Michezo kama eneo la utengenezaji ajira

XhosaVica

Senior Member
Sep 29, 2020
132
133
Kila siku tumekua tunasikia malalamiko kuhusu ajira.

Ni wakati sasa ukatiliwa mkazo wa kutafuta vipaji vya watoto na kuviendeleza.

Kwa kuanzia ziteuliwe baadhi ya shule na mitaala ya michezo ielekezwe huko ili kutengeneza wanamichezo na walimu wa michezo.

Hawa watakua wamepata ajira lakini wataitangaza nchi pamoja na vivutio vyake.

Si vyema kutokua na wawakilishi washindi katika mashindano ya kimataifa.

Nchi nyingi zimefanikiwa kwa kuwekeza katika michezo kwani michezo pia hujenga nidham na afya.

Michezo itaenda sambamba uundwaji wa viwanda vya vifaa vya michezo nchini kuanzia jezi na hivyo matumizi ya pamba tunayolima.

Uundwaji wa mipira kutumia ngozi za wanyama na mpira unaolimwa Tanga.

Mahoteli yatajengwa, viwanja na kambi mbalimbali na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi wa mtu mmojamoja na taifa.

Ni wakati mhafaka wa kuangalia upande wa michezo na vipaji vya watoto.
 
Back
Top Bottom