Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
TFF yazipiga mkwara klabu Ligi Kuu


Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limezipiga mkwara klabu za Ligi Kuu Bara kusajili wachezaji walio huru kwa mikataba na si vinginevyo.Hadhari
hiyo inatokana na tukio lililotokea msimu uliopita ambapo wachezaji Steven Marashi, Wisdom Ndlovu, John Njoroge na Ally Msigwa wa Yanga waliachwa na mpaka leo hawajalipwa fidia zao.

Suala hilo liliendelea mpaka kufika katika Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji ambapo kama hiyo iliiamuru Yanga, iwalipe na mwezi uliopita wachezaji hao walitishia kusimamisha usajili wa klabu hiyo mpaka walipwe fedha zao.

Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuulizwa kuhusu pilika pilika za usajili zinazoendelea kwa timu mbalimbali nchini, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura alisema usajili rasmi unaanza Juni 20, mwaka huu mpaka Julai 20.

"Kwa mujibu wa kanuni, kipindi cha usajili ni Juni 20 mpaka Julai 20, hivyo katika kipindi hicho klabu inatakiwa isajili mchezaji ambaye yupo huru au klabu yake imevunja mkataba naye.

"Pia ndicho kipindi ambacho klabu zinatakiwa kuweka wazi wachezaji inaowaacha, ili wasajiliwe na timu zingine na zihakikishe zinaingia nao mikataba," alisema.

Wakati huo huo, Wambura aliongeza kuwa timu ya taifa 'Taifa Stars', inatarajia kuondoka kesho kwenda Msumbiji kuumana na timu ya taifa ya nchi hiyo ikiwa na msafara wa watu 30.

Alisema wanatarajia kuumana na Msumbiji Jumamosi katika mchezo wa ufunguzi wa Uwanja wa kisasa wa michezo kama ulivyo wa Taifa, Dar es Salaam na kurudi Jumapili.
 
Usajili Kili Cup kuaanza Aprili 26


Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema usajili wa wachezaji kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Taifa 'Kili Taifa Cup', utaanza Aprili 26, mwaka
huu kwa mikoa yote.

Mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi katika vituo sita vya mikoa mbalimbali nchini kuanzia Mei 7, mwaka huu ambayo yameandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Lager.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura alisema Mei 2 ndiyo siku ya mwisho kwa mikoa kuweka pingamizi ambapo baada ya hapo Kamati ya Mashindano hayo, itakutana siku inayofuata.

"Mei 5 tunatarajia timu za mikoa kuanza safari ya kwenda vituoni tayari kwa mashindano na tuna imani fedha za maandalizi zitakuwa zimewafikia kwani wadhamini TBL, walishaanza kuzitoa," alisema Wambura.

Wakati huo huo, Wambura alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF), limeteua waaamuzi sita nchini kwenda kuchezesha michezo ya awali ya michezo ya Afrika (All African Games), katika nchi mbalimbali zinazowania kufuzu michezo hiyo.

Aliwataja waamuzi hao kuwa ni Waziri Sheha, John Kanyenye na Hamisi Chang'walu ambao watakwenda kuchezesha mchezo kati ya Malawi na Afrika Kusini utakaopigwa jijini Lilongwe Aprili 30, mwaka huu.

Wengine ni kwa upande wanawake ambapo Judith Gamba, Saada Hussein na Mwanahija Makame wao watakwenda nchini Zimbabwe kuchezesha mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo, itakayoumana na Angola katika mchezo utakaopigwa Mei 14, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Wambura alisema timu ya Gaborrone United inahitaji kocha wa kuifundisha timu hiyo kutoka nchini ambapo mwenye sifa anatakiwa awasiliane na TFF, ili kujua taratibu za kufuata.
 
Tamasha la Muziki la Mzalendo Halisi laja tena


na Stella Mushi


amka2.gif
TAMASHA la aina yake la sanaa na muziki asilia wa Tanzania maarufu kama ‘Mzalendo Halisi 2011’ linatarajiwa kuanza kurindima kuanzia Juni 17-19 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo, Cassius Mlewa, tukio hilo linalosherehekea sanaa, utamaduni na muziki asilia, kwa mara ya kwanza lilifanyika Mei mwaka jana, ambako washiriki walifarijika na mvuto wa uasilia katika tasnia hiyo ulioonekana kwenye jukwaa.
Mlelwa alisema kivutio kikubwa kilitoka kwa Wazazi Cultural Troupe, maarufu kama ‘Segere’, bendi ya Wahahapa na wasanii kama Irene Sanga, Che Mundu, Jhikoman, Mrisho Mpoto na Vitalis Maembe.
Mratibu huyo aliongeza kuwa, mwaka huu kunatarajiwa kuwa na vikundi kutoka mikoa ya Mbeya, Dodoma na Morogoro, sambamba na kikundi cha sanaa na utamaduni kutoka Msumbiji.
Pia aliwataja washiriki watakaorudi mwaka huu kuwa ni pamoja na Black Roots, wakiongozwa na ‘Makombora’, bendi yenye msisimko kwenye jukwaa kutoka Zanzibar na Segere.
“Tamasha hili la pili, litaanza siku ya Ijumaa kama ufunguzi rasmi, ambapo kutakuwa na onyesho la bendi mbili na sherehe ya kutoa Ngao Ya Mzalendo. Ngao hii ni maalum kwa kuenzi kazi za muziki na sanaa kutoka kwa wasanii, bendi au vikundi kutokana na mchango wao katika jamii,” alisema.
Aliongeza kuwa, tamasha la mwaka huu pia litapambwa na wasanii wa sanaa za aina mbalimbali, vyakula vya kuvutia, maonyesho ya vitu vya sanaa kama nguo, michezo na vivutio kwa watoto.
Alifafanua kuwa, Juni 17, ambayo itakuwa ni Ijumaa litaanza saa 12 jioni hadi saa 3 usiku, huku siku inayofuata ni saa 4 asubuhi hadi 4 usiku wakati Juni 19 litaanza saa 4 asubuhi hadi saa 3 usiku, ambako viingilio vitatangazwa hivi karibuni.
 
Wizara kukamilisha muswada wa hatimiliki


na Makuburi Ally


amka2.gif
WIZARA ya Viwanda, Biashara na Masoko, imesema iko katika mchakato wa kukamilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya hatimiliki na hakishiriki ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu, Waziri wa wizara hiyo, Cyril Chami, alilisititiza kuwa, serikali inatambua kilio cha wasanii juu ya uboreshwaji wa sheria ya hakimiliki na hakishiriki ya mwaka 1999 na kwamba, jitihada zinafanyika kufanikisha marekebisho hayo.
"Wizara inatambua kilio cha wasanii na inajali maslahi, wasanii ni kundi muhimu na tunalipa umuhimu na umakini unaostahili, kazi zao zinahitaji kulindwa na kuheshimiwa na kumekuwa na jitihada kuhakikisha hilo linafanyika," alisema Chami.
Waziri Chami alibainisha kwamba, kuchelewa kwa mchakato wa kupitisha muswada huo, kunatokana na tofauti zilizopo kati ya makundi mawili ya wasanii, lile la muziki na wa fani nyinginezo, ambazo zitajadiliwa katika kikao baina ya wizara mbili.
Wizara hizo ni ile ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na ile ya Viwanda, Biashara na Masoko.
 
Msondo wairithi rasmi Sikinde


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music ‘Mambo Hadharani', imehamishia rasmi maonyesho yake ya kila Jumapili kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, uliokuwa ukitumiwa na mahasimu wao, Mlimani Park Orchestral ‘Sikinde Ngoma ya Ukae'.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Said Kibiriti alisema kuwa wameishakubaliana kwa maandishi na wamiliki wa ukumbi huo, Shirika la Uchumi na Maendeleo Dar es Salaam (DDC), kufanya shoo kila Jumapili.
Sikinde ilikuwa ikiutumia ukumbi huo kama ukumbi wake wa nyumbani, ikifanya maonyesho ya kila Jumapili tangu mwaka 1978, baada ya kuwa chini ya umiliki wa DDC na ilibadili jina na kuitwaa DDC Mlimani badala ya Mlimani Park la awali.
Kibiriti, aliwaomba mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao kila Jumapili kwenye ukumbi huo wa DDC Kariakoo, kwa kuwa unafikika kwa urahisi hata kwa wale wasio na usafiri binafsi.
"Tunapenda kuwaambia wapenzi wa Msondo Ngoma kuwa kuanzia sasa tumehamia rasmi kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo katika maonyesho yetu ya kila Jumapili," alisema Kibiriti.
Hilo linakuwa pigo la pili la Msondo kuipa Sikinde, kwani hivi karibuni ilimtwaa mwimbaji wa siku nyingi wa Sikinde, Shaaban Dede, ingawa mwanamuziki huyo alianzia Msondo, lakini aliimbia Sikinde kwa muda mrefu, kiasi kwamba sauti yake ilikuwa kama alama ya Sikinde.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom