Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,501
- 911,251
- Thread starter
- #8,301
Angola, Tunisia fainali CHAN Send to a friend Wednesday, 23 February 2011 19:59
KHARTOUM, Sudan
TIMU ya Angola imewachapa wenyeji Sudan kwa penati 4-2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika za kawaida na kupata tiketi ya kucheza fainali ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya bara la Afrika.
Pia timu ya Tunisia na yenyewe imepata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Algeria kwa penati 5-3 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika za kawaida.
Kwa matokeo hayo Angola na Tunisia zitacheza mechi ya fainali Februari 25, huku wenyeji Sudan waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa kombe hilo wakicheza mechi ya kuwania mshindi wa tatu dhidi ya Algeria kabla mechi ya fainali haijachezwa.
Katika mechi kati ya Angola dhidi ya wenyeji Sudan, mashabiki wa soka wa Sudan wapatao 42,000 walijitokeza kushuhudia mechi hiyo ya nusu fainali na kuujaza uwanja wa Al-Merreikh uliopo huko Omdurman, lakini ndoto za mashabiki hao kushuhudia timu yao ikiingia fainali ziliyeyuka baada ya Mohamed Tahir na Mudathir Eltaib kukosa penati.
Angola wenyewe walifunga penati nne huku Masunguna 'Dani' Afonso akifunga penati ya mwisho ambayo iliipeleka Angola fainali.
Katika mechi hiyo, Sudan walikitawala kipindi cha kwanza, ambapo mshambuliaji wa Sudan, Saifeldin Ali Idris aliipatia timu yake bao la kwanza, mbele ya raisi wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Sepp Blatter, raisi wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya, Michel Platini na raisi wa Shirikisho la Soka Asia AFC,Mohamed Bin Hammam.
Viongozi hao wa mashinrikisho hayio makubwa wapo Afrika kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF.
Hata hivyo katika dakika ya 71, Angola walisawazisha bao hilo ambalo lilifungwa na Arsenio 'Love' Cabungula aliyeunganisha faulo iliyopigwa na Osorio Carvalho.
Baada ya kusawazishwa bao hilo baadhi ya mashabiki wa Sudan walianza kurusha mawe uwanjani, pia mashabiki hao walifanya hivyo katika dakika majeri baada ya kipa wa Angola, Luis 'Lama' Joao kupoteza muda.
Baada ya kusawazishwa bao hilo pia hasira zilionyeshwa hadi kwa wachezaji uwanjani, ambapo kipa wa Sudan, Baha Eldin alichezea faulo ya wazi mchezaji hatari wa Angola, Regio 'Mingo Bille' Zalata.
Pia beki wa Sudan, Haitham Mostafa katika dakika ya 23 ya dakika za nyongeza alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Angola, ambapo refa kutoka Angola alimuona na kumpa kadi nyekundu.
Katika mechi ya Tunisia dhidi ya Algeria, timu ya Tunisia ilifunga penati zote tano katika mechi nyingine ya nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Khartoum, huku Khaled Korbi akifunga penati ya mwisho baada ya Hocine Metref kukosa penati kwa upande wa Algeria.
Katika mechi hiyo, Tunisia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya Slama Gasdaoui kuipatia bao timu hiyo katika dakika ya 18, ambapo alipiga mpira uliokwenda upande wa kushoto wa kipa Mohamed Zemmamouche.
Katika kipindi cha pili Algeria ilifanya mabadilipo ilimuingiza Hadj Aissa aliyesaidia kuongeza mashambulizi katika safu ya ushambuliaji na hivyo Abdelmoumene Djabou alipiga shuti la mbali na kuipatia timu yake bao la kusawazisha.
Timu hizo zilikwenda katika muda wa ziada baada ya muda wa wakawaida kumalizika huku wachezaji wakiona wamechoka baadaya kutumia knguvu nyingi katika dakika 90 za kawaida.
Mashindano hayo ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi kuu za ndani ya bara la Afrika yalianza Februari nne na yanatarajiwa kumalizika Februari 25 kwenye Uwanja wa Merreikh nchini Sudan.