Timu tatu zapeta ligi Arusha
Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 28th February 2011 @ 08:38 Imesomwa na watu: 12; Jumla ya maoni: 0
TIMU tatu za Kundi B zimejihakikishia kuingia hatua ya sita bora ili kupata timu bingwa wa Mkoa wa Arusha.
Timu zilizoingia hatua hiyo ni Flamingo, Golden Kids na Mbuni.
Kaimu Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Gerald Munis alisema timu hizo zote zimebakiwa na mchezo mmoja mmoja.
Munis alisema katika kundi hilo Flamingo ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo na timu za Mbuni na Golden zote zimepoteza mchezo mmoja mmoja.
Akizungumzia Kundi A, Munis alisema timu ya Polisi imecheza michezo yote mitano na kubakiwa na mmoja na imeshinda yote na ndio iliyojihakikishia kuingia hatua ya sita bora.
Kaimu Katibu huyo alisema timu za TMA, Mana Baptis na Duluti zote zinawania nafasi mbili na kila timu ina nafasi ikiwa itashinda mchezo wake wa mwisho.
Alisema ligi ya sita bora itaanza mapema mwezi huu ikiwa ni njia mojawapo ya kutaka ligi hiyo imalizike mapema na bingwa aweze kujiandaa vema katika Ligi ya Kanda.