Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #11,761
Zomboko aponda utaratibu wa tuzo
na Shehe Semtawa
Mchambuzi maarufu wa muziki wa dansi nchini, Rajabu Zomboko, amesema haridhishwi na utaratibu wa kupiga kura ili kuwapata washindi wa tuzo za ‘Kili awards'.
Zomboko aliiambia Tanzania Daima kuwa mtindo huo wa kupiga kura kwa kutumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu umekuwa ukitoa ushindi kwa watu ambao hawana uwezo kimuziki.
Alisema kinachofanyika pale ni kudanganyana kutokana na kwamba baadhi ya washiriki wana uwezo kifedha hivyo hutumia ushawishi wao kwa kuwaongezea pesa jamaa zao kwenye simu zao ili watume ujumbe mra nyingi.
Aidha, Zomboko alibainisha kuwa wale wenye uwezo wa kuimba wamekuwa wakikosa tuzo kutokana kwamba hawana uwezo wa kuwaingizia fedha jamaa zao kwenye simu zao ili wawapigie kura kwa wingi.
Zomboko alisema kwa upande mwingine utaratibu uanaotumika umekuwa ukiwanufaisha zaidi makampuni ya simu kadiri ujumbe unavyotumwa kwa wingi huku washindi wakipata fungu dogo.
"Unajua ile ni biashara ya wajanja wachache ambao wanajinufaisha wenyewe kwani ujumbe unaotumwa ni mwingi sana ingawa sina uhakika ujumbe ni kiasi gani," alisema Zomboko.
Zomboko alisema mwanamuziki wa kweli hapatikani kwa kupigiwa kura bali wanapambanishwa jukwaani na kuonyesha vitendo kama enzi za nyuma zilivyokuwa zinapambanishwa bendi mbalimbali za muziki wa dansi.