Simba yauweka Ubingwa rehani
Send to a friend Wednesday, 06 April 2011 21:39 0diggsdigg
Washambuliaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi na Mbwana Samata akiwania mpira huku beki wa JKT Ruvu akiwachini na wengine akijiandaa kuupokea wakati wa mechi la Ligi Kuu iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam/picha na Jackson Odoyo.
Sweetbert Lukonge
SIMBA ya Dar es Salaam jana ilijikuta ikilazimisha sare ya 1-1 na JKT Ruvu katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na hivyo kutibuliwa harakati zake za kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Mpaka hivi sasa Simba imefikisha pointi 46 ikiwa imebakiza mchezo mmoja ikifuatiwa na Yanga ambayo inacheza leo dhidi ya African Lyon huku ikiwa na pointi 43 na mchezo mmoja mkononi.
Kwa matokeo hayo, kama Yanga itashinda leo itafikisha pointi 46 sawa na Simba, lakini Simba itakuwa ikiongoza ligi hiyo kwa kuwa na idadi ya magoli mengi ya kufunga.Hivi sasa mechi za mwisho za ligi hiyo ndizo zitakazoamua nani bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2010/11.
Simba ambayo ilitolewa na TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Jumapili iliyopita baada ya kuchapwa mabao 3-2 ilianza mechi hiyo ya Ligi Kuu dhidi ya JKT bila kasi, ila katika dakika ya sita mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan'Mgosi' alikosa bao alipopiga shuti ambalo lilitoka nje baada ya kipa wa JKT Ruvu, Shaaban Dihile kupangua shuti la Mbwana Samata.
Hussein Bunu aliipatia JKT Ruvu bao katika dakika ya 26 baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Pius Kasambale.Mpaka mapumziko JKT Ruvu walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0, huku katika kipindi cha kwanza washambuliaji wa Simba wakiongoza kwa kukosa mabao kwa sababu walikosa nafasi tisa za wazi.
Simba walianza kipindi cha pili kwa kasi huku wakionekana kutaka kusawazisha bao, lakini ukuta wa JKT Ruvu ambayo ina pointi 26 ulikuwa imara kukataa kuruhusu bao lolote.
Iliwachukua Simba mpaka dakika ya 79 kusawazisha bao hilo ambalo lilifungwa na Emmanuel Okwi kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa JKT Ruvu kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Katika mechi hiyo kipa wa JKT Ruvu, Shaaban Dihile alipewa kadi nyekundu baada ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na beki wa timu hiyo Kessi Mapande ambaye alikuwa akicheza beki wa kulia kwa sababu JKT ilikuwa imemaliza kuingiza wachezaji wa akiba.
Pia katika dakika ya 82 mwamuzi Klina Kabala alimtoa mchezaji wa JKT Ruvu, George Minja kwa kadi nyekundu baada ya mchezaji huyo kumpiga ngumi mshambuliaji wa Simba, Ally Mohamed Shiboli.
Akizungumzia pambano hilo kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda amewaponda waamuzi kwa maamuzi yao mabaya yaliyoonyesha wazi kuibeba Simba.Kocha wa Simba, Patrick Phiri alisema timu yake ilipata nafasi nyingi za wazi na kushindwa kuzitumia, ila anajipanga kwa ajili ya mechi ijayo.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Comments
0
#6 addie 2011-04-07 12:29 naamini timu ya jeshi ni timu ya kuonyesha nidhamu miongoni mwa timu zote ktk mashindano yoyote yale.. jkt jana wameonyesha nidhamu ndogo sana n wanapaswa kufungiwa. tuache unazi lets face the facts.
Quote
0
#5 mark 2011-04-07 12:15 mimi nilikuwepo mpirani na sikuona makosa ya refa ni yapi kwani kjt walitaka mwamuzi awasikilize wanavyotaka hata km wanamakosa msilaumu kwa ushabiki tu wa usimba na uyanga wachezaji wajkt walikuwa hawananidhamu
Quote
-1
#4 kivatiro 2011-04-07 10:59 KWA KWELI SOKA LA TANZANIA HALITAWEZA ENDELEA KAMWE BILA YA SHIRIKISHO LETU KUAMKA NA KWENDA NA WAKATI.WAAMUZI WETU NDIO WANAOCHANGIA KWA ASILIMIA 100 KUAU SOKA LETU.REFA WA JANA ANASTAHILI KUADHIBIWA KWA KUCHAPWA VIBOKO KABISA.HATA KAMA UNAMAPENZI NA TIMU FULANI NA UNATAKA KUIBEBA BASI BEBA KWA KUSOMA NYAKATI SI KUBEBA KWA HALI HIYO NI AIBU KUBWA SANA.TIMU INABEBWA IKIINGIA KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA NA KUVURUNDA VISINGIZIO VINGI KWELI ILIHALI IMEBEBWA.HIVYO TFF IANGALIE SWALA ZIMA LA WAMUUZI WETU ILI TUWEZE PIGA HATUA KATIKA SOKA LETU.
Quote
0
#3 aggrey akaro 2011-04-07 10:10 soka la bongo kichefu chefu tu,kama nilivyoona soka hili ni tofauti sana na jinsi linavyo zungumziwa kwenye vyombo vya habari.Soka halina fomesheni halina ladha utafikiri ni sarakasi.kwa maana hiyo soka la bongo halitafika mahali popote ni uchafu mtupu.ukitaka kuhakikisha hilo kama mliangalia jana man na chelsea au baca na shaka,utagungud ua hapa bongo ni maneno tu????
Quote
0
#2 Paschal Rweyemamu 2011-04-07 08:17 kwakweli mechi ilikuwa nzuri na ilikuwa ngumu, binadamu yoyote ameumbwa na saikolojia zinazofanana, ila uvumilivu ndo tunaozidiana. ndipo mana hata ziddane alishindwa uvumilivu. refa wa jana aliikwaza timu ya jkt na yote ni ktk kufanikisha kile alichoadhimia, kumbuka wale wanaofanyiwa ni binaadamu na wakijua fika lengo ni nn.
Nachoweza kusema Physcology ya muamuzi wa jana ni ndogo sana, na ndo mana waliichezea saikoljia yake mpaka akamaliza mpira kabla ya muda kwakuwa alishindwa kuhandle Pressure toka upande mmoja.
Ni lazma refa aangalie kwanza mechi anayochezesha ni ya hatua ipi ktk ligi, mfano tutakumbka ilikuwa ni Brazil na Ivory coast. na Brazil ilikuwa itolewe, mchezaji wa Brazil aliunawa live, na hakufanya chochote kwakuwa madhara yake yangeweza kumharubia status yake milele.
Nahitimisha kusema refaree wa jana aliharibu mchezo kwakuwa hana uwezo wa kuchezesha mechi ngumu kulingana na uwezo wake mdogo wa kufikiri.
Nitaomba ifanyike shule ya Physcology kwa mwaka mzima kwa marefaree wote, na anayefeli asitishwe kazi hiyo.
Quote
0
#1 Mohamed Hassan 2011-04-07 07:18 Shaaban Dihile ni kipa hodari sana kwani aliisaidia timu yake kuikosesha simba ushindi,aliokoa hatari nyingi golini mwake,naweza kusema alikuwa "man of the match" lakini aliaribu pale alipotolewa nje ya uwanja kwa kadi nye[NENO BAYA] kwa kutoa lugha ya [NENO BAYA] kwa mwamuzi.Shaaban punguza jazba na nidhamu inaitajika kwenye soka.you are good in goalkeeping.