Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Alex Msama afuta tamasha Mwanza


na Mwandishi wetu


amka2.gif
WARATIBU wa tamasha la Pasaka wameamua kulifuta tamasha la Mwanza na sasa tamasha hilo litafanyika katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma na Shinyanga pekee.
Mwenyekiti wa Kamati ya Msama Promotions waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa jijini Dar es salaam tamasha hilo litafanyika Aprili 24 na mjini Dodoma litafanyika siku ya Aprili 25 ambayo ni Jumatatu ya Pasaka na Shinyanga litafanyika Aprili 26.
Alisema sababu za kufuta onyesho la Mwanza zimekuwa nje ya uwezo wao hivyo wakawaomba radhi wapenzi na mashabiki wa nyimbo za Injili kwa kufutwa kwa onyesho hilo la Mwanza.
"Tunasikitika kwamba tumelazimika kulifuta tamasha la Mwanza, tunawaomba radhi wote ambao wameathiriwa na kufutwa huko lakini tunawaahidi kuboresha katika maeneo ambako litafanyika," alisema Msama.
Aliwaomba wapenzi wote wa nyimbo za Injili kujitokeza kwa wingi siku ya Pasaka Aprili 24, ambapo tamasha hilo litafanyika kwenye Ukumbi wa Dimond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Msama alisema tamasha la Pasaka la mwaka huu litashirikisha waimbaji kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, DR Congo, Afrika Kusini, Zambia na Tanzania na lengo lake kubwa ni kukusanya fedha za kuwasaidia watoto yatima pamoja na mitaji ya wanawake wajane kote nchini.
Aidha, pia fedha zitakazopatikana kutokana na matamasha hayo zitatumika kuwasaidia wahanga wa mabomu yaliyotokea katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
 
Kuziona Simba, Yanga 3,000


na Makuburi Ally


amka2.gif
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara baina ya mahasimu wa jadi nchini Simba na Yanga unaotarajia kupigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kwamba katika mechi hiyo kiingilio cha chini kitakuwa sh 3,000 ambacho kitahusu watakaokaa viti vya kijani mzunguko, ambavyo vina uwezo wa kuchukua watazamaji 19,648 na cha juu VIP A ni sh 30,000 ambavyo vina uwezo wa kuchukua watazamaji 748.
Wambura alitaja viingilio vingine kwa kuwa ni sh.5,000 kwa viti vya bluu mzunguko ambavyo vina uwezo wa kuchukua watazamaji 17,045, huku watakaokaa viti rangi ya chungwa vinavyoingiza watazamaji 11,897 watalipa sh 7,000, wakati VIP C yenye viti 4,060 watalipa sh 10,000 na VIP B lenye viti 4,160 watalipa sh 20,000.
Wambura aliongeza kuwa tiketi hizo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho kuanzia saa mbili asubuhi katika vituo vya mbalimbali ikiwemo Shule ya sekondari Benjamin Mkapa, Big Bon Msimbazi na mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio na Uwanja wa Uhuru.
"Pia siku ya mchezo zitaendelea kuuzwa katika maeneo hayo kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana na baada ya muda huo zitaendelea kuuzwa katika Uwanja wa Uhuru pekee", alisema Wambura.
Wambura alisema Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam ndiye atakuwa mwamuzi wa mechi hiyo akisaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Maxmillian Nkongolo wa Rukwa, huku mwamuzi wa mezani atakuwa Hashim Abdallah, wakati kamishna atakuwa mchungaji, Army Sentimea wa Dar es Salaam.
 
Nchunga amlamba miguu Manji


na Juma Kasesa


amka2.gif
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jjijini Dar es Salaam umeamua kumuangukia aliyekuwa mjumbe wa bodi ya udhamini na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuf Manji, ili kuinusuru na anguko la uchumi ambalo linaweza kuikumba klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Llyod Nchunga, alisema maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Februari 28, mwaka huu ambapo walikubaliana kumuangukia Manji.
Alisema maamuzi hayo yalitokana na kutambua mchango wake mkubwa aliokuwa akiutoa kwa klabu hiyo kupitia kampuni yake ya Quality Media Group na ufadhili katika usajili na masuala mengine yanayohusu timu.
Aliongeza kuwa kamati hiyo ilisisitiza kufanyika kwa jitihada mbalimbali za kumrejesha mfadhili huyo kwa maelewano mapya ya kibishara ili kupanga namna ya kuendelea kuisadia klabu hiyo ambayo kwa mwaka inahitaji shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kujiendesha.
Alifafanunua kuwa kiasi hicho cha pesa kinahusisha shilingi milioni 600 za usajili, milioni 50 kwa ajili ya mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi, watumishi wa utawala na gharama za umeme na maji huku Yanga ikiingiza shilingi milioni 212.4 kupitia mkataba wa udhamini na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Nchunga alisema kupitia mchanganuo huo ni wazi Yanga inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mapato, kwani kiasi kikubwa cha fedha kilikuwa kikitolewa na Manji kwa takriban miaka mitano, hivyo ni pigo kubwa kwa klabu hiyo kumkosa mfadhili huyo.
Alisema wakati jitihada za kumrejesha mfadhili huyo zikiendelea uongozi wake umelazimika kubuni na kukaribisha vyanzo vipya, ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu kwa ajili ya mashabiki wa klabu hiyo ili kuweka amana.
Aidha, Nchunga alisema Kamati ya Utendaji imeridhia kupelekwa kwa majina yote ya wanachama wakorofi katika mkutano mkuu wa klabu ambao walihusika katika kutoa maneno ya kumfedhehesha Manji kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Aliongeza kuwa kamati hiyo imeona kuna umuhimu wa Manji kuendelea kuifadhili timu hiyo kutokana na Yanga bado ilikuwa haijakomaa katika kujitegemea.
Hivi karibuni Manji alitangaza kujiondoa katika shughuli za klabu hiyo kutokana na kitendo cha baadhi ya wanachama kumtolea maneno ya kashfa kabla ya uongozi wa klabu hiyo kumuangukia mara mbili kwa kumuandikia barua kumuomba abadilishe uamuzi wake, lakini akagoma.
 
