Michango style ya Mzee Kingo ni hatari

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Ukiona watu wanachangishana msibani au harusini ili kuwezesha mazishi au ndoa jua hali sio nzuri kwenye familia. Mzee Kingo aliwahi kuchangisha msibani watu wakajua za sanda. Walishangaa karudi yuko mbwii! Kumuuliza akawajibu "Wakati nawachangisha niliwaambia matumizi"?

Hivi CHADEMA hamkujua kutakuwa na kampeni mkafanya resource mobilization kama mlivyofanya 2015? Yaani mnachangishana siku ya uzinduzi? Au ni kweli kuwa wafadhili wenu wamesusa kutokana na ninyi kuwa na matumizi ya hovyo na kutokuwa na dalili za kushinda? Kama mlipanga ndugu kuchangishana ndio mfanye huku mkitegemea TBC? Au ndio maana mlikasirika walipositisha matangazo? Hivi mlitaka BBC ishiriki lile zoezi? Hamjui kuna ethics za vyombo vya habari?

Kama kweli mna wanachama nchi nzima kwa nini hamkuchangishana kimyakimya kabla ya uzinduzi? Hamjui namba zao? Mliwaandikishaje?

Mmejiumbua sana jana! Hamna hela ya kampeni. Na hivi hii njia mbona ndiyo mliyodai kuitumia wakati wa kutafuta hela ya faini? Kwani kipindi cha faini mlitumia TBC? Au ilikuwa uongo hawakuchangia? Maana ingekuwa ukweli si mngeshaitumia bila kujiumbua kama jana? Haya TBC mmewafukuza sasa mtawatangaziaje hao wanachama hizo namba? Star TV? ITV? Channel 10?

Na mnaochangishwa mmeambiwa matumizi? Yasije yakawa ya Mzee Kingo? Aisee Bora Hashimu tunamuelewa.

1599033066159.png
1599033076807.png
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom