Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Simba yaibipu Yanga, yainywa Mtibwa 4-1 Send to a friend Sunday, 27 February 2011 21:23

patrick%20phiri.jpg
Kocha wa timu ya Simba,Patrick Phiri

Clara Alphonce
MABAO matatu (hat-trick) ya Mbwana Samatta, yakiwamo mawili ya kipindi cha pili na jingine la Amri Kiemba yameipa Simba ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na kuirejesha kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 37.

Katika mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Samatta ambaye alifungua milango kwa kupachika bao la dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza baada ya krosi ya Kiemba alirejea tena nyavuni dakika ya 65 na 89 kwa mabao mawili zaidi yaliyokamilisha siku nzuri kwake.

Kiemba, ambaye alianzishwa katika mchezo huo aliiandikia timu yake bao la pili, dakika ya 46 ya mchezo huo uliokuwa wenye ushndani kutokana na kona ya Rashid Gumbo.

Nao Mtibwa waliandika bao la dakika ya 55 kupitia kwake Hussein Javu baada ya pasi ya Machaku ambaye aling'ara katika mchezo huo.

Mapema, katika mchezo huo Mtibwa ambao walimkosa kipa wao namba moja, Shaaban Kado anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mechi ya karibuni walipata pigo baada ya kipa wao, Omary Ally kuumia dakika ya nane ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Soud Slim.

Kipa huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa mbaya.

Kwa sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, sehemu ya kiungo ya Simba ilipwaya na kuwapa nafasi Mtibwa kuchezea mpira, ingawa safu ya ushambuliaji ya Wekundu wa Msimbazi iliwapa wakati mgumu mabeki wa wakata miwa hao wa Manungu.

Kama katika kipindi cha kwanza, Machaku Salum alikosa nafasi nzuri ya kuipa bao timu yake dakika ya 53 ya mchezo kwa kushindwa kumalizia pasi ya Issa Rashid.

Samatta angeweza kupata mabao matatu (hat-trick) yake mapema, lakini alikosa nafasi nzuri ya kufanya hivyo dakika ya 75 ya mchezo kwa kushindwa kutumia pasi nzuri ya Mussa Hassan Mgosi aliyekuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Nico Nyagawa.

Mtibwa nao walikosa nafasi ya kupunguza idadi ya mabao baada ya mkongwe Yona Ndabila kushindwa kutumia pasi ya Issa Rashid, dakika ya 84 ya mchezo huo.

Kocha Tom Olaba wa Mtibwa alisema nafasi ya kipa ndiyo iliyomwangusha katika mchezo huo kiasi cha kuwapa urahisi washambuliaji wa Simba kupachika mabao kirahisi.

Naye Patrick Phiri wa Simba alimsifu Samatta kwa uchezaji mzuri licha ya umri wake mdogo na kueleza kuwa ushindi huo ni faraja kubwa kwao kabla ya mechi dhidi ya Yanga mwisho wa wiki.
 
Mr II awachomea wasanii wanaoipigia debe CCM
• Ataka wananchi kutohudhuria matamasha yao

na Janet Josiah, Musoma


amka2.gif
MBUNGE wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr.II (CHADEMA) amewataka Watanzania kuwahukumu wasanii wa miziki hapa nchini ambao wamekuwa wakikipigia debe Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kutoingia kwenye matamasha yao.
Mbunge huyo amesema, wapo wasanii ambao wamekuwa wakiishabikia CCM kuwabeza wananchi na kwamba wasanii wa namna hiyo ambao wanafahamika wanapaswa kuhukumiwa kwa wananchi kutoingia katika maonyesho wanayoyafanya kwenye maeneo yao.
Mbilinyi aliyasema hayo juzi mjini Musoma mkoani Mara, wakati alipozungumza na halaiki ya watu waliojitokeza kwenye maandamano makubwa ya CHADEMA, yaliyofanyika katika viwanja vya Mkendo mjini hapa.
"Ndugu zangu wapo wasanii wanawasaliti wananchi kwa kukodiwa na CCM wakati wa kampeni...wasanii hawa msiwe mnaenda na kulipa kwenye matamasha ama maonesho yao.
"Kama wanakula meza moja na CCM ina maana hawawapendi Watanzania, hukumu yao ni ya kutokwenda wala kununua miziki yao, si mnawajua lakini?" alihoji Sugu ambaye aliwahi kutikisa anga la muziki miaka ya nyuma.
Aidha, mbunge huyo alisema wasanii wanaoshirikiana na CCM hawawatakii mema wananchi na kwamba watu hao ni sawa na wasaliti wakubwa, hivyo wanatakiwa wahukumiwe kwa staili ya kususiwa kazi zao.
Katika mkutano huo ambao ulifurika maelfu ya watu, Sugu ambaye aliitwa na wananchi kupanda jukwaani kuwapa mistari (kuwaimbia muziki), alihitimisha mkutano huo mkubwa kwa kuimba nyimbo zake kadhaa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom