Michango ya Rambirambi za Misiba kwenye makundi ya Whassap imegeuka mzigo kwa wachangiaji

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,695
51,820
Ukiwa member wa makundi ya Whassap, ya kifamilia, ukoo, mliosoma wote primary, O-Level, High School, Chuo, Kazini, Mtaani Kuna mzigo mzito sana wa michango ya rambirambi inakungoja.

Kila kundi unakuta lina wastani wa watu 20 mpaka 50 na mengine yanafika watu 100. Katika makundi haya, ndani ya miezi miwili unakuta angalau kuna msiba katika kundi mojawapo. Wakati mwingine unakuta zaidi ya makundi 3 kuna msiba na unahitajika mchango!.

Michango ya misiba imekuwa ni kitanzi kizito sana kwa members ila wanaugulia kimyakimya ili wasionekane wabaya.

Na Michango ya Rambirambi kimsingi imetengenezwa in such a way siyo ya hiyari kivile japo hakuna kulazimishwa kwa nguvu bali kuna kulazimishwa kisaikolojia na pia jinsi hiyo michango ilivyo haiko kwa namna ya kuonyesha upendo au kuguswa na msiba, bali imegeuka kuwa kama VIKOBA kuwa Ukichanga basi na wewe utachangiwa!. Usipochanga basi hakuna hata kuitisha rambirambi kwenye kundi ili kila mtu atoe kwa hiyari yake bila kujali policy ya kundi!.

Katika maisha haya ambayo uchumi unazidi kuwa mgumu, Hii michango ya rambirambi katika makundi ya Whassap imegeuka shubiri kwelikweli.
 
Vipi kuhusu michango ya harusi na sherehe zingine za anasa na ufahari ipo kwenye makundi hayo? Afadhali huko kwenye whatsaap, hapa mtaani balozi kachosha kukusanya hela za rambirambi kila mara. Hata kama haupo umesafiri ukirudi tu atakuambia kuna misiba mitano ilitokea mtaani unatakiwa utoe rambirambi kila msiba ni elfu moja na kuendelea ukimpa tu hapeleki kulikotokea msiba anachikichia mwenyewe. Mbaya zaidi kumbe mchango ni mia tano yeye huongeza kwa hila tu anakula cha juu. Wakati mwingine huongeza idadi ya misiba ambayo haikutokea anajua hutahoji ni wapi ulipo msiba na hutafuatilia kwa kuwa mjini kuna watu wengi na huwajui wote zaidi ya majirani tu. Cha ajabu ni kama unalazimika uchangie msiba usiokugusa na humjui kabisa marehemu wala wafiwa
 
Michango ya Harusi nayo ni balaa tena ni Pledge siku hizi ni malaki ya pesa. Lakini tofauti ya Harusi na Rambirambi ni kuwa wanaooa ni wachache kuliko wanaokufa na ni personal sana
 
Unapata faida gani kua member kwenye hayo magroup?
Kwani hua mnalazimishwa kujiunga kwenye hayo magroup?

Mkuu,ishi maisha yako,usiishi kwa kuogopa watu kua eti watanionajee,
Fanya ambacho kitakupa peace kwenye nafsi yako badala ya kujitesa,
Life is too short,enjoy it.
 
Michango ya birthday parties iongezwe pia hadi bongolala waamke.

Michango hii pamoja na ile ya harusi za wenye kuozeshwa na marafiki, majirani, co-workers n.k kwa jina la ufadhili wa harusi inaumiza na kuharibu bajeti za wachangiaji.
 
Naunga Mkono Hoja
Hili Nalo Baadaye Watu Hujitoa Kutokana Na Ukata
Mbaya Zaidi Viongozi Wa Hayo Makundi Sasa Oops
Kisaikolojia Ni Kulazimishana.

***Hayana Maana Wala Msaada Wowote Ila Viongozi Huwajengea Hofu Members
Maiti Haitupwi, Pia Manispaa Inazika Tu
 
Nadhani kila mtu afanye anachoona kinamfaa,as long as hakuna anayelazimishwa kutoa/changa wewe ukiona acha lipite wenye kuguswa watoe wewe baki kufanya yale unaona yanakufaa ndani ya kundi.

Kuna jamaa yangu nilisoma nae primary alimuuguza baba yake almost 9 years alipofariki kwenye group la shule yetu ilichangwa karibia 1.5mill kusaidia msiba na jamaa anasema ilimtosha kumzika baba yake so haya mambo ya misiba kama halijakukuta huwezi kuona umuhimu wa kumchangia mwenzako Tsh 5,000/=
 
Kuna group lilianzishwa miaka ya 2017 la members wa hapa JF lilikuwa na members 75 kama sijasahau, ila kila siku huku kwenye group kila member kafiwa anahitaji mchango, sasa nani atamchangia mwingine? Baadae tukaamua kuweka utaratibu wa kuchanga 10k kila mwezi kuwe na shida kusiwe na shida. Baada ya miezi kama mitano admin akadelete group lile la whatsapp na hela zetu kamega. Ukija huku jukwaani JF anajifanya great thinker sana. Baada ya kuopoa kimwana humu kapotea jukwaani na iD kaitelekeza, kumbe alienda unganishwa kwenye gridi ya taifa bila kujijua. Saivi anashinda huko X ana kazi ya kuretweet maneno ya biblia. Hela za rambi rambi sio za kuzila. 😏
 
Ebhanaeee duh
 
Ni michango kwa ajili ya kumfariji Mfiwa, kinacholeta shida ni kutokana na hali ngumu ya uchumi.
Bro,suala la msiba siyo la kuzungumza kwamba shida ni uchumi umekuwa mgumu.

Jiulize yule aliyefiwa anajisikiaje maana kibongo bongo unakuta wote wewe na yeye ni unga unga mwana siku ziende na umekuja msiba juu unadhani kumpa 5K yako kama rambirambi kutazidi kukufanya maskini?kama tumefikia hadi kuhoji ishu za rambirambi na kabisa tupo hapa tunajadili basi mentality tutakuwa tuna shida kubwa mahali.
 
Back
Top Bottom