Spurs yajizatiti kumaliza kazi kwa AC Milan Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 19:49 0diggsdigg
LONDON, Uingereza
KLABU ya Tottenham Hotspur imejiandaa kuonyesha mashabiki wake kwamba imeiva wakati ikiikabili AC Milan katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo.
Katika mchezo huo, Spurs inataka kuendeleza ubabe dhidi ya klabu za Milan, baada ya awali kuiadhiri Inter katika hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mabao 3-1 baada ya awali kufungwa 4-3 mjini Milan.
Msimu huu, mashabiki wa Spurs wamefurahia matokeo ya timu yao inayoshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa Ulaya ambako ilifunga mabao 18 katika hatua ya makundi.
Katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa San Siro, Spurs ilionyesha ukomavu wa kuilaza Milan 1-0 na leo inahitaji kukamilisha hilo kwa ushindi ili kucheza robo fainali.
Bao safi la Peter Crouch ugenini linaipa timu hiyo faida katika mchezo wa leo jijini London.
Kocha Harry Redknapp, ambaye aliiongoza Spurs kuiadhiri Inter 3-1 katika makundi, amedhamiria kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri zaidi
ìUnapokuwa na faida ya baola ugenini, hutaki kukaa chini na kulemaa unatakiwa kuangalia mbele kwa mafanikio makubwa zaidi ili kuepuka aibu," alisema.
ìTunatakiwa kuingia uwanjani kana kwamba hatujashinda. Si kawaida yetu kulemazwa na matokeo ya bao 1-0, tunasubiri dakika zote 90.
ìTutacheza zaidi mchezo wa kushambulia tangu mwanzo, hivyo ndivyo tutacheza.î
Katika mchezo wake wa mwisho, Spurs ilitoka sare ya 3-3 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumapili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Jumapili, matokeo ambayo kocha Redknapp alisema yanakatisha tamaa, ingawa alifurahia kurejea kwa winga wake Gareth Bale akicheza kwa dakika 20 na pia Jermain Defoe akipachika mabao mawili.
Bale, ambaye aliitesa Inter nyumbani na ugenini alikuwa majeruhi, kiasi cha kukosa mechi kwa wiki sita akisumbuliwa na tatizo la mgongo , lakini leo ataanza mchezo huo kusaidia mashambulizi akimsaidia Aaron Lennon.
Mshambuliaji Rafael van der Vaart, ambaye amekuwa nyuma ya mafanikio ya timu hiyo tangu ajiunge nayo msimu huu, anatakiwa kuwa fiti kucheza mchezo huo baada ya kuwa majeruhi.
Defoe aliyefunga mabao mawili Jumapili amejiwekea lengo la kufunga bao leo ili afikishe mabao 100 kwa klabu hiyo ambako safu ya ushambuliaji itasaidiwa pia na Roman Pavlyuchenko naCrouch .
Vinara hao wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A wameshinda mechi tatu za ligi kabla ya kuivaa Spurs, lakini watawakosa wachezaji wao kadhaa kutokana na kuumia.
Miongoni mwao ni kiungo Kevin Prince Boateng ambaye huenda akaikosa Spurs aliyoichezea akiwa England. Tayari, Milan inawakosa viungo wake, Andrea Pirlo na Massimo Ambrosini walio majeruhi na, Mark van Bommel hawezi kucheza kwa kuwa alikuwa Bayern na Gennaro Gattuso amefungiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Huenda kocha Massimiliano Ambrosini akawachezesha katika kiungo, Clarence Seedorf, Mathieu Flamini na kinda wa Kijerumani, Alexander Merkel au beki wa kati Marek Jankulovski akisogezwa mbele.
Mshambuliaji Alexandre Pato anatarajiwa kuwa fiti kucheza badala ya Antonio Cassano.
Comments
0
#2 CHADEMA-DAMU 2011-03-09 13:29 Milan wakiwa kwenye Win or die march wanatisha isivyo kawaida.Milan inashinda leo...
Quote
0
#1 shallamar 2011-03-09 10:38 we waache hao spurs tupo london leo mtaona moto wetu wazee sie kama msemavyo.
vita mbele sisi uzoefu tunao wakutosha.
mtabakia kinywa wazi hatutegeme refa kama
barcelona jana penalt wamepewa ile card
nye[NENO BAYA] mapema. FORZA MILAN
Quote