Tawi la Simba launda kamati ya ushindi


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KATIKA kuelekea mechi ya watani wa jadi itakayozikutanisha Simba na Yanga ambayo imepangwa kupigwa keshokutwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tawi la Simba Shibamu Magomeni limeunda kamati ya ushindi ya watu wanne ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
Ofisa Habari wa tawi hilo, Mao Lofombo, alisema kamati hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Yassin Mwete, itakuwa na jukumu la kushirikiana uongozi wa juu wa Simba ili kupata ushindi katika mchezo dhidi Yanga na ule wa kimataifa na TP Mazembe ya Congo.
Aliwataja wajumbe wanaounda Kamati hiyo kuwa ni Chuma Selemani, Ally Bachu na Ramadhani Sudi ambapo watatumia uzoefu walionao katika masuala ya soka katika kuweka mipango ya Simba kushinda michezo hiyo.
Kwa upande wake Bi Chuma , ambaye ni mzoefu na mechi za Simba na Yanga, alisema , atatumia mbinu walizotumia mwaka 1977 kuifunga Yanga bao 6-0 huku Ramadhani Sudi, akisema kipigo walichokipata watani zao hao katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar hivi karibuni kitajirudia ili kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Katika kikao hicho wanachama wengi wa Tawi hilo ambalo ndilo la kwanza kuanzishwa Tanzania Bara, walionyesha matumaini makubwa kwa Simba kushinda michezo hiyo kutokana na kiwango cha soka kinachoonyeshwa na timu hiyo katika mashindano mbalimbali yanayoendelea.
 
Awadh, Ashraf sasa Machi 12


na Samia Mussa


amka2.gif
PAMBANO la ndondi la kimataifa baina ya mabondia, Awadh Tamim na Ashraf Suleiman lililokuwa lifanyike keshokutwa kwenye ukumbi wa DDC Mlimani Park, Mwenge jijini Dar es Salaam limesogezwa mbele hadi Machi 12.
Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Aurora inayoandaa pambano hilo, Shomari Kimbau alisema kusogezwa kwa pambano hilo kunatokana na siku hiyo kuwepo kwa mechi baina ya Simba na Yanga.
Alisema wameona ni muhimu kulisogeza ili kutoa fursa kwa wadau wa michezo kwenda kushuhudia mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao wanatarajiwa kuzipiga katika pambano la raundi kumi uzito wa Heavy, ambapo Awadhi anatetea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati.
Kimbau alisema pambano hilo litatanguliwa na michezo kadhaa ya kirafiki ambapo David Mrope atazipiga na Swedy Wilson ‘Kiza Kinene', Amour Mzungu akizichapa na Ramadhani Kido, Suleiman Said atazidunda na Said Yazidu, huku Benson Mwakyembe akipigana na Dickson Joseph.
 
Yanga sasa 'kumwangukia' Manji


Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa Yanga umepanga kufanya jitihada za kuhakikisha zinamshawishi mfadhili wake ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Udhamini, Yusuf Manji ili
kumrejesha baada ya kuamua kujiuzulu nyadhifa hizo.

Pia uongozi huo umepanga kuelewana naye upya hata kama ni kibiashara.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga alisema Februari 15, mwaka huu Manji aliwasilisha barua kwenye Kamati ya Utendaji ya kujiuzulu katika nyadhifa zake, baada ya baadhi ya wanachama kumkashifu.

Nchunga alisema kutokana na hatua hiyo ya Manji kujiuzulu, Kamati ya Utendaji iliamua katika kipindi hiki wakati mfadhili huyo akiwa hayupo watalazimika kubuni na kukaribisha vianzio ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti maalumu kwa ajili mashabiki wa Yanga kuchangia.

Alisema pia kamati hiyo ilitoa tamko kulaani vitendo vya kashfa ambavyo viongozi wamekuwa wakituhumiwa akiwemo Manji na ikakubaliwa kupeleka majina ya wanachama wakorofi katika Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

"Kimsingi maazimio ya mkutano wa matawi na Kamati ya Utendaji ni kwamba bwana Manji bado tunamhitaji

Alisema baadhi ya wanachama wa klabu hiyo mwezi uliopita waliitisha mkutano na kuthubutu kumfedhehesha Manji audilifu wake ndani ya Yanga, kitendo ambacho kilimvunja moyo mdhamini huyo na kuamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu.

"Kabla ya kunikabidhi barua nilitumia uwezo wangu wote kumsihi asitishe azima yake lakini alikataa, pia makundi mbalimbali ikiwa pamoja na wazee walimsihi nadhani kuna mambo watakuwa wamekubaliana kwa manufaa ya Yanga, yaani kurejea kwake katika nyadhifa zake," alisema Nchunga.

Alisema siku hiyo hiyo, aliyokabidhiwa barua na Manji aliwaita viongozi wa Kamati ya Utendaji na moja kwa moja katika ajenda yao ilikuwa ni kuwapa taarifa za tukio la kujiuzulu kwa mdhamini huyo.

Nchunga alisema kamati kwa mara nyingine tena ikaamua kumuandikia barua Manji, ili asitishe uamuzi wake pia wapate fursa ya kuonana naye kuongelea suala hilo, hata hivyo Manji aliijibu barua hiyo na kusisitiza msimamo wake kukaa kando.

Mwenyekiti huyo alisema hatua hiyo ilimfanya aitishe mkutano wa matawi ambao ulifanyika Februari 26 mwaka huu na ajenda kubwa ilikuwa ni suala la Manji kujiuzulu, kitu kilichowashtua viongozi wa matawi.

Aliongeza kwamba Yanga kila mwaka inahitaji takribani sh. bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeshea mambo mbalimbali ya klabu.

 
Simba Temeke wataka jihadi Jumamosi


Na Andrew Ignas

UONGOZI wa matawi ya Klabu ya Simba Wilaya ya Temeke umewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanacheza kwa jihadi katika mechi ya
Ligi Kuu dhidi ya watani wao jadi Yanga itakayopigwa Jumamosi ili washindi na kutoka kifua mbele.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam juzi Katibu wa matawi hayo, Hussein Simba alisema wachezaji wao wanatakiwa kujituma katika mchezo huo kama fainali.

"Nachotaka kuwaomba wachezaji wa Simba ni kuhakikisha mchezo wetu dhidi ya watani wetu Yanga, tunautumia vizuri ili tuweze kurudi kileleni," alisema.

Alisema licha ya ushindi mzuri waliopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, lakini wanachotakiwa kuangalia zaidi mbio za ubingwa.

Hata hivyo Katibu huyo amewataka wachezaji kuwa na ushirikiano wa hali na mali katika mechi hiyo, badala ya kutegeana uwanjani.




1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... mnapiga kelele mambo kibao utafikiria kuna ti za maanaoooooooo vijitim vyenyewe feki ubabaishaji tu havina mbele wala nyuma maendeleo hakuna tim zina zaidi ya miaka 40 ubabaishaji tu nashanga mtu mzima na akili yake eti anataka hata kupigana au kujaribu hata kupoteza uhai wake sababu ni mshabiki wa simba au yanga hainiingii akilini
March 2, 2011 8:42 PM
 
AFC yakiri Ligi Kuu ngumu kwao


Na Addolph Bruno

BAADA ya kuchapwa mabao 4-2 na JKT Ruvu juzi, uongozi wa Klabu ya AFC Arusha umekiri kwamba uwezo wao ni mdogo katika Ligi Kuu
Tanzania Bara.

AFC inayoshikilia mkia katika ligi hiyo, ina pointi 11 ambapo imebakiwa na mechi nne dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba, Kagera Sugar na Polisi Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya JKT, Mwenyekiti wa AFC Peter Temu alisema baada ya matokeo hayo sasa nguvu zao wanazihamishia katika michezo iliyosalia.

"Kweli hali yetu si nzuri, lakini hii si sababu ya sisi kushindwa kufanya vizuri, ukizingatia tuna michezo minne mpaka sasa, ambayo tutacheza kufa na kupona tushinde," alisema.

Alisema kama watashinda michezo hiyo yote watakuwa wamefikisha pointi 23 kutoka pointi kutoka 11 walizokuwa nazo sasa ambazo zinaweza kuwanusuru na kushuka daraja.

Kuhusu mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Mwenyekiti huyo alisema wachezaji wake hawakutulia, ingawa walikuwa na uwezo wa kuibuka na ushindi ambapo hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo alikuwa na upungufu wake.

"Siwezi kulisemea sana hilo la mwamuzi, huu ndiyo mpira wa nchi hii ninachoweza kusema mwamuzi hakuwa anatenda haki kwa sababu katika penalti mbili, tumepewa moja na nyingine ikapotezewa," alisema
 
Mechi ya watani wa jadi:TFF yatarajia mavuno nakubwa ya Sh373 m Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 20:03

wamburatff.jpg
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura

Clara Alphonce

WAKATI homa ya mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga ikizidi kupanda na timu hizo mbili zikiingia mafichoni kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kuingiza kiasi cha Shilingi 373,688,000 katika mchezo huo endapo mashabiki 57,558 watajitokeza na kuingia uwanjani.

TTF imesema inatarajia kupata fedha hizo baada ya jana kutangaza viingilio vya mechi hiyo, ambapo kile cha juu kitakuwa Sh30,000 na cha chini kikiwa Sh3,000.

Mchanganuo huo wa TFF unaonyesha kuwa viti vya kijani mzunguko kiingilio chake ni Sh 3,000 na wataingia watu 19, 648, viti vya bluu mzunguko wataingia watu 17,045 kwa kiingilio cha Sh 5,000, rangi ya chungwa, viti 11,897 kwa kiingilio cha Sh7,000,

Vingine ni VIP C , viti 4,060 kwa kiingilio cha Sh10,000, VIP B viti 460, kiingilio Sh20,000 na VIP A viti 748 kwa kiingilio cha Sh30,000. Jumla wanatarajiwa kuingia mashabiki 57,558.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa wameweka viingilio hivyo vidogo ili watu wengi wa hali zote za kimaisha waweze kuona mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki.

Alisema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho katika vituo mbalimbali na mauzo hayo yataendelea hadi Jumamosi wakati tiketi zitakapoletwa uwanjani kuanzia saa 6:00 mchana wakati mechi hiyo itaanza saa 10:00 jioni.

Wambura aliwataja waamuzi wa mchezo huo kuwa ni Oden Mbaga ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Maxmilian Nkongolo kutoka Rukwa. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hashim Abdallah na kamishna wa mechi hiyo ni Mchungaji Amy Sentimea.

Wakati hilo likiendelea, timu hizo mbili zimekwenda mafichoni ambapo Simba wao waliondoka Jumatatu jijini Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wakati wapinzani wao, Yanga waliondoka juzi jioni kwenda Bagamoyo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na pande zote mbili kuzidiana kwa pointi moja moja katika msimamo hadi sasa. Simba inataka kutetea ubingwa wake huku Yanga wakidhamiria kuwavua ubingwa huo.
 
Yanga bila Manji yateseka kimapato Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 20:00

Sweetbert Lukonge

UONGOZI wa klabu ya Yanga unahangaika kusaka vianzio mbadala ya mapato ili kuiendesha klabu hiyo baada ya kujitoa kwa mdhamini na mfadhili, Yussuf Manji.

Kwa kuanzia, uongozi huo umepanga kuwahamasisha wanachama wake kuchangia maendeleo ya klabu hiyo kupitia akaunti maalum ya amana ambayo itaiwezesha klabu yao kupata Sh 1.2 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya uendeshaji.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga alisema jana kuwa ili kukabiliana na upungufu huo ndani ya klabu hiyo, uongozi wake umelazimika kubuni na kukaribisha vianzio vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na akaunti maalum kwa ajili ya mashabiki wote.

Nchunga alisema kuwa klabu hiyo imekuwa ikipata Sh 212.4 milioni kila mwaka kwa njia ya mkataba wa udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambazo ni sawa na Sh 17.7 kila mwezi kwa mkataba huo unaomalizika Aprili mwaka huu.

Alisema fedha nyingine kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitolewa na Manji kwa takribani miaka mitano na pia amekuwa akitoa misaada mingine midogo midogo katika klabu hiyo.

Alisema Sh 500 milioni zimekuwa zikitumika kwa ajili ya usajili wa wachezaji kwa mwaka wakati kiasi kingine cha Sh100 m hutumika kwa ajili ya gharama za usajili wakati wa dirisha dogo.

"Ukiachana na fedha hizo, pia kiasi cha Sh 32 milioni kwa mwezi hutumika kwa ajili ya mishahara ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

"Shilingi 10m nyingine kila mwezi hutumika kwa mishahara ya watumishi mbalimbali wa utawala wakati Sh8milioni nyingine hutumika kwa ajili ya maji, umeme na gharama nyinginezo ndani ya klabu yetu," alisema Nchunga.

Nchunga alisema kujiondoa kwa Manji ndani ya klabu hiyo ni pengo kubwa kwa klabu hiyo kwa sababu msaada wake ulikuwa bado ukihitajika katika kipindi hiki ambacho timu hiyo ilikuwa kwenye hatua changa kuelekea kujitegemea.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa Manji atabakia kuwa mtu muhimu katika klabu hiyo na wanachama wa timu hiyo wanatakiwa waelimishwe umuhimu wa kuheshimu wafadhili, wadhamini na uongozi kwa ujumla.

Pia, wajiepushe na uvunjaji wa katiba na kuongeza kuwa kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa yeyeyote anayekiuka katiba.
 
Emima yaendelea kugawa pointi Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 19:58

Salome Millinga
TIMU ya soka ya Evergreen, imejitutumua na kuifunga Emima mabao 3-1 katika mechi kali ya Ligi ya Soka ya wanawake mkoa wa Dar es Salaam, mchezo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Ligi hiyo ambayo kwa sasa imekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa mashabiki kuhudhuria kwa wingi kutokana na kuongezeka kwa ushindani kwa timu hizo.

Evergreen ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la wapinzani wao na ilipata bao la kwanza katika dakika ya 14 lililofungwa na Mwapewa Mtumwa baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Emima.

Mwapewa aliyekuwa akiisumbua ngome ya wapinzani wao, alipachika bao la pili dakika ya 33 baada kumlamba chenga beki wa Emima, Sakina Nyumba.

Vumilia Maarifa alifumania nyavu za Emima katika dakika ya 62 kwa bao safi baada ya kuzidi maarifa mabeki wa Emima. Bao la Emima lilifungwa na Fatuma Salum dakika ya 34.

Akizungumza na Mwananchi kocha wa Evergreen, Daud Shanga alisema: "Timu imefanya vizuri katika mechi ya leo (juzi) na imeonyesha upinzani mkubwa ila waamuzi bado wamekuwa tatizo kubwa.

"Ukilinganisha na michuano iliyopita timu yangu haikuwa na inafanya vizuri ili mwaka huu timu imeonyesha upinzani mkubwa na mategemeo yetu kuchukua ubingwa wa mkoa wa Dar es Salaam mwaka huu kwa sababu timu yangu ina uwezo mkubwa."

Naye kocha wa Emima, Mwenzerim Omary alisema: "Kupoteza mchezo huu ni bahati mbaya kwa sababu timu yangu imecheza vizuri mwanzo hadi mwisho na wachezaji wameonyesha kiwango."
 
U-23 ya Julio yakamilika Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 19:57

Kalunde Jamal
WACHEZAJI watakaounda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kutoka Zanzibar wamejiunga na wenzao wa Bara kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya awali kuwania kufuzu Michezo ya Olimpiki itakayofanyika kwenye jiji la London, England Agosti mwakani.

Kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' aliiambia Mwananchi jana kuwa kwa sasa wachezaji wameshaingia kambini tayari kwa maandalizi hayo isipokua wachezaji wa klabu za Simba na Yanga.

Julio alisema wachezaji wanaounda timu hiyo wako 44 na watachujwa hadi kufikia 25 watakaokwenda katika mashindano hayo.

"Maandalizi yameanza na timu imeangia kambini katika hoteli ya Bamba Beach nje kidogo ya jiji...kuhusu mechi za kirafiki tayari tumewasiliana na TFF ambao kwa sasa wapo katika harakati za kututafutia," alisema Julio.

Alipoulizwa kuhusiana na suala la kuitafutia mechi za kirafiki timu hiyo ya U-23, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura alisema bado kamati ya maandalizi inalishughulikia na mechi zuitachezwa kati ya Machi 13 na 20 na mashindano yataanza Machi 26.

 
Ferguson amtishwa zigo la lawama mwamuzi Atkinson Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 19:56

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amemlalamikia mwamuzi Martin Atkinson aliyechezesha mechi yao dhidi ya Chelsea juzi usiku kuwa ndiye aliyesababisha timu yake ifungwe mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Ferguson alimlaumu Atkinson kwa kutoa penalti ya utata ambayo iliipa Chelsea bao la ushindi, pia akimlaumu mwamuzi huyo kwa kushindwa kumtoa uwanjani beki David Luiz ambaye aliyemchezea faulo Wayne Rooney.

"Unakuwa na matumaini ya kupata mwamuzi bora katika mechi kama hii, ilikuwa ni mechi kubwa kwa klabu zote mbili, unatakiwa kuwa na mwamuzi ambaye atachezesha kwa haki, mwamuzi imara, lakini hatukuwa na mwamuzi wa aina hiyo, sijui kwa nini mechi ilimshinda. Kabla pambano halijaanza nilipomuona mwamuzi niliogopa, niliogopa sana,"alisema Ferguson.

"Yalikuwa ni maamuzi magumu kuyapokea, faulo aliyecheza Luiz ilikuwa ni mita sita au nane mbele ya mwamuzi huyo , lakini hakufanya maamuzi, sijui alikuwa akifanya nini uwanjani kwa sababu ile penalti aliyotoa haikuwa ya haki, Chris (Smalling) alichukua mpira, lakini mchezaji huyo wa Chelsea aliacha mguu kwenye miguu yake ( Chris) akaanguka, haikuwa penalti,"alisema Ferguson.

Aliongeza,"Mwamuzi alikuwa na maamuzi ya ajabu, Chicharito alifanyiwa faulo na Luiz, tena refa alikaa kimya, pia Rooney alifanyiwa faulo na mwamuzi huyo alikaa kimya, maamuzi hayo yalibadilisha mechi yote halafu mwamuzi huyu ataendelea kuchezesha kila wiki!,"alishangaa Ferguson.

Ferguson aliongeza,"Lakini, nimefurahishwa sana na wachezaji wangu,walionewa sana na mwamuzi, lakini walipambana,walifanya walichoweza, walitengeneza nafasi nzuri, hawakustahili kushindwa.

Alipoulizwa kama Chelsea hivi sasa watakuwa wamerudi kwenye harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, Ferguson alisema,"Kama watakuwa wanafanyiwa maamuzi ya namna hii watabadilisha kila kitu, wamefanyiwa maamuzi mengi ya ajabu ambayo yamenishangaza sana."

Katika mechi hiyo, beki wa kati wa Man Unted , Nemanja Vidic alionyeshwa kadi nyekundu, huku beki mwingine wa timu hiyo, Rio Ferdinand akiwa bado majeruhi.

"Sidhani kama Rio atakuwa amepona na kuweza kucheza katika mechi dhidi ya Liverpool, nadhani atacheza Wes Brown

Akimzungumzia mwamuzi wa pambano hilo, kocha wa Chelsea, Carlo Ancelotti alisema,"Kulikuwa na mambo mengi yanatokea uwanjani, hivyo siyo rahisi kwa mwamuzi kufanya maamuzi mara kwa mara, inaweza ikawa David Luiz pia alikuwa na bahati kwa sababu yanatokea mambo mengi na mwamuzi mengine huyaacha."

"Mwamuzi huwa anafanya maamuzi, lakini huwa sipendi kuhukumu maamuzi ya mwamuzi,"alisema Ancelotti.

Kocha huyo aliongeza ,"Luiz alikuwa kwenye kiwango cha juu kabisa, alifunga pia bao muhimu ambalo lilibadilisha mchezo, kweli huyo pia ni mchezaji mzuri."

