Mianamke mingine bwana!!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,781
Last year niliachana na mwanamke wangu wa zamani.
Baada ya kimya kirefu nikapata kitu kipya ambacho tuna mipango ya kufunga ndoa na kujenga familia imara.
Mwanamke niliyeachana naye mwaka jana, amemuadd kama rafiki huyu mchumba wangu, na amebandika kwenye ukuta wake picha ambayo tulipiga wote kipindi cha mapenzi yetu.
Kibaya zaidi ni kwamba mchumba wangu kaiona hiyo picha mchana huu na kisha nitumia msg ya kiukorofi.
Sijui jioni nkirudi home hali itakuwaje?
 
hahaaaaaaa lol
mwaga mboga nimwage ugali ............visa hivi jamani duh!!!
 
hahahahah pole sana ila huyo mwanamke ni mkorofi sana ama bado anakupenda ?
jiandake kunyoosha mistari Bujibuji
 
Mambo ya Facebook nini hayo?? Maana kule nako kuna visa kibao usipimie. Tayarisha maneno matamu matamu ya kumpooza bi mkubwa
 
Mambo ya Facebook nini hayo?? Maana kule nako kuna visa kibao usipimie. Tayarisha maneno matamu matamu ya kumpooza bi mkubwa

huyo dada atakuwa kajisahau hata baada ya kuachana na Buji Profile foto yake hakubadilisha................(mweh usikute bado ana mafilingi, mimi hilo lingefanyika asap)
 
Du!!! Mkuu inabidi umtafute Juma Necha akusaidie kupanga mistari maana hicho kimbembe!
 
@ Buji kumbe ni mwehu??? msamehe bure..........
 
Ulitokana wapi na mwehu?
Huyu wa sasa ushampima akili akajua siyo juha? Nakutania ..ila ulivyomponda yule wa zamani siyo ustaarabu hata kidogo!
Ukipata chungu kipya usidharau cha zamani...
 
Tupatie xpiriensi za huko bina!

MJ kule kwenye facebook kule wacha kabisa. Kule wananchi wanaeka picha zao za ukweli kabisa. kule visa vya mapenzi kama cha Bujibuji mtu ndo anachukulia chance ya kukuharibia. Kule bwana kule ni kuchorana kishenzi mimi naonyesha niko hivi nimeumbwa hivi sijui nikismile niko hivi yani kule ni balaa.......................kule mtu anakuomba urafiki na picha yake ya ajabu ajabu inaonyesha maungo.................
 
Ulitokana wapi na mwehu?
Huyu wa sasa ushampima akili akajua siyo juha? Nakutania ..ila ulivyomponda yule wa zamani siyo ustaarabu hata kidogo!
Ukipata chungu kipya usidharau cha zamani...

Tausi unamaanisha aweza kukitumia tena hiki cha zamani au?
 
Wehu wake haujathibitishwa na wataalam.
Ila kwa nini awe mkorofi namna hiyo na tulisha achana tangu mwaka jana mwezi wa nane?

labda hamkuachana kiustaarabu au mligombana? au ulimwacha bila sababu? ila usimwite mwehu haipendezi unless ni mwehu kweli. sasa mbona na huyo mchumba kakutumia msg ya kiukorofi au nae mwehu? Pole sana ila kama mchumba wako ni mwelewa atakuelewa tu mpangie maneno mazuri
 
Tausi unamaanisha aweza kukitumia tena hiki cha zamani au?
BHT ..
we acha tu... mi napenda kuhakikisha cha zamani sikitupi jalalani! Nakihifadhi vizuuuri stoo. Kipya kikikorofisha.. basi najua kuna fall back!

Huyu kaona kimwana kipya..hajajua vimbwanga vyake bado!
 
BHT ..
we acha tu... mi napenda kuhakikisha cha zamani sikitupi jalalani! Nakihifadhi vizuuuri stoo. Kipya kikikorofisha.. basi najua kuna fall back!

Huyu kaona kimwana kipya..hajajua vimbwanga vyake bado!

hahaaa TM we kiboko aisee!!! mie nakivunja kabisa na vipande vyake staki kuviona kamwe!!!
 
unalo ilo Buji, mliachana ila bado mwanamke anakupenda au anataka kuharibu tu, kaa na bibie mpya mweleze kinagaubaga kama anakupenda kweli atakuelewa. pole sana
 
hv uncle Bujibuji, kwani hiyo picha ilikuwa na ubaya gani kuwa kwenye profile ya huyo ex wako?? labda yeye pia alisha move on na maisha yake but hakuon atatizo kuendelea kutundika hiyo picha.........kwanini siku zote hizo aliiweka mpaka jana usiku tu ndo aitoe? lini alim-add huyo mchumba wako kwenye list yake ya marafiki?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom