwa kufuzu kwenye michuano hiyo hivyo star huyo na yeye anaingia kwenye list ya wachezaji watakaokosekana nchini Qatar.

FRANK KESSIE NA WILFRED ZAHA (IVORY COAST)
Nyota wa Barcelona na IVORY COAST hatokuwepo kwenye michuano hiyo baada ya team yake kuondolewa na Cameron kwenye michezo ya awali ya kufuzu kombe la dunia tutakosa kipaji kingine kutoka Africa huku nyota wa crystal palace wilfred zaha naye akiwa miongoni mwa mastaa watakaokosa fainali hizo.

VICTOR OSIMHEN (NIGERIA)
Nyota wa NAPOLI na kinara wa mabao kwenye league hyo atakosekana kwenye fainali hizo baada ya team yake kuondolewa kwenye hatua za mtoano za kufuzu world cup na GHANA na hivyo nyota huyo atakosekana kwenye mashindano hayo.

PAUL POGBA, BENZEMA NA KANTE (FRANCE)
Nyota na kiungo wa Chelsea ngolo kante ataikosa michuano hyo baada ya kupata majeraha miezi machache kabla ya kuanza kwa fainali hizo huku kiungo wa Juventus Paul pogba naye akikosekana kwasababu ya majeraha huku France wakiwa ndio mabingwa wateteze na walikuwa na mchango mkubwa kwenye fainali zilizopita huku mshambuliaji wao akipata majeraha masaa machache kabla ya kuanza kwa fainali hizo karim benzema naye atakosa fainali hizo.

SADIO MANE (SENEGAL)
lionel messi wa Africa na star wa Bayern's Munich na team ya taifa ya Senegal hatukuwepo nchini Qatar baada ya kupata majeraha siku chache kabla ya fainali hizo kuanza na kuacha huzuni kwa team yake ya Senegal pamoja na mashabiki wa Africa kwa ujumla.

THIAGO ALCANTARA, DAVID DEGEA NA SERGIO RAMOS (SPAIN).
Hali ya sintofahamu na taharuki ilitawala miongoni mwa mashabiki wa team ya taifa ya Spain baada ya kuachwa kwa mastar hao licha ya kuwa kwenye kiwango bora siku za karibuni lakini hilo halikumfanya luis Enrique kuwajumuisha wachezaji hao huku mashabiki wakiwa na maswali ni kigezo gani kilitumika kuwaacha nyota hao lakini mwisho wa siku kocha ndo mwenye maamuzi ya mwisho hivyo maamuzi yake yanaheshimiwa licha ya wadau kulalamika.

COUTINHO, FIRMINO, GABRIEL BARBOSA NA GABRIEL MAGALHAES (BRAZIL).
Mashabiki wa Brazil walikuwa na taharuki baada ya kikosi cha team ya taifa ya brazili kukosekana jina la gabriel Barbosa mshambuliaji kinara wa flamengo na league kuu ya nchini Brazil pamoja na Robert firmino kukosa kwenye kikosi hicho huko coutinho na gabriel wakiachwa kwenye kikosi hicho mwisho wa siku kocha ndo anajua zaidi mchezaji gani anamfaa kwenye mfumo na yupi hamfai ila kwa hakika ni pigo kuachwa kwao hasa gabriel Barbosa.

VERRATTI,CHIESA NA DONARRUMA (ITALY)
Kiungo wa mpira na mlinda mlango wa PSG pamoja na nyota wa Juventus hawatakuwa miongoni mwa mastaa watakakuwepo world cup baada ya team ya taifa ya ITALY kushindwa kufuzu kwenye mashindano hayo hivyo mashabiki na wadau wa soka watakosa kuona ufundi wa wachezaji hao nchini Qatar.

MARCO REUS, TONI KROOS, WERNER NA MATTS HUMMELS (GERMANY).
Toni kroos ataikosa michuano hyo baada ya kutundika daluga mwaka jana licha ya kuwa fit na kuwa kwenye kiwango bora ila hatokuwepo Qatar wakati huo reus na werner wakiachwa kwasababu ya majeraha na matts hummels kuachwa licha ya kuwa fit huku nikolas sule na Antonia rudiger wakiitwa kuziba nafasi yake.

RIYAD MAHREZ (ALGERIA)
Nyota wa Manchester city na mchezaji wa team ya taifa ya ALGERIA atakosekana nchini Qatar baada ya team yake kushindwa kufuzu kwenye hatua za awali za kombe la dunia baada ya kufungwa na Cameron katika mechi ya marudiano licha ya kushinda mechi ya kwanza na kupoteza kwa goli mbili kwa moja kwenye mechi ya marudiano hivyo star huyo atakosekana kwenye michuano hiyo licha ya kuwa fit na kwenye kiwango bora.

Mastaa waliochwa katika team zao na watakaokosa kombe la dunia ni wengi ila hawa ndio kuachwa kwao au kutokuwepo kwao kumewagusa watu wengi wadau na mashabiki wa soka hivyo kufanya baadhi ya mashabiki kuwa na taharuki na pengine huzuni baada ya taarifa za kuthibitisha kutokuwepo kwao katika michuano hii itakayoanza leo nchini Qatar,

Leo itapigwa mechi moja ya ufunguzi kati ya mwenyeji Qatar na Ecuador mida ya saa moja katika dimba la al bayt stadium.
 
Hivi GARNACHO hajaitwa.
Huyu Promising New Messi natamani kumuona sana.
Dogo wanadai ana chembe chembe za Spain maana alishawahi kucheza mechi za under 18 za team ya taifa ya Spain hvyo baadhi ya wadau wanadai huenda ndio sababu inayomfanya aachwe katika kikosi cha Brazil.
 
Dogo wanadai ana chembe chembe za Spain maana alishawahi kucheza mechi za under 18 za team ya taifa ya Spain hvyo baadhi ya wadau wanadai huenda ndio sababu inayomfanya aachwe katika kikosi cha Brazil.
Huyo ni Mu Argentina sio Brazilian
 
Back
Top Bottom