CONSTRUCTIVE THOUGHT
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,158
- 417
Amani iwe nanyi!
Wapendwa Watanzania wenzangu naimani sote tunakumbuka kuwa Mh. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward lowassa, aligombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananch (UKAWA).
Katika jitihada za kuongeza nguvu kifedha ili Mh. Lowassa ashinde Uchaguzi, Watanzania wote tuliokuwa tayari kumuunga mkono Mgombea, tuliombwa kumchangia Mh. kwa kutuma pesa kupitia mitandao ya simu mfano TIGEO. Mimi nilikuwa ni mmoja kati ya watu tuliotoa huo mchango japo hatukufanikiwa mgombea wetu kushinda.
Baada ya Uchaguzi, nilitarajia kupata ufafanuzi wa mapato na matumizi ya pesa hizo za mchango lakini cha ajabu hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa na CHADEMA au Lowassa mwenyewe ikiwa ni sehemu ya kuwajulisha na kuwashukuru wote waliotoa mchago huo.
Nauliza kwa nia njema, ivi hiyo michango ilienda wapi? Kama ilitumika katika Uchaguzi, iliobaki ipo wapi?