Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Obren, Nadir kutua Azam Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 20:07

Mwandishi Wetu
MATAJIRI wa jiji, Azam wameanza mapema kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumnasa kipa wa zamani wa Yanga, Obren Circovick.

Akithibisha usajiri wa nyota huyo mwenyekiti wa Azam, Mohamed Said alisema wamemsajili kipa huyo baada ya kumkosa Mghana, Yew Berko aliyeongeza mkataba na Yanga.

Mbali na Obren pia Azam imefanya mazungumzo na beki wa Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' na kufikia makubaliano binafsi na Cannavaro aliyebakiza mwaka moja na Yanga.

"Mama yake Nadir anataka mwanaye acheze Azam kwa vile ana undungu na mwenyekiti wa Azam na sasa wapo tayari kulipa dau kubwa kwa Yanga ili imnyakue mchezaji huyo,"alisema mmoja wa viongozi wa Yanga.

Akifananua jambo hilo Nadir alisema,"Mimi ninachoangalia ni maslahi, haya ni maisha na hii ni ajira yangu kama watamalizana mimi nipo tayari kuichezea Azam hata sasa," alisema Cannavaro muda mfupi baada ya kuzungumza na mama yake kwa njia ya simu kuhusiana na suala la yeye kujiunga na Azam.

Kwa upande wa pili Azam inadaiwa kuwa ipo mbioni kuwatupia virago nyota wake watatu ambao ni Ramadhani Chombo 'Redondo', Kali Ongala na kipa Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi.
 
Simba kibaruani tena leo

Na Zahoro Mlanzi

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, timu ya Simba, leo itajitupa tena uwanjani kuumana na maafande wa JKT Ruvu katika mchezo utakaopigwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili.

Simba itashuka uwanjani ikiwa na machungu ya kuondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na mabingwa watetezi wa michunao hiyo, TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemnokrasi ya Congo (DRC) kwa jumla ya mabao 6-3.

Timu hiyo itashuka uwanjani ikiwa na lengo moja la kuibuka na ushindi na kama ikishinda itafikisha pointi 48 na kubakiwa na pointi mbili tu, iweze kutetee ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo.

Simba ikifikisha pointi 50 hakuna timu yoyote itakayoweza kuzifikia pointi hizo kwani Yanga, ambayo ipo nafasi ya pili kwa pointi 43 ikishinda michezo miwili iliyobaki itafikisha pointi 49.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya TP Mazembe, alisema sasa nguvu anazielekeza katika michezo miwili iliyobaki kwa kuhakikisha wanatwaa ubingwa.

Alisema kutwaa ubingwa wa ligi hiyo, itarudisha morali kwa timu yake baada ya kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa na itafungua njia kwa ajili ya kujipanga kwa mwakani.

Kwa upande wa timu ya JKT Ruvu, yenyewe haina chakupoteza kwani ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 26 hivyo haina cha kuwania wala hatihati ya kushuka daraja, kwa hiyo itakuwa ikijiimarisha katika msimamo wa ligi hiyo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Charles Kilinda akizungumzia mchezo huo, alisema timu yake siku zote inacheza soka la kufundishwa na haitakuwa tayari kufungwa na Simba, kwani wanachozingatia ni kupata rekodi nzuri.
 
Ngasa, Kigi waongezwa U-23 Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 20:05

Kalunde Jamal
KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, Jamhuri Kiwhelu 'Julio' ameongeza wachezaji saba katika kikosi chake ili kukiongezea nguvu kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kutafuta nafasi ya kucheza mashindano ya Olimpiki dhidi ya timu ya Cameroon utakaofanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya kocha huyo msemaji wa Shirikisho la soka nchini, Boniface Wambura alisema kulingana na umuhimu wa mchezo huo kocha wa timu hiyo ameongeza wachezaji saba katika kikosi hicho.

Wambura aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mrisho Ngasa kutoka katika timu ya Azam ,Kigi Makasi wa Yanga ,David Luhende kutoka katika timu ya Kagera Sugar ,Jabiri Azizi wa Azam, Calvin Charles wa Simba Ally Lundenga wa Kagera Sugar na Juma Abdul wa mtibwa Sugar.

"Kulingana na umuhimu wa mchezo huo mwalimu ameona aongeze nguvu kwa kuwaita wachezaji hao, Kwa kuwa kigezo cha kucheza katika timu ya vijana ni umri hivyo hilo la kuwaongeza wachezaji hao siyo tatizo,"alisema Wambura.

Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaza viingilio vya mechi hiyo ambapo kiingilio cha juu kitakuwa ni shilingi 10,000 na kiingilio cha chini ni shilingi 1000.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mashabiki watakaokaa kwenye viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa ndio watalipa shilingi 1000.

Alifafanua kuwa mashabiki watakaokaa VIP B na C kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000 na jukwaa la VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000.

Alisema kuwa tiketi za mchezo huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa taifa kuanzia saa kumi jioni zinauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo ,Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ,Mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora na Ohio.Aidha aliyataja maeneo mengine ambayo tiketi hizo zinauzwa kuwa ni pamoja na Big Bon Msimbazi Kariakoo na Uwanja wa Uhuru.

Alisema kuwa timu ya Kameroon imewasili juzi saa tano usiku na ndegeya Kenya Air Ways ikiwa na wachezaji 23 na imefikia katikas Hoteli ya Paradise
iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam na itakuwa inafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
 
Barca itaiweza Shakhtar leo? Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 20:02

BARCELONA, Hispania
WAKATI timu ya Barcelona imejiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania kwa mara ya tatu mfululizo, leo itakuwa na kibarua kikali wakati itakapoingia uwanjani kwa ajili ya kupambana na Shakhtar Donetsk katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola ameiwezsha timu hiyo kufanya vizuri tangu aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 2008 na hivi sasa Barca ipo kwenye mwisho wa msimu ikitaka kutwaa makombe matatu.

Guardiola alichukua kazi ya kukinoa kikosi cha Barca baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Frank Rijkaard kushindwa kuipa mafanikio timu hiyo na kusimamia nidhamu ya wachezaji wa timu hiyo kuanzia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, pia Guardiola aliikuta timu ipo katika hatua ya kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Katika msimu wake wa kwanza, kocha Guardiola aliiwezesha Barca kutwaa mataji sita na mwaka jana waliweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania na Kombe la Copa del Rey, lakini hawakuweza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutolewa na Inter Milan iliyokuwa ikifundishwa na na kocha Real Madrid hivi sasa Jose Mourinho.

Katika mechi ya ligi kuu ya Hispania waliyocheza Barca dhidi ya Villarreal na Barca kushinda bao 1-0, wachezaji wao Carles Puyol, Eric Abidal, Maxwell Pedro Rodriguez kwa sababu ya kuwa majeruhi, Xavi Hernandez pia hakucheza na Leo Messi alianza mechi hiyo akiwa benchi.

Pedro anatarajiwa atakuwepo katika mechi ya leo dhidi ya Shakhtar Donetsk, pia Messi na Maxwell wanatarajiwa kuwepo, lakini Puyol anaweza asiwepo hivyo ukuta wa Barcelona unatarajiwa kusimamiwa na Sergio Busquets na Gerard Pique.

Barca ambayo inatarajiwa kucheza pia mechi ya fainali ya Copa del Rey mwishoni mwa mwezi huu, mshambuliaji wake mahiri David Villa alidai kuwa wiki chache zijazo ni muhimu kwa mafanikio ya klabu hiyo.

"Hatua tuliyofikia sitakubali tutwae makombe mawili kati makombe matatu tunayowania, tunazo mechi ngumu mbele yetu, tunatakiwa tuifunge Shaktar Donetsk katika mechi ya kwanza tunayocheza nao katika uwanja wetu wa nyumbani ili tusiangaike tutakaporudiana nao,"alisema David Villa.

Barca inatarajia kuifunga Shaktar Donetsk kwa mara ya tisa katika Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shaktar Donetsk kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Mwaka 2009, Barca iliifunga Shaktar Donetsk katika mashindano ya Uefa Super Cup, lakini mara ya mwisho zilipokutana Shaktar Donetsk na Barcelona, timu ya Shaktar Donetsk ilishinda kwa mabao 3-2.
 
Barca itaiweza Shakhtar leo? Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 20:02 0diggsdigg

Similar Discussions

Back
Top Bottom