ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Michael Wage, alikuwa mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Serikali imemsimamisha kazi yeye na Watumishi wengine kwa tuhuma za ubadhilifu wa Tshs. 900milioni na mamlaka husika zinaendelea na uchunguzi ili kupata ushahidi wa kina wa kuwezesha Serikali kumfikisha Wage na watuhumiwa wengine Kizimbani.
Wage ambaye sina shaka analikuwa ana mfahamu Bw. Jerry Muro muda mrefu, anakwenda kutokana na taarifa za kipolisi, anaamua kukimbilia Polisi kumripoti Jerry Muro kuwa anamwomba rushwa ya Tshs. 10 Millioni kwa nguvu na kujifanya yeye ni mtumshi wa TAKUKURU!, Polisi wanamwandalia Wage mazingira ya kutendea uhalifu (Scene of Crime) kama ilivyo kwenye michezo ya kuigiza, wanamweleza wataweka mtego kumnasa Jerry na Wage anapaswa "kupozi" kama msanii wa Hollywood ili picha isijeikakosa mauzo.
Wage kweli ni mwadilifu kwa Serikali yake, anafanikisha kazi aliyotumwa na Serikali pasipo hata posho!. Jerry na wenzake watatu wanakamatwa katika siku na mazingira tofauti na baadae kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumwomba Wage rushwa kwa nguvu……
Hakika Wage ni mtumishi muadilifu, ameweza kujikosha wa jamii kuwa yeye ni safi kabisa, pamoja na kudaiwa kuchota mijihela yote hiyo Serikalini, lakini hakuwa tayari kutoa hata senti moja ya rushwa na akijua kuwa tukio zima la kuombwa rushwa likarekodiwa kwa kamera za CCTV za polisi, Wage hakusita kuonyesha umahiri wake kwenye sanaa za maigizo Serikalini kwa kuwa mgumu kutoa rushwa ili polisi (Serikali) ipate kielelezo kamili kuwa nguvu zilitumika katika tukio zima la Wage kuombwa rushwa.
Wage ameonyesha upendo kwa Serikali yake kwa kukubali kusimama kama shahidi wa kwanza upande wa mashtaka pamoja na tuhuma dhidi yake za kuchota na kufuja mamilioni ya Serikai katika Halmashauri ya Bagamoyo, pamoja na kuwa benchi kwa ubadhirifu..... Kwa kweli hapa Wage amecheza sinema ya Katun ya Tommy & Jerry!.
.............Nchi yangu Tanzani, jina lako ni tamu sana, nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama weee,...
................Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisaaa...ah,
.............Tanzania Tanzani, watu wako ni wema sana weeeee...
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=UXDh7OwlOOM"]http://www.youtube.com/watch?v=UXDh7OwlOOM[/ame]