Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,715
45,114
Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
 
Nimeangalia fainal za kombe la dunia miaka hii:

1. 1990 Italy
2. 1994 Marekani
3. 1998 France
4. 2002 Korea na Japan
5. 2006 German
6. 2010 SA
7. 2014 Brazil
8 . 2018 Russia.

Kati ya fainali bora ni zile za 2006 pale uUerumani. Mechi bora za wakati wate kwangu ni nusu fainali kati ya German na Italia. Italia wakibuka washindi kwa mabao ya Vicenzo Ianquita na mkonge Del Piero.

Ujerumani ikiwa na kikosi cha vijana wadogo kabisa. Meaut Ozil, Sammy Khadera ect.

Itali chini ya kocha Marcelo Lippi na wakongwe, Del Piero, Zambrotta, maestro Pillo, Alesandro Nesta, Fabio Canavaro na beki mtukutu Materatzzi.

Wengine ni Fabio Groso, Luca Toni, Claudio Marchsio na mzee mzima Genarro Gatuso. Captain gigi Buffoni akisimama katikati ya stick.

Hizo ni fainali zangu bora kuona.
 
World Cup 2002 (Korea and Japan)

Nilikuwa nawapenda Spain kuliko Wakatalunya.

Fernando Hierro alikuwa ndiye shujaa wangu.
Ruben Baraja
Gaizka Mendietta
Frnando Morientes
Gonzalez Raul
Ivan Helguera.
Carles Puyol

Wanafungwa kwa mikwaju ya penalty dhidi ya Korea ya Kusini.
 
Nimeangalia fainal za kombe la dunia miaka.
1. 1990 Italy
2. 1994 marekani
3. 1998 france
4. 2002 korea na japan
5. 2006 german
6. 2010 SA
7. 2014 Brazil
8 . 2018 russia.

Kati fainal bora ni zile za 2006 pale ujerumani. Mechi bora za wakati wate kwangu ni nusu fainali kati ya German na italia. Italia wakibuka washindi kwa mabao ya Vicenzo Ianquita na mkonge Del Piero.

Ujerumani ikiwa na kikosi cha vijana wadogo kabisa. Meaut Ozil, Sammy Khadera ect.

Itali chini ya kocha Marcelo Lippi na wakongwe, Del Piero, Zambrotta, maestro Pillo, Alesandro Nesta, Fabio Canavaro na beki mtukutu Materatzzi.

Wengine ni Fabio Groso, Luca Toni, Claudio Marchsio na mzee mzima Genarro Gatuso. Captain gigi Buffoni akisimama katikati ya stick.

Hizo ni fainali zangu bora kuona.
Kuweka rekodi sawa...

Ozil, Khedira wameanza kucheza timu ya Tiafa ya Ujerumani mwaka 2009 na World Cup yao ya kwanza ni 2010 pale South Africa.

Marchisio 2006 hakuwepo kikosini wakati Italy ikitwaa Ubingwa wa Dunia na Kepteni wa Italy alikuwa Fabio Cannavaro na wala sio Gigi Buffon.
 
Back
Top Bottom