Michezo:Je Kesi ya Benard Morrison na Yanga Fc ndio ushindi tuliohaidiwa/ubingwa

kipenseli2021

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
832
783
UTANGULIZI
Hakika katika msimu huu ukiondoa matokeo mbalimbali na mafaniko waliyo yapata Klubu ya Simba na mwenendo mzima wa ligi kuu bara basi moja ya jambo ambalo limeshika sana katika vichwa vya wapenda soka mashabiki wa Simba na Yanga basi bila shaka ni sakata la kesi ya Benard Morrison na Klabu ya Yanga (Mabingwa wa Kihistoria).
Benald Morrison aka Mzee wa kukera ni winga matata sana aliye sajiliwa na Yanga (Mabingwa wa kihistoria) kabla ya kwenda kwa wapinzani waho Simba sc ,kitendo cha mchezaji huyu kuamia kwa Mahasimu waho Simba sc kimeleta maneno mengi hadi Klub ya Yanga wakapeleka kesi TFF (Chama cha Soka Tanzania) lakini maamuzi yalipotoka basi Benard Morrison akaibuka mshindi wa kesi hiyo na wajuzi wa mambo wakampa jina Wakamuhita AKIMU MSOMI aka MZEE WA KUWAKERAAAAAH.
Baada ya muda kufika Klabu ya Yanga haikurizika na hukumu hiyo na kupitia Makamu Mwenyekiti waho Mwakalebela akatangaza kuwa kesi wameipeleka kwenye Mahakama ya usuluhisho ya Michezo (CAS), mambo yakaanza upya lakini kukiwa na ukimya sana na giza neno kuhusiana na kesi hiyo ambayo wajuzi wa mambo wanasema kila Benard Morrison akishinda basi keshi hiyo inafufuliwa upya.

Hadi leo hii naandika makala hii bado viongozi wa Yanga kupitia msemaji waho na Makamu Mwenyekiti bado wanasema kuwa ifikapo tarehe 23/7/2021 basi hukumu ya kesi hiyo iakuwa imekamilika.

waandishi mbalimbali waliandika nanukuu toka kwa blogspot ya salehe jembe
"
Kesi yake kuhusu utata wa usajili na Klabu ya Yanga katika Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo, (Cas) inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa Cas wamethibitisha kupokea barua ya rufaa ya kesi hiyo tangu Mei 25 mwaka huu.

"Pande zote mbili kwa maana ya klabu ba mchezaji tumetakiwa kupeleka maelezo Cas na hadi kufikia Juni 2 mwaka huu tayari kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

"Kama klabu sisi Yanga tutapeleka maelezo ila hatujajua kuhusu huyo mchezaji kikubwa tunataka kuona haki inatendeka," .



Kwa sasa Morrison ambaye alisaini dili la miaka miwili Simba akitokea Yanga yupo zake Mwanza ambapo timu yake kesho ina mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting. "

LAKINI NAJIUULIZA YAFUATAYO


  • JE WEWE SHABIKI WA YANGA HUKUMU YA KESI HII INAWEZA KUWA NDIO AHADI YA UBINGWA KWA MWAKA 2020/2021
  • JE KESI HII INAWEZA KUWA KIPIMO CHA UAMINIFU NA UTENDAJI KAZI WA VIONGOZI WA YANGA
MAPENDEKEZO
Viongozi wa Yanga hili kuweza kulinda heshima mbele ya mashabiki waho basi watoke na kusema ukweli juu ya kesi hii maana isipofanyika itawaletea sifa mbaya sana

kwangu mimi kesi hii ikifanyika basi ni ushindi tosha kwa Klabu Yangu ya Yanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom