Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Watoto 500 Tamasha la kuadhimisha Siku ya Malaria


Na Zahoro Mlanzi

WATOTO zaidi ya 500 wa jijini Arusha, wanatarajiwa kushiriki katika tamasha la mpira wa miguu la kuadhimisha siku ya Malaria duniani litakalofanyika kesho
kwenye Uwanja wa Sheikh Amr Abeid, jijini humo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Mradi wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Furaha Kabuye alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa soka kama Benki ya NMB na Kiwanda cha A to Z, wameamua kuendesha kliniki ya watoto itakayohusisha wanafunzi wa shule za msingi tu.

Alisema wanafunzi hao watashiriki mchezo huo kwa nyakati tofauti, ikiwa na lengo la kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani ambao umekuwa ukiuwa watu wengi kwa kipindi kifupi.

"Kilele cha maadhimisho hayo ni Aprili 25, mwaka huu ambapo barani Afrika mtoto mmoja hupoteza maisha kila baada ya sekunde 30 ambapo pia husababisha umasikini kwa jamii kutokana na kuharibu nguvu kazi katika jamii," alisema Kabuye.

Alizitaja shule zitakazoshiriki tamasha hilo ni Sanawari, Mwangaza, Daraja, Meru, Levolosi, Engosengu, Unga na Makumbusho ambapo michezo hiyo itakuwa chini ya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Jan Poulsen.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo, Sunday Kayuni alisema alikishukuru chuo hicho na kwamba watatumia nafasi hiyo kuhakikisha wanaandaa utaratibu kwa wanafunzi hao kuendelezwa.

Alisema watawaalika makocha mbalimbali wa jiji la Arusha kwenda kuangalia vipaji vya wanafunzi hao na kwamba wanafunzi watakaoshiriki watapatiwa vyeti na vyandarua kila mmoja.
 
Wilaya ya Ilala yaingukia Serikali


Na Tumaini Maduhu

OFISA Utamaduni Manispaa ya Ilala, Shani Kitongo ameiomba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kuisaidia wilaya hiyo kifedha ili iweze kuibua vipaji
katika Manispaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya changamoto zinazoikabili Manispaa hiyo, Shani alisema wilaya hiyo imeshindwa kutimiza malengo yake katika kuhakikisha inaibua vipaji na kukuza michezo kutokana na ufinyu wa bajeti waliyonayo.

Alisema ili wilaya hiyo iweze kufika mbele na kupiga hatua, Serikali na wadau mbalimbali wa michezo nchini wanatakiwa waiunge mkono katika kuichangia kwa mawazo na fedha ili iweze kupiga hatua.

``Mimi mwenyewe, Ofisa utamaduni sina gari wala bajeti yoyote ya kwenda kuwatembelea wadau wangu, bali ninalazimika kutumia mguu wangu kwa kuwa nina mapenzi na Watanzania wenzangu hususani katika kuhakikisha tunainua na kuibua vipaji vya michezo.

Katika hatua nyingine, Kitongo alitoa mwito kwa wasanii kutoa taarifa pale wanapopata mialiko ya kwenda sehemu mbalimbali nchini ili pale watakapopata matatizo iwe rahisi katika kuyatatua.

``Sisi wenyewe, wasanii ni mashahidi tumejionea wasanii wanapopata matatizo hata huko walipo inakuwa shida kuwasaidia kutokana na kutokufuata taratibu maalumu zakusafiria,`` alisema Kitongo.
 
Rooney afungiwa mechi mbili Send to a friend Tuesday, 05 April 2011 20:01

LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amefungiwa kucheza mechi mbili za Ligi Kuu ya England baada ya kushangilia bao kwa kutukana katika kamera za televisheni zilizokuwa zikirekodi pambano hilo.

Rooney ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa England baada ya kufunga penati ambalo lilikuwa ni bao lake la tatu katika mechi alizifuata kamera zilizokuwa zikirekodi pambano hilo na kutukana mbele ya kamera hizo.

Katika mechi hiyo Manchester United iliichapa West Ham mabao 4-0.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la England FA ilisema," FA leo imemfungia mchezaji wa Manchester United, Wayne Rooney kwa sababu ya kutukana."

Kama Rooney akikubali tuhuma hizo atafungiwa kucheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Fulham ambayo ni mechi ya Ligi Kuu ya England na ile ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City iliyopangwa kufanyika Aprili 16.

Kama Rooney akipinga tuhuma hizo, kesi yake hiyo itasikilizwa na tume maalum ya FA ambayo inaweza kutoa adhabu kubwa.

Hata hivyo baada ya mechi hiyo ya Manchester united dhidi ya West Ham Kumalizika, Rooney alisikitikia kitendo chake cha aina ya ushangiliaji aliouonyesha na pia televisheni ya Sky Sports iliyoonyesha mechi hiyo iliwaomba msamaha watazamaji wake kwa kitendo hicho kilichoonyeshwa na Rooney.

Rooney ambaye ni mchezaji bora wa mwaka wa England msimu uliopita amekuwa na wakati mgumu msimu huu kwa sababu ya matatizo yake binafsi, kuwa majeruhi na kiwango chake kupungua.

Lakini katika wiki za hivi karibuni aameanza kuonyesha kiwango kizuri huku akifunga mabao tisa katika mashindano yote aliyocheza tangu mwezi Februari.
 
Villa yatangaza kumuuza Ashley Young


LONDON, England

TIMU ya Aston Villa imeitaarifu Manchester United, kuhusu mchezaji ambaye inamnyemelea, Ashley Young kuwa ina mpango wa kumuuza msimu huu.Awali
vyanzo vya habari vilikuwa vikieleza kuwa Villa, imeshaamua kutomruhusu Young, kuondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya Manchester United kuonesha nia ya kumsajili ili akakipige kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.

Lakini hata hivyo inaelezwa kuwa baada ya kumwachia aondoke bure, wakati wa usajili wa msimu wa 2012, Villa inaona ni bora ikamuuza kwa kitita cha pauni milioni 12.

Inaelezwa licha ya kuwa hadi sasa Villa imeshapokea ofa za kumtaka Young kutoka Manchester United na Liverpool, lakini inaamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atajiunga na Sir Alex Ferguson.
 
Azam yaiva Polisi Send to a friend Monday, 04 April 2011 22:22

Jessca Nangawe
MATAJI wa jiji Azam leo wanashuka dimbani kujaribu bahati yao dhidi ya Polisi Tanzania katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu mchezo utaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Azam iliyopoteza matumaini ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya kufungwa na Yanga itaingia uwanjani kwa lengo moja la kushinda ili iweze kubaki katika nafasi yake ya tatu au kusubiri miujiza ya Simba na Yanga kupoteza michezo yake.

Mchezo huo muhimu kwa pande zote mbili utazidi kuziweka timu hizo katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi ambayo inafikia tamati mapema mwishoni mwa juma hili.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wao mwenyekiti wa Azam,Idrisa Nasoro amesema wamejiandaa vyema kukabiliana na Polisi licha ya kushindwa katika mchezo uliopita watahakikisha hawapotezi tena mchezo huo.

Alisema wamepoteza matumaini ya kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kutibuliwa na Yanga na kukubali kichapo cha magoli 2-1, lakini watahakikisha wanashinda ili kubaki nafasi ya tatu.

Kwa upande wa kocha wa Polisi, John Simkoko amesema wamejiandaa vyema kushinda katika mchezo huo na lengo lao ni kuona wanakuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom