Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,501
- 911,251
- Thread starter
- #14,461
TFF yafuta matokeo mechi ya Yanga, Azam
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 31st March 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 929; Jumla ya maoni: 0
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limefuta matokeo ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa Machi 30 kati ya Yanga na Azam zote za Dar es Salaam.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yote yakifungwa na Jerry Tegete, huku lile la Azam likifungwa na
John Bocco.
Taarifa zilizopatikana jana jioni baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Mashindano
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilieleza kuwa uamuzi huo ulitokana na Yanga kumtumia
beki Shadrack Nsajigwa akiwa na kadi tatu za njano.
"Ni kweli tumemaliza kikao muda huu, Azam walikata rufani na kwa kuwa wajumbe wote walikuwa Dar es Salaam na kwa vile Yanga ilishapewa angalizo kabla ya mechi isimtumie Nsajigwa, uamuzi ukafikiwa haraka," alieleza Boniphace Wamaru ambaye ni msemaji wa kamati hiyo, lakini akasema maelezo zaidi aulizwe Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Alipoulizwa Osiah alijibu kwa kifupi: "Wewe umepata taarifa hizi wapi? Aliyekueleza mwambie akufafanulie vizuri," alisema na kukata simu.
Hata hivyo baadaye Osiah alituma ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi kuwa leo shirikisho
hilo litafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia jambo hilo.
Lakini kwa mujibu wa mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo, walikuwa na mabishano ya muda mrefu huku wengine wakitaka Azam ipewe ushindi, lakini wakafikia uamuzi wafute
kwanza matokeo na kuwa uamuzi zaidi kama itarudiwa au la utatolewa na Kamati ya Nidhamu
ya TFF.
Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu alipoulizwa jana alisema wamepata taarifa hizo na kuwa hawatakubali kupokwa pointi ama mchezo kurudiwa kwani Nsajigwa hana kadi tatu za njano.
"Hizi ni njama za Simba, hatujapata barua bado lakini tunawaomba wanachama wote kesho (leo) saa mbili asubuhi tukutane klabuni, tujadili uamuzi huu wa uonevu.
"Tutaandamana kupinga mambo haya, Simba wanaona tumewakuta wanaanza fitina," alisema Sendeu.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alipoulizwa alisema wao hawana sababu ya kuiwekea
fitina Yanga kwani wana uhakika watashinda mechi zao mbili zilizobaki, hivyo wataibuka na
ubingwa na wanachofanya sasa ni kujiandaa na mechi yao na TP Mazembe keshokutwa.
"Liko wazi kwamba Nsajigwa ana kadi tatu za njano, tena TFF imekosea Azam inatakiwa ipewe
pointi, mbona kanuni ziko wazi?
Yanga inabebwa katika hili," alisema Rage, ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini. Yanga baada ya juzi kuifunga Azam ilifikisha pointi 43 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Simba inayoongoza ikiwa na pointi 45.
Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 37. Zote zimecheza mechi 20, hivyo kwa kufutwa matokeo hayo ina maana Yanga sasa ina pointi 40.
*Leo ni Siku ya Wajinga.

PRINT