Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,501
- 911,251
- Thread starter
- #16,821
Simba kuzineemesha Coastal, Lyon
na Dina Ismail
KLABU ya Simba imepanga kuzineemesha baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake, imefahamika.
Hatua hiyo, inatokana na Kamati ya Ufundi ya Simba kupendekeza baadhi ya wachezaji ambao hawakutumika ipasavyo katika msimu uliopita wa Ligi Kuu bara, kutolewa kwa mkopo.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinasema kwamba kamati hiyo imependekeza wachezaji hao kupelekwa timu za African Lyon na Coastal Union ya Tanga.
Baadhi ya wachezaji ambao wamependekezwa kutolewa kwa mkopo ni pamoja na Ali Ahmed Shiboli, Juma Jabu, Salim Aziz Gilla na Meshack Abel.
Mmoja ya wajumbe wa kamati hiyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alisema kuwa pamoja na hilo, wameamua kufanya hivyo ili kunusuru vipaji vya wachezaji hao, ambao walishindwa kungara katika mzunguko wa lala salama wa ligi hiyo.
Tupo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji si kuviua, tunataka kuwatoa kwa mkopo katika timu kadhaa za ligi kama Moro United, African Lyon na Coastal, alisema.
Alisema, pamoja na hilo, wametoa mapendekezo kadhaa ambayo wameyawasilisha katika kamati ya utendaji ambayo inatarajiwa kukutana leo.
Simba ipo katika mkakati wa kuisuka upya timu yake, baada ya kushindwa kutetea ubingwa wa ligi hiyo ambao ulikwenda kwa mahasimu wao wa jadi, Yanga.
Pamoja na hilo, Simba inadaiwa kutaka kuwapiga panga nyota wake mahiri wakiwemo Juma Kaseja, Musa Mgosi, Mohammed Banka, Salum Kanoni, Kelvin Yondan na Rashid Gumbo.

PRINT