Akizungumzia kuachwa kwa pointi 12 na Man United katika msimamo wa ligi, Ancelotti alisema,"Ni pointi niyngi, tumeachwa mbali, lakini ushindi tulioupata ni muhimu na umetuongezea kujiamini, tunafikiria kurudi katika nafasi za juu hivi karibuni."

Ancelotti, pia alikiri kuwa Man United ilikuwa vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini vijana wake waliweza kupambana.
 
Fifa yaridhia uwanja wa Corinthians kuchezewa 2014 Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 19:46

SAO PAULO, Brazil

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa, Fifa limepitisha mpango wa klabu ya Corithians na kukubali uwanja wake mpya kutumiwa katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zitakazofanyika Brazil.

Hata hivyo, katika taarifa hiyo Fifa haikueleza kama uwanja huo wa Corinthians utatumika katika mechi ya ufunguzi.

Fifa ilipanga mechi ya ufunguzi ichezewe kwenye mji wa Sao Paulo, lakini mipango hiyo imeshindikana baada ya uwanja wa Morumbi kukataliwa kwa sababu ya kukosa fedha za uhakika za kuuboresha.

Mapendekezo ya Corinthians ya kujenga uwanja mpya yalipewa kipaumbele mwezi uliopita baada ya maofisa wa jiji la Sao Paulo kutangaza mpango mpya wa kulipa kodi.

Mpango huo ambao ni kama motisha kwa ajili ya kuchochea mpango wa Corinthians wa kujenga uwanja utakaochukua mashabiki 65,000 badala ya 48,000.

Sao Paulo ambao ni mji mkubwa nchini Brazil ulikuwa hauna mradi wa uwanja mkubwa.

Wiki iliyopita kundi la wakaguzi wa Brazil lilisema nchi hiyo inatakiwa kuboresha miundombinu yake ya viwanja vya ndege, barabara na viwanja kabla ya fainali za 2014.

Kundi hilo la wakaguzi ambalo linafanya kazi ya kuikagua serikali inatumia vipi fedha za umma, pia liliwalaumu maofisa wengi wa serikali ya nchi hiyo kwa kushindwa kubana matumizi na kushindwa kufanya kazi kwa uwazi.

Taarifa ya wakaguzi hao inasema mwaka 2011 ni mwaka mzuri wa kuanza kuishughulikia miradi mikubwa kabla ya kufanyika kwa fainali za Kombe la Dunia 2014, lakini imekuta bado kuna matatizo mengi katika miji yote 12 ya nchi hiyo ambayo itaandaa fainali hizo.

Kundi hilo lilitoa onyo hilo baada mchezaji mkongwe wa nchi hiyo Pele pamoja na Raisi wa zamani wa Fifa, Joao Havelange kuelezea umuhimu wa maandalizi wa mashindano hayo makubwa duniani.
 
Carlo: Title still out of reach


RivalsDM



PRINT RSS

7 comments »

Updated Mar 2, 2011 7:36 AM ET
Carlo Ancelotti ruled out the prospect of Chelsea producing an amazing late comeback in the title race despite the win over Manchester United.
The Blues won a highly-controversial game at Stamford Bridge on Wednesday night, denting United's bid to deposing them as champions and keeping their own paper-thin hopes of retaining their crown alive.


But the 2-1 victory was too little, too late as far as manager Ancelotti was concerned as he claimed Champions League qualification was now the only realistic target for Chelsea.
"We are too far from Manchester United," said Ancelotti, whose side are now fourth in the table, 12 points adrift of United with a game in hand.
"It's difficult for them to lose points in the next few games.
"We have to concentrate on ourselves and look not too far in the future.
"I cannot believe we are this far behind, but we have to be honest.
"This is where we are in the table, and United have played with more consistency than us."
Chelsea could close the gap to nine points if United lose at Liverpool on Sunday and they win at Blackpool the following evening.
And with a trip to Old Trafford to come and Sir Alex Ferguson's men also yet to visit Arsenal, there is still the tiniest glimmer of hope for the faltering champions.


Midfielder Frank Lampard, who netted the winner last night with a controversial penalty, said on Sky Sports: "We just had to win the game, close the gap and send out a signal that we're still fighting.
"There's still a long way to go - Manchester United are still deservedly top of the league at the moment."
Having written off Chelsea's title challenge, United boss Ferguson last night joked bitterly that they might get back into it if they continued to benefit from the kind of refereeing decisions that went their way in the second half.
It was debatable whether Chris Smalling had tripped Yury Zhirkov for the winning penalty or whether the Russian had stuck his own leg out to ensure contact was made with the defender.
But there was no doubt David Luiz - who had equalised with his first Chelsea goal - should have been shown a second yellow card for a cynical trip on Wayne Rooney two minutes before the spot-kick.
Ancelotti admitted Luiz may have been lucky to escape but refused to comment on referee Martin Atkinson's performance.
He said: "The referee took some decisions, but I don't want to judge them."
Of the all-action display of £25million January signing Luiz, Ancelotti added: "He scored an important goal, the key to the game, and he's a very good player."
Ancelotti also shrugged off another goalless outing from his other January capture, £50million man Fernando Torres.
He said: "Ask him, not me, if it will affect him but I don't think it will."
 
Carrick: Quick response needed


RivalsDM



PRINT RSS

182 comments »

Updated Mar 2, 2011 8:45 AM ET
Michael Carrick is sure Manchester United will bounce back from the disappointment of losing to Chelsea when they face Liverpool on Sunday.
The Red Devils' grip on top spot in the Premier League was loosened as they slipped to a 2-1 defeat to reigning champions Chelsea at Stamford Bridge on Tuesday night.


The result leaves them four points clear of nearest rivals Arsenal, having now played a game more, and with a series of tricky fixtures still to come.
A trip to Anfield to face fierce rivals Liverpool is next on the agenda and it will not be easy to return to winning ways against a side that has shown considerable improvement under Kenny Dalglish.
However, Carrick fully expects United to respond in the right manner and is relishing the opportunity to play another big game so quickly.
"At the moment we feel pretty down, but we can move on quickly. We have to," the midfielder told MUTV.
"We're used to doing that and we're normally good at that, so hopefully we can bounce back again.
"We have to get rid of this game, forget about it and move on. It's obviously a huge game on Sunday and we'll be ready for that. We have to be.

Mon., Feb. 28
AC Milan 3-0 Napoli | Recap
Tue., Mar. 1
Chelsea 2-1 Man United | Recap

Wed., Mar. 2
Arsenal 5-0 Leyton Orient | Recap
Sat., Mar. 5
Arsenal vs. Sunderland
Man City vs. Wigan
Juventus vs. AC Milan
Sun., Mar. 6
Liverpool vs. Man United
Wolves vs. Tottenham
Lazio vs. Palermo
Inter Milan vs. Genoa
Fox Soccer Scores | Video | Photo


"That's the nature of the beast. We move on and we take a lot of positives from tonight and look to put things right that didn't go well. We'll be ready."
Sir Alex Ferguson criticised referee Martin Atkinson after the final whistle at Chelsea and Carrick agrees that the key decisions went against United.
The 29-year-old was also frustrated by the way his side lost their way somewhat in the second half after taking the lead through Wayne Rooney's fine strike in the opening period.
David Luiz equalised for the Blues in the 54th minute before Frank Lampard blasted home a late penalty to seal United's demise.
"It is disappointing, especially after the first half and the way we played," Carrick reflected on the result.
"We were in control. Second half we weren't as quick and decisive in our passing as we were in the first half, but we still felt quite comfortable and I still thought we might score again.
"Some decisions didn't go our way and we're on the end of a defeat, which is very hard to take.
"That type of decision plays a huge part in the game. Big decisions you've got to get right, especially in a game of this importance, so we're disappointed.
"What can I say apart from that? It's hard to take."
Meanwhile, United defender John O'Shea has claimed Ryan Giggs could still be playing at 40.
Giggs has now completed 20 years as a first-team player and even though many of Giggs' team-mates have been around Old Trafford for some considerable time themselves, they are lost in admiration for the 37-year-old.
And, having signed a one-year contract extension earlier this year, O'Shea feels Giggs could carry on for at least another three years.
"Without a doubt," said the Republic of Ireland star.
"His physical shape hasn't changed since I've known him and he looks after himself so well.
"Depending on injuries he could easily carry on, although I am sure he just wants to take it one season at a time.
"He is just enjoying it so much at the minute so I can't see why he can't but I'll let him decide on that."
If nothing else, Tuesday night's game allowed Giggs to equal Sir Bobby Charlton's record of 606 league appearances, another record in addition to the scores the Welshman already has.
Indeed, in the modern era, the only player O'Shea can think of that is remotely comparable is recently-retired Italian legend Paolo Maldini.
"You see how the manager has built squads and Giggsy has been a vital part of every single one of them," he said.
"It's just incredible. Maldini springs to mind with AC Milan but I think Giggsy has even gone past him.
"The speed and the balance he still shows to go past whether it be an old, experienced defender or a new, up-and-coming young strong defender is incredible.
"Every cliche in the book has been used about the man already and I am sure they will be said many times again.
"He is an absolute legend."
 
Neuer's United link resurfaces


RivalsDM



PRINT RSS

18 comments »

Updated Mar 2, 2011 8:54 AM ET
Schalke chairman Clemens Tonnies has claimed Manchester United are interested in signing goalkeeper Manuel Neuer.
Sir Alex Ferguson is looking for a replacement for Edwin van der Saar with the 40-year-old Dutchman retiring at the end of the season.

TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

Neuer is Germany's number one and, at 24, already one of the most highly-rated goalkeepers in Europe.
Tonnies told the Bild newspaper: "An international agent approached me and informed me that Manchester United are interested in Neuer.
"If Manchester United make a written inquiry then we will deal with it."
Neuer's contract with the Royal Blues expires next year and there would be no shortage of suitors should he choose to move on.
Bayern Munich are long-standing admirers and coach Louis van Gaal on Tuesday openly declared his interest in the player.



PRINT RSS




Member Comments

Please note by clicking on "add a comment" you acknowledge that you have read the Terms of Use and the comment you are posting is in compliance with such terms. Be polite. Inappropriate posts may be removed by the moderator.
LOG IN TO ADD A COMMENT Page 1 of 2 PREV PREV NEXT NEXT


Post Comment


  • Report Abuse rotwiessessen222
    • 3/2/2011 9:41:40 PM
    Rooney gets 250,000 a week, no wonder Man United are in debt.
  • Report Abuse pYn.0905_1990ca.FCB
    • 3/2/2011 6:01:43 PM
    KOAN NEUER!!!!!! KOAN NEUER!!!!!
  • Report Abuse Zidane510
    • 3/2/2011 5:05:16 PM
    A German at United? Not happening.
  • Report Abuse henryuja
    • 3/2/2011 4:43:08 PM
    did anyone see the match today Nuer is a beast, I say the only spending Fergie should do this summer is on a CAM and Nuer
  • Report Abuse DRIZZ_IS_M.I.A
    • 3/2/2011 1:55:25 PM
    we are failing to remember that, while yes VDS does have some gas left in the tank, he does have a sick wife. He can get a job as a GK coach for any team in the world and can be closer to his family when they need him. Neuer is quality for sure and I would love to have the Berlin Wall come to Old Trafford
  • Report Abuse redevil_83
    • 3/2/2011 1:44:25 PM
    'ron freak' wazza earns $250k a wk at man united now. yeah. sad.
  • Report Abuse futbolman15
    • 3/2/2011 1:39:08 PM
    Van der Sar still looks like he has got quite a bit of soccer left in him. I think man utd should look to get lloris.
  • Report Abuse canadianunleashed
    • 3/2/2011 12:33:15 PM
    I have to agree with you Barca_v history VDS has been excellent even yesterday game he was awesome between the post if it wasn't for stupid ref handing giving Chelsea a win... I was hoping VDS would get man of the match.
  • Report Abuse ronaldinho_freak
    • 3/2/2011 12:19:08 PM
    woody im sorry bro but im afraid ur statment will be invalid in the next 2 years as bayern will become the richest club in europe..um u and lots of ppl here including some bayerns have failed to realize that the only debts bayern have is the allianz arena which luckly its debts being paid by audi and addidas soo the gaint of fc bayern not just a successful football club but we have a great business image and acpects....look at it this way tooo wayne rooney gets paid 90000 a week vs ribery 150000 a week soo if bayern wana snatch neuer man u barca and madrid have to conceder bayern clout...ask schwini...ribery and lahm why they did not leave bayern even tho they were # 8 on the table.....good luck....bayern till i die
  • Report Abuse Barca-v-History
    • 3/2/2011 10:54:06 AM
    I think SAF should ask Edwin to stick around for another season or two. The past couple of games hes been a beast.
LOG IN TO ADD A COMMENT Page 1 of 2 PREV PREV NEXT NEX
 
Duisburg beats Cottbus to reach German Cup final


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

0 comments »

Updated Mar 1, 2011 5:15 PM ET
Duisburg advanced to the German Cup final after holding on with 10 men to beat Energie Cottbus 2-1 in a match between two second-division teams on Tuesday.

The home of the best LIVE soccer and rugby awaits at FoxSoccer.tv -- don't miss a second of the action.

Stefan Maierhofer put Duisburg ahead in the 24th minute, and captain Srdjan Baljak doubled the lead in the 54th.
Duisburg defender Bruno Soares was sent off in the 77th for a foul in the penalty area. Nils Petersen converted the resulting penalty, and Cottbus missed several late chances to level the match.
Duisburg will play either Bayern Munich or Schalke, who meet Wednesday.
The final is on May 21 in Berlin.
 
Schalke stuns Bayern 1-0 to reach German Cup final


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

25 comments »

Updated Mar 2, 2011 5:44 PM ET
Raul Gonzalez scored in the 15th minute to lift Schalke to a 1-0 victory over title holder Bayern Munich in the semifinals of the German Cup on Wednesday.
Raul's goal put Schalke in the May 21 final in Berlin against second-division Duisburg.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

Bayern lost a German Cup game at home for the first time in 20 years and suffered a second straight setback at home after losing 3-1 to Bundesliga leader Borussia Dortmund, a result that all but left Bayern without hope of defending the championship title.
"A betting man would have made a lot of money by betting on Schalke tonight," Schalke coach Felix Magath said. "We could have scored another goal in the first half, but in the second half we only defended. I was hoping that Bayern wasn't that fresh after two tough games."
Bayern is on the verge of reaching the quarterfinals of the Champions League after beating Inter Milan 1-0 in Italy. Inter beat Bayern in last season's final.
"It's a great disappointment for my players," Bayern coach Louis van Gaal said. "That's football, one team only defends and counterattacks and scores. We played with a lion's heart in the second half but we were unlucky.
"And we should have been awarded a penalty," van Gaal added, referring to an incident late in the game when Atsuto Uchida appeared to bring down Bayern striker Mario Gomez
Raul's goal was a powerful header into the roof of the net. Jefferson Farfan's corner was headed to the far post by defender Benedikt Hoewedes and Raul connected with a powerful header for the lead.
Raul had another opportunity in the 19th but drove wide.
The Spaniard then set up Farfan's solo run but the Peru striker's attempt was smothered by Bayern goalkeeper Thomas Kraft.
Hoewedes had another header in the 35th, but Thomas Mueller cleared on the line.
Bayern's first big opportunity came two minutes into the second half but Arjen Robben failed to connect with a cross from Danijel Pranjic.
Bayern stepped up the pace and Bastian Schweinsteiger had his header stopped by Manuel Neuer, the Schalke and Germany goalkeeper, before Robben shot wide.
Neuer, who got a hostile reception from Bayern fans although the club has expressed interest in signing him, caught a good effort by substitute Toni Kroos.
Franck Ribery was the next to threaten but Neuer again stood his ground.
Ribery should have equalized in the 87th, but Neuer was again able to stop the Frenchman's shot from 11 meters (yards) out.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom