WoooiLeo tunaimalizia
SEHEMU YA 154
Akaondoka kanisani hapo, kitu cha kwanza alichokitafuta kilikuwa kisu, akafanikiwa kukinunua katika supamaketi ambayo haikuwa mbali kutoka hapo alipokuwa.
Mwanaume aliyemuuzia ndani ya duka hilo alimwangalia kwa makini mno, sura yake haikuwa ngeni, ni kama aliwahi kumuona sehemu fulani.
Fareed akaogopa, akahisi kwamba mwanaume huyo aliliona tangazo la kutafutwa kwake hivyo alichokifanya ni kuondoka harakaharaka huku akiwa na kisu alichokinunua.
Alipofika kanisani, hakuingia katika mlango wa mbele, akapitia katika mlango wa nyuma, ule aliotolewa na padri yule, akafungua nati za kitas, akakitoa na kuingia ndani.
Kulikuwa na giza, akapiga hatua mpaka alipoufikia mlango mwingine ambao ulikuwa ni wa nyuma kuingia katika ofisi ya padri huyo. Akaingia na kutulia katika kochi moja. Padri hakuwepo, alikuwa katika chumba cha kuungamia dhambi akimsikiliza mtu mwingine.
Alikaa hapo kwa dakika ishirini, akamsikia padri huyo akija kule alipokuwa, haraka sana akaelekea nyuma ya mlango na kusimama, padri huyo akaingia.
Hata kabla hajafanya kitu, akamkaba kwa nyuma, padri Luke akashindwa hata kupiga kelele, akajikuta akianza kulegea. Hapohapo Fareed akamuacha.
“Do you remember this face?” (unaikumbuka sura hii?) aliuliza Fareed huku akimwangalia padri Luke.
“Please! Don’t kill me,” (usiniue tafadhali) alisema padri huku akipiga magoti.
“Do you?” (unaikumbuka?)
“I saw you a while ago,” (nilikuona muda mfupi uliopita)
“Okey! I came to kill you,” (Sawa! Nimekuja kukuua) alisema Fareed huku akimwangalia padri huyo.
“I’ve done nothing! Please! Have mercy, I have done nothing,” (sijafanya lolote! Tafadhali nihurumie! Sifanya lolote) alisema Padri huyo huku akiwa amepiga magoti.
Fareed akaanza kumkumbusha padri huyo kila kitu kilichokuwa kimetokea kuhusu wao. Alianzia mbali, jinsi alivyokuwa ameathirika kwa vitendo vya kishoga mpaka kufikia hatua ya kwenda kanisani hapo kwa ajili ya kuungama dhambi zake.
Padri Luke akakumbuka, akamwangalia vizuri Fareed, akamkumbuka. Akazidi kulia na kuomba msamaha zaidi kwamba kile alichokifanya ni shetani tu ndiye aliyempitia.
Sawasawa mke mweeeLeo tunaimalizia
ShikamooBaby yake naniliu endelea basi
Am proud of you myloveAsante babe ake Davet jamanii... Asante kwa kuniweka busy humu kwa hadithi
SEHEMU YA 158
Alilala mitaani na masikini, hakukuwa na mtu aliyejali, kila mmoja alikuwa na mambo yake, ilipofika siku ya nne huku akiwa mtaani na akiendelea kufanya harakati za kutafuta msaada wa siri kuuondoka nchini humo maumivu ya tumbo yakaanza tena.
Yalikuwa ni maumivu makali, alihisi tumbo lake kama likiungua moto, alitapika madonge makubwa ya damu, wakati mwingine mpaka kwenye makalio yake kulikuwa kukitoa damu hali iliyomuogopesha kupita kawaida.
Kilio chake cha maumivu ndicho kilichowashtua masikini waliokuwa mitaani, walipomfuata na kuona tatizo lake, wakaanza kumpeleka hospitalini huku akiwa hoi, kifua chake kilitapakaa damu kutokana na kukohoa madonge ya damu sana.
Akafikishwa katika Hospitali ya Britain Medical Center ambapo moja kwa moja akapelekwa katika chumba kimoja na kuanza kufanyiwa vipimo. Bado Fareed alikuwa akilia kwa maumivu makali, madaktari ambao walikuwa wakimwangalia hawakumgundua kama alikuwa Fareed, mwanaume aliyeua watu wengi kwa kuwalipua katika kituo cha treni.
Akafanyiwa vipimo na kugundulika kwamba alikuwa na kansa katika utumbo wake mkubwa.
Madaktari wakashangaa, hawakujua sababu iliyomfanya mtu huyo kupata tatizo hilo kubwa ambalo mara nyingi lilikuwa likiwapata watu wenye kula vitu vilivyokuwa na kemikali nyingi kupitiliza.
Walitaka kujua chanzo cha tatizo hilo, wakamwambia kwamba alitakiwa kuchunguzwa kwa ukaribu na kugundulika chanzo cha tatizo hilo ili wajue ni kwa namna gani wangeweza kumsaidia.
Uchunguzi ulifanyika kwa saa kadhaa na kugundua kwamba tatizo kubwa lilisababishwa na mapenzi ya jinsi moja aliyokuwa akiyafanya zamani.
Kilichomletea matatizo ni mafuta ya vilainishi ambayo yalikuwa yakitumiwa na wanaume waliokuwa wakimuingilia kinyume na maumbile.
Mafuta yale vilainishi yalikuwa yakipenya moja kwa moja mpaka kwenye utumbo mkubwa na kuganda huko, utumbo ukaathiriwa na moja kwa moja kumletea tatizo ambalo lilisababisha utumbo huo kushambuliwa na virusi vilivyosababisha kansa.