Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,509
- 911,249
- Thread starter
- #8,321
Airtel Flava yazinduliwa Dar
na Shehe Semtawa
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Airtel jana ilizindua huduma ya ‘Airtel Flava', ambayo ni ya kwanza kutolewa hapa nchini na ya kipekee katika burudani kwa njia ya simu.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Kelvin Twissa, alisema wakati wa hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam jana kuwa, huduma hiyo ya ziada katika simu ni ya kisasa zaidi, ambayo inamwezesha mteja wa Airtel kupata miziki mbalimbali katika simu yake na kuweza kumiliki, kuitumia na hata kuwatumia wengine vile apendavyo.
"Kwa kuwa na ‘Airtel Flava' wateja sasa wanaweza kujichagulia miziki waipendayo na kusikiliza kupitia simu zao za Airtel, wakati wowote kwa kupiga namba 15565 na kuchagua muziki husika," alisema Twissa.
Pia aliongeza kwamba, ikiwa imeambatana na aina kadha wa kadha, Airtel Flava inatoa fursa kwa msikilizaji kuchagua muziki wa kusikiliza, kulingana na hisia zake.
"Bila ya kujali aina ya muziki unaopenda kuchangamka nao, iwe wa kisasa au wa kizamani, kwa hakika kila mtu atapata kile akipendacho, Bongo Flava, Hip Hop, Rhumba, Taarab, Injili pamoja na zilipendwa," alisema Twissa.
Naye Meneja wa Huduma za Ziada wa kampuni hiyo, Frank Semaganga, alisema, ujio wa Airtel Flava, wateja wataweza kuchagua miziki na kuituma kwenye namba nyingine za ndugu, jamaa na marafiki, hata kuweza kuchagua muda na siku ya muziki aliochagua kumfikia mhusika.
Alisema, huduma hiyo inatolewa bure katika mwezi wa kwanza kwa kujiunga na kuwa, huduma ya Airtel Flava inatarajia kuleta mirindimo motomoto, hasa kwa wote wenye kupenda kupata burudani wakati wakiendelea kujishughulisha na kazi nyingine au wakiwa mapumzikoni.

PRINT