Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 122

“Nashukuru sana!”
Mzee Al Fakh akaondoka na kwenda chumbani kwake, alipofika, haraka sana akachukua simu yake na kupiga namba fulani. Baada ya kupokelewa tu akaanza kuongea na mtu aliyekuwa upande wa pili.

“Nimefanikiwa kumpata mmoja, anaonekana kuwa na hamu ya kufika nchini Marekani! Ndiyo! Sasa huyo ndiye tutakayembebesha mabomu kwenda kulipua jijini New York katika kituo cha treni cha Pennsylvania.

Haina shida, ataingia kama kawaida na hakuna ambaye atamshtukia, wasiliana na Hassan Bin Latif umpe maelekezo ya kumpokea mtu huyu na kumuelekeza ni kitu gani anatakiwa kufanya. Inshallah!” alisema Mzee Al Fakh na kukata simu.

**** Zaidi ya watu hamsini walifariki dunia katika mgahawa mmoja huko Amsterdam nchini Uholanzi baada ya bomu kulipua eneo hilo lililokuwa limekusanya watu wengi. Hiyo ilikuwa taarifa iliyoishtua dunia, ilikuwa ni idadi kubwa ya watu kuliko milipuko yote ambayo iliwahi kutokea katika nchi za Ulaya.

Watu walikuwa wakiendelea kujitoa mhanga, lilikuwa tukio baya la kujitoa mhanga ambalo lilitokea mwaka huo. Watu walilalamika, kundi la kigaidi la Al Qaeda lilijitokeza hadharani na kutangaza kwamba wao ndiyo walikuwa wamehusika katika mlipuko huo.

Marekani ikachukia, kila siku ilijitahidi kupambana na ugaidi, magaidi walikamatwa na kupelekwa katika gereza lililojaa mateso la Guantanamo lakini ugaidi haukupungua.

Watu wengi, hasa vijana wa Kiarabu walikuwa wakikamatwa, walifundishwa kufanya matukio ya kigaidi huku akili zao zikijengwa kisaikolojia kwamba kuua katika ugaidi hakukuwa dhambi bali ni kuitetea dini.

Vijana wengi wa Kiarabu wakaingia katika mkumbo huo, waliahidiwa mambo mengi kwamba familia zao zisingepata shida tena na kama wangejitoa mhanga siku hiyohiyo wangekuwa peponi, pembeni ya mtume wakifarijiwa kwa kazi kubwa waliyoifanya duniani.

Hiyo ndiyo ilikuwa mbinu nyepesi ya kuwapata vijana wengi na wakafanikiwa hivyo kujitoa mhanga. Dunia ilionekana kubadilika, amani ikapotea, nchi nyingi za Ulaya zikawa na hofu na watu kutoka Mashariki ya Kati kwamba hawakuwa watu wa kuaminika na muda wowote ule wangeweza kufanya mauaji.
 
SEHEMU YA 123

Kwa kipindi kirefu kundi hilo la kigaidi likatamani kulipua Marekani. Walikumbuka jinsi walivyotumia ndege mwaka 2001, hawakutaka kuridhika hivyo kutamani kulipua tena kwani waliamini kwamba wanaonewa, walitaka kuyaondoa majeshi ya Marekani na Uingereza nchi mwao, kitu pekee kuonyesha kwamba walichukizwa na uwepo wao huko kilikuwa ni kuwalipua tu.

Hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza kuingia nchini Marekani. Waliwatumia watu wengi kwenda huko lakini ilishindikana, hata kabla hawajaingia nchini Marekani, walikamatwa na hivyo kufungwa katika gereza la Guantanamo.

Walijiuliza ni sababu zipi ziliwafanya kukamatwa kirahisi namna hiyo na jibu pekee walilolipata ni kwa sababu waliwatumia Waarabu wenzao.

Ili kuingiza bomu nchini Marekani ilitakiwa kumtumia Mzungu au mtu mweusi, hawakujua wangewapata vipi, kwa Wazungu ilikuwa vigumu sana lakini kwa watu weusi halikuonekana kuwa jambo gumu hata kidogo.

Wakakutana nchini Uturuki, nchi pekee barani Ulaya ambayo walikuwa wakikaa kwa usalama kwa kuwa watu wa nchi hiyo walikuwa Waarabu wenzao.

Hapo ndipo walipopanga mipango, wakawafuata watu weusi waliotaka kuingia Marekani, waliwaambia kwamba walikuwa tayari kuwasaidia lakini walipowaambia kuhusu mabomu, waliogopa.

Walipoteza watu wengi, wakaweka vikao na kuona kwamba hawakutaka kuwaambia lengo la kuingia nchini Marekani bali walitakiwa kubaki kimya, wawape mizgo ya mabomu pasipo wao wenyewe kujua.

Kitendo cha Fareed kupatikana kiliwapa uhakika kwamba mwanaume huyo angefanikiwa kuingiza mabomu nchini humo, mawasiliano yakafanyika na hivyo taarifa kupelekwa kwamba tayari kijana mmoja alikuwa amepatikana, kijana aliyekuwa na hamu ya kuingia nchini Marekani.

“Hata mimi ninao wawili huku,” alisikika kijana aliyeitwa Mohammed Mustapha, mwanaume aliyekuwa akipanga safari za kwenda nchi mbalimbali kulipua.
“Safi sana. Basi nitaomba uje kumchukua na huyu,” alisema Mzee Al Fakh.
“Haina shida.”

Fareed hakuwa na hofu, moyo wake ulifurahi mno kwa kuona kwamba hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake ya kuelekea nchini Marekani. Hakuhisi kama watu hao walikuwa wabaya waliotaka kumbebesha mabomu mpaka nchini MArekani.
 
IMG_1672.JPG




Njoo tusherehekee Tumosa
Shunie kesha fika
 
Back
Top Bottom