Michango ya ujenzi wa kanisa kukusanywa baa ni sawa?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,272
Nilikuwa nimekaa katika bar moja Mbezi milango kama ya saa 4 kuelekea 5 usiku. Wakaja watu wanawake kwa wanaume wakawa wanazunguka kila meza na fomu za kuchangisha michango ya ujenzi wa kanisa la dhehebu fulani sitalitaja hapa lakini sio RC. Baadhi ya wanywaji walichangia huku wakisema kumbe Mungu anatutambua na kutufuata mpaka huku. Kwangu mimi hii ilikuwa ni mpya kwani huko makanisani wanaoshambuliwa sana kwa mahubiri na kuonekana ni wadhambi wakuu ni wazinzi na wanywaji wa pombe kwa maana ya walevi. Hili lilinifanya niwaze kuwa kama wamefikia hatua hii wanaweza kwenda hata kwenye nyumba za wageni na kuanza kugonga kila chumba kuomba michango. Mimi kwa maoni yangu nafikiri kukusanya michango ya ujenzi wa kanisa ni sawa lakini kwenda mpaka baa tena usiku naona kama kuna mushkeli.
 
Sawa kabisa. Ni lazima tugawane na shetani au tumnyang'anye kila kitu.
 
Si afadhali hao wako kidogo linient na pombe halafu ni watu wazima kuna imani fulani ilikuwa inawatuma vijana wadogo kukusanya hiyo pesa
 
Dah..hizi nyumba za ibada zimetosha kwa sasa....tuangalie nyumba vya madarasa sasa
 
Mtu mmoja kaniambia labda wamegundua waumini wengi wanatumia pesa nyingi baa kuliko kutoa sadaka na michango mbali mbali wanapokuwa kanisani hivyo ni bora kuwafuata huko huko waliko. Lakini hii ni staili mpya. Bora wangekuwa wanawapa wanywaji wenyewe hizo kadi ili wachangishane wenyewe huko huko
 
Si afadhali hao wako kidogo linient na pombe halafu ni watu wazima kuna imani fulani ilikuwa inawatuma vijana wadogo kukusanya hiyo pesa
Kwani kuwatuma vijana wadogo ni kosa? Hata hivyo uko nje ya mada mkuu
 
Ni kosa kubwa sana
Mzazi anajua mtoto yuko anapata elimu ya dini, mwalimu anamtuma mtoto akachangishe pesa kwenye mabar? Unafahamu risk zake? Niambie ni sheria gani imeruhusu hili..
Zaidi sipo nje ya mada bali ndio nimezidi kupanua mjadala wa watu kuomba michango ya nyumba za ibada sehemu za vilevi
 
Nilikuwa nimekaa katika bar moja Mbezi milango kama ya saa 4 kuelekea 5 usiku. Wakaja watu wanawake kwa wanaume wakawa wanazunguka kila meza na fomu za kuchangisha michango ya ujenzi wa kanisa la dhehebu fulani sitalitaja hapa lakini sio RC. Baadhi ya wanywaji walichangia huku wakisema kumbe Mungu anatutambua na kutufuata mpaka huku. Kwangu mimi hii ilikuwa ni mpya kwani huko makanisani wanaoshambuliwa sana kwa mahubiri na kuonekana ni wadhambi wakuu ni wazinzi na wanywaji wa pombe kwa maana ya walevi. Hili lilinifanya niwaze kuwa kama wamefikia hatua hii wanaweza kwenda hata kwenye nyumba za wageni na kuanza kugonga kila chumba kuomba michango. Mimi kwa maoni yangu nafikiri kukusanya michango ya ujenzi wa kanisa ni sawa lakini kwenda mpaka baa tena usiku naona kama kuna mushkeli.

Sasa kama kondoo hampatikani mazizini wafanyaje
 
Naona ni ujinga tu kushangaa kukusanya mochango bar, WAKATI HUSHANGAI WATOA MICHANGO KUWA BAR, NA WALA HUULIZI WWCHANGAJI WANATOA WAPI HIZO HELA WANAZOCHANGA
 
Nilikuwa nimekaa katika bar moja Mbezi milango kama ya saa 4 kuelekea 5 usiku. Wakaja watu wanawake kwa wanaume wakawa wanazunguka kila meza na fomu za kuchangisha michango ya ujenzi wa kanisa la dhehebu fulani sitalitaja hapa lakini sio RC. Baadhi ya wanywaji walichangia huku wakisema kumbe Mungu anatutambua na kutufuata mpaka huku. Kwangu mimi hii ilikuwa ni mpya kwani huko makanisani wanaoshambuliwa sana kwa mahubiri na kuonekana ni wadhambi wakuu ni wazinzi na wanywaji wa pombe kwa maana ya walevi. Hili lilinifanya niwaze kuwa kama wamefikia hatua hii wanaweza kwenda hata kwenye nyumba za wageni na kuanza kugonga kila chumba kuomba michango. Mimi kwa maoni yangu nafikiri kukusanya michango ya ujenzi wa kanisa ni sawa lakini kwenda mpaka baa tena usiku naona kama kuna mushkeli.
Labda nikujibu kwa mfumo wa swali (maana hata Yesu awakati mwingine alipoulizwa swali, alianza kuwajibu kwa kuwauliza swali wanafiki. Mfano, aliulizwa, "Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?" Yeye pia akawauliza kuhusu sarafu waitumiayo kulipa kodi, ..."Sura na chapa hii ni ya nani?").
Sasa nakuuliza:
Hivi ni haki mbele ya Mungu kulibadilishia matumizi jengo fulani kutoka kuwa kilabu cha pombe na kuwa jengo la kumuabudu Mungu, yaani kanisa?
 
Back
Top Bottom