Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Twanga Pepeta waandaa onyesho kuchangia Gongo la Mboto


na Mwandishi wetu


amka2.gif
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta' kesho inatarajiwa kufanya onyesho maalumu la kuchangia walioathirika na mabomu ya Gongo la Mboto, onyesho lililopangwa kufanyika katika ukumbi wa Zhonghua Garden uliopo maeneo ya Victoria.
Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (Aset), Asha Baraka, inayomiliki bendi hiyo, alisema jana kwamba maandalizi ya onyesho hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, yanaendelea.
Alisema wameamaua kuandaa onyesho hilo kutokana na kuguswa na tu iliyowapata maelfu ya wakazi wa Gongo la Mboto wengi wao kukosa makazi na kupoteza kila kitu hivyo kujikuta katika maisha mapya kabisa ambayo hawakuyategemea.
"Aset kupitia bendi yake ya African Stars ‘Twanga Pepeta' imeamua kuchangia kwa kufanya onyesho maalumu ili kila atakayeingia kwa kulipa kiingilio cha tshs 5,000 ambapo fedha zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto," alisema Asha.
Awali Aset ilichangia walioathirika kwa mabomu kwa kutoa vitu mbalimbali, lakini imeona mchango huo hautoshi hivyo kuandaa onyesho rasmi ili kupata fursa ya kupata michango zaidi kutoka kwa wapenzi na mashabiki wa Twanga Pepeta na wa burudani kwa ujumla.
 
Lowassa kuzindua Bonde la Kukata Maneno


na Irene Mark


amka2.gif
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, na yule wa Viti Maalumu, Martha Mlata wataongoza baadhi ya wabunge katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa injili uliolenga kuchangia ujenzi wa kituo cha kulelea yatima, uzinduzi utakaofanyika Machi 6 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mratibu wa uzinduzi wa albamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Bonde la Kukata Maneno' ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Rudisha Music, Fredrick Fussi alisema gharama za ujenzi huo ni sh milioni 120.
Alisema albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo nane imetengenezwa na mwanamuziki Mchungaji Maximilian Machumu, ambaye ni kiongozi wa bendi ya Mwanamapinduzi, ambapo itakuwa katika muundo wa kaseti, VCD na DVD.
"…Tumepanga kufanya mnada wa albamu hiyo kwenye VCD, DVD na Tape, hapa tunalenga kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha yatima kule Kiluvya," alisema Fussi na kuongeza kuwa dhumuni la kampuni yake ni kuinua uchumi wa wanamuziki wa injili na kuwawezesha kueneza neno la Mungu," alisema.
Alisema wanamuziki wengine watakaopamba uzinduzi huo ni Ambwene Mwasongwe, Martha Mwaipaja, John Lisu, Jakson Benty, Mchungaji Stephen, Wambura na wengine wengi pamoja na wabunge wenye vipaji vya muziki huo kuimba.
 
Mbunifu vazi la taifa ailaumu BASATA


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MSHINDI wa shindano la ubunifu wa vazi la taifa, Agnes Gabriel, amelishutumu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushindwa kulitangaza rasmi vazi alilobuni ili liweze kujulikana na kuvaliwa na Watanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima, kwa njia ya simu kutoka mjini, Bukoba, mkoani Kagera, Agnes alisema tangu aibuke kidedea katika shindano hilo mwaka 2004, BASATA imekuwa kimya na kushindwa kulitangaza vazi hilo kama walivyoahidiwa.
Alisema katika shindano hilo aliibuka mshindi katika kubuni vazi la mwanamke huku mbunifu mwingine Rose Valentine kutoka jijini Dar es Salaam akifanikiwa kubuni vazi la kiume.
Agnes alisema baada ya shindano hilo mavazi ya yalichukuliwa na Baraza hilo kwa lengo la kwenda kuyatunza na kupanga namna ya kuyapromoti ili yaweze kutambulika nchi nzima lakini ameshangazwa na ukimya wa muda mrefu na hata alipowauliza watendaji wa BASATA hakupata majibu ya kuridhisha.
"Hawa jamaa ni wababaishaji tangu 2004 vazi la taifa halijulikani kwa Watanzania, ili hali washindi tulishapatikana, nadhani walikuwa na watu wao wanataka washinde ndiyo maana wanatukwamisha sisi wengine kutokana na unyonge wetu, huku ni kuua vipaji vyetu," alisema Agnes.
Alisema kushindwa kulitangaza vazi hilo kumesababisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana, Emmanuel Nchimbi, kutangaza bungeni hivi karibuni BASATA iendeshe mchakato huo haraka wakati tayari zoezi hili lilishafanyika.
"Sasa hata waziri hana taarifa ya kufanyika kwa shindano hilo kutokana na baraza hilo kutokuwa na mawasiliano mazuri na wizara wakati shindano lililopita ambalo lilikuwa la kitaifa lilihudhuriwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye," alisema Agnes.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom