Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 106

Akaondoka na kwenda kuchukua chumba katika Hoteli ya Red Dragon iliyokuwa hapohapo Cairo ambapo alipanga kukaa kwa usiku mmoja na kesho kuondoka kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kuanza harakati zake za kutaka kumuua bilionea huyo ambaye alitaka kumuua kipindi cha nyuma ila hakufanikiwa katika hilo.

Hakuchukua muda mrefu akafika katika hoteli aliyokuwa akienda. Akachukua chumba na kwenda kupumzika. Siku hiyo hakupumzika kwa raha, alikuwa akifikiria safari yake lakini cha zaidi ni kwamba alikuwa akifikiria hali ilivyokuwa ikiendelea.

Aliamini kwamba Maria angewaambia polisi kile kilichokuwa kimetokea, angetoa siri kwamba si yeye aliyefanya mauaji bali ni Fareed jambo ambalo lingemuweka kwenye wakati mgumu kwamba hata kusafiri asingeweza kutokana na ulinzi ambao ungewekwa kila kona.

Hakutaka kuona akizuiliwa kusafiri, ilikuwa ni lazima kuondoka na hata kama ingeshindikana kuondoka kwa kupitia uwanja wa ndege, basi angetumia hata meli lakini mwisho wa siku afanikiwe kuingia nchini Marakani.

Akapumzika huku akiwa na mawazo tele, ilipofika majira ya saa kumi jioni, akafungua televisheni na kuanza kuangalia. Habari kubwa ilikuwa ikipita ikionyesha kwamba kulikuwa na mtu alimuua Bilionea Keith kwenye piramidi lililopo Giza.

Moyo wake ukafurahia zaidi lakini akashtuka baada ya kuona picha zile alizokuwa amepigwa kwa kamera za CCTV zikionyesha kwamba muuaji alikuwa yeye na binti mmoja ambaye alikuwa akishikiliwa na polisi.

Moyo ulimlipuka, hakuamini alichokuwa amekiona, mapigo ya moyo yalikuwa yakimdunda kwa nguvu kwa kuamini kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, kama picha zake zilianza kuwa maarufu kwenye luninga, basi ilikuwa ni lazima atafutwe, atakapoonekana, basi akamatwe.

“Hapa napo si salama kabisa,” alisema Fareed huku akiwa ndani ya chumba kile.
Akafunga mlango kwa ufunguo, akatulia huku akifikiria ni kwa jinsi gani angeondoka ndani ya hoteli hiyo. Ilipofika majira ya saa moja usiku, akasikia sauti za watu kutoka nje.
 
SEHEMU YA 107

Haikuwa kawaida kwenye hoteli kubwa kama hiyo, akachungulia chini kupitia dirishani, alichoweza kuona ni kundi la polisi waliokuwa na bunduki wakiwa wamefika hotelini hapo na walikuwa wakiwasisitizia wafanyakazi waruhusiwe kuingia ndani ya vyumba vya hoteli hiyo.

“Mungu wangu! Wamejuaje kama nipo humu?” alijiuliza, hakupata jibu. Hakujua ni kwa jinsi gani angeondoka ndani ya hoteli hiyo, alibaki akitetemeka kwa hofu kubwa kwani kule chini ambapo ndiyo kulionekana kuwa rahisi kwake, pia kulikuwa na polisi.

“Nifanye nini? Mungu nisaidie,” alisema huku akiwa hajui ni kitu gani alitakiwa kufanya.

**** Maria alioga haraka sana, mwili wake uliwehuka, Fareed alimchanganya kupita kawaida, hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria mahali hapo zaidi ya ngono tu. Alijisugua hasa, kuanzia chini, kati mpaka juu kuhakikisha mtoto wa kike anakuwa msafi.

Alipomaliza, akachukua taulo lake na kuanza kujifuta, tena huku akihakikisha anakausha maji ya kila sehemu. Alipohakikisha kila kitu kipo sawa, akaufungua mlango wa bafu na kutoka.

Chumbani hakukuwa na mtu, alijaribu kumwangalia Fareed huku na kule lakini hakuweza kumuona sehemu yoyote ile.

Hakujua mwanaume huyo alikwenda wapi, mara ya kwanza alihisi kwamba inawezekana aliamua kufuata chakula chini, hakutaka kumsumbua mhudumu lakini kitu cha ajabu kabisa, hata kibegi chake kidogo hakikuwepo chumbani humo.
“Mmmh!” aliguna.

Akaanza kumuita mwanaume huyo chumba humo, hakusikia kitu chochote, hakumuona, akaufungua mlango na kutoka ndani ya chumba kile. Akaanza kuwa na hofu, akahisi kulikuwa na mtu aliingia ndani ya chumba hicho na kumteka mpenzi wake huyo.

Akarudi chumbani na kuanza kuvaa nguo zake harakaharaka lakini hata kabla hajamaliza, akasikia mlango ukianza kugongwa kifujofujo hali iliyomfanya kuwa na hofu.

“Nani?” aliuliza kwa sauti.
“Fungua mlango!” alisikika mwanaume aliyekuwa nje ya chumba kile.
 
Shunie umerudia bwanaaaaa
Sitaki mimiiiiii
 
Back
Top Bottom