Ile thread iliyozungumzia michango ya harusi sijui (ya bwana harusi kuomba apewe kodi ya miezi sita) sijui imepotelea wapi!! Hat hivyo, thread hii imenikumbusha jambo linalofanana na hilo!! Nilipomaliza chuo, nilikaa mtaani karibu miezi tisa bila hata angalau ya tempo!! By the way, my first option ilikuwa ni kujiajiri mwenyewe, but i'd no capital! Wazazi nikawaomba angalau milioni moja (it was 2003) nianze na kabiashara, wakanitolea nje! Miezi 5 baada ya kumaliza chuo, kukawa na graduation ambapo family wakapanga budget ya sh. 1.5 m kwa ajili ya sherehe!!!! But still, muda huo nilikuwa mtaani!! Nikawaambia ni kwanini basi hizo pesa wasinipe mimi nianzishe biashara, hata kama ni ya kufuata mchele mkoa!! Wakanichomolea!! Hata nilipowaambia kwamba sioni maana ya mimi kuserebuka usiku halafu asubuhi naamkia mkunguni( hapa ndo kilikuwa kijiwe chetu majanki!) bado sikueleweka!!! Nami kuonesha kwamba hicho kitu hakikuwa muhimu sana kwangu as compared to my propasal, nikasusia sherehe za graduation!!! Mama yangu alinikasirikia karibu miezi miwili, lakini sikujali!!! Ni kweli, ingawaje nina elimu ya chuo kikuu lakini sijawahi kuvaa joho!! Hata hivyo, hadi leo sijajutia uamuzi wangu!!!!