Miaka zaidi ya 10 Baada ya Janga la Kikwete bado Watanzania hatujui tunataka Rais mwenye Sifa zipi!

Sijaona tofauti ya kipindi kile unaniheshimu na sasa unaponidharau.... No difference at all.😁😁😁 Ajira watu wenye sifa watapata na wasio na sifa watapoteza tu. Kila taasisi zilizokuwa zinaishi kijanja janja will collapse too. Binafsi naendelea kusimama neutral na kufurahia maisha.

GuDume sio mtu makini. Mambo yote haya watu wanalalamika kutwa kukicha yeye haoni. Maelfu ya watu wamepoteza ajira kwa sababu ya biashara kufungwa na makampuni kupunguza watu, benki zaidi ya nane zimecollapse (ajira nyingi hapa zimepotea), wawekezaji wamefunga biashara na kukimbiza mitaji nje. Sitaki kuzungumzia mateso na dhuluma nyingine.Pamoja na mapungufu ya utawala wa Kikwete, hatukuumia kiasi hiki. Wewe Gudume nimekudharau sana, halafu unavyojifanya philosophical! Pimbi mkubwa.
 
Kila utawala una falsafa zake ila kumuelewa jiwe inahtaji MAARIFA ya juu sana
 
abdi ally umenishangaza sana kwa maoni yako.sikutegemea bado kuna kundi la watu kadhaa lina akili na uelewa kama wewe. Ninyi watu wa namna hii huwa mnakuwa 5 katika 100. Unachosema sikipingi hata kidogo.

Kila utawala una falsafa zake ila kumuelewa jiwe inahtaji MAARIFA ya juu sana
 
Subiri rais atakayekuja kukuondolea umaskini au kukupatia ajira. Wewe umewapatia ajira wangapi mpaka sasa? Kwa nini kila mtu anataka nchi imfanyie kitu. Nani anawaza yeye kuifanyia kitu?

Kazi ya serikali ni kupambana na ukuaji wa uchumi kwa wananchi wake, je, toka magufuli ameingia ikulu amefanikiwa kwa kiwango gani kupunguza umasikini nchini?

Magufuli amefanikiwa kwa kiwango gani kupunguza tatizo la ajira nchini?
 
Kama msomi nilitegemea kuona ukilinganisha kulingana na mafanikio yao wakiwa viongozi kisiasa, kijamii na kiuchumi ingawa ni mapema mno hasa ukizingatia Magufuli ndio kwanza anamalizia awamu yake ya kwanza. Ninachoona hapa ni kulinganisha maneno na matendo yao ambayo pia ulipaswa kuangalia yana tija gani kwa mwananchi
 
Sijaona tofauti ya kipindi kile unaniheshimu na sasa unaponidharau.... No difference at all.😁😁😁 Ajira watu wenye sifa watapata na wasio na sifa watapoteza tu. Kila taasisi zilizokuwa zinaishi kijanja janja will collapse too. Binafsi naendelea kusimama neutral na kufurahia maisha.
Hivi wewe unajua nini maana ya neutrality? Kama wewe ni neutral na unafurahia maisha kihehere cha nini kuja hapa kusifia ujinga na kumponda mwingine! Siku nyingine jifunze kufanya comparative analysis! Angalia maeneo na variables zote. Hujui hata Political Economy wewe! Halafu kuna tofauti ya neutrality na objectivity. Niishie hapa sitaki kubishana na wewe.
 
Kwa nini usinywe maji kwanza ukatuliza munkari? Nyie watu kwa nini mnakuwa na ghadhabu zisizo na sababu?

Hebu soma taratibu then nioneshe nimemlinganisha kikwete na nani. Maana mimi nmesoma tena na tena. Nikaona nimpe mtoto wangu wa darasa la pili naye asome.😁😁😁 Kanambia kuwa hajaona kama nmelinganisha watu hapa.

So please if you want to use some terms like"comparative analysis " kuonesha unajua jua... Find appropriate environment.😁😁😁 Nuoneshe nimemlinganisha kikwete na nani.

Angalia utawala wa mwalimu,mwinyi,mkapa,na jk alafu utazame utawala wa jpm kisha angalia kwa jicho lisilo jaa chuki wala husda alafu tafakari maneno ya wanasiasa wenye chuki na unafki ndio mtajua mtoa mada alikuwa anawaza nin TATIZO WATZ WENG WANAFKI HAPA ILIPO TZ HAIKUTAKIWA KUWA HAPA ATLEAST TUNAONA MABADILIKO KILA MAHALI JAPO KWA UCHACHE LAKIN TUNAENDA NA MAISHA YANAENDA WENG WAPIGAJI NDIO WANAO LALAMA HAKUNA PESA ILE ONA JIJI BILION3 MWAKA MZIMA HAZIKUTUMIKA KUTENGENEZA MACHNJIO VINGUNGUTI ZIMERUDI SERIKALINI JE NI MANGAPI TUMEPIGWA AWAMU ZILZOPITA? TUWE WA KWELI TUSIWE WANAFKI NA ROHO MBAYA
 
Kinachotokea ni kila awamu ya uongozi kuzalisha changamoto mpya kutokana na style na uthabiti katika uendeshaji wa nchi.

JK kwa kweli hakuwa anaongoza hii nchi. He was ruling and not governing! Nchi hii ilikuwa ikiongozwa na 'genge' fulani la watu. Watu hawa ni hasa wenye maslahi ya kibiashara. Matokeo yake ufisadi, biashara haram, ubabe wa kiserikali, matumizi mabaya ya fedha za umma vikashamiri.. Matokeo yake tukawa na 'fake economy'. Uchumi ambao ulijengwa hasa na mifereji ya fedha kutoka serikalini. Kwa wakati wa JK, malalamiko makubwa ya wananchi ilikua ni Ufisadi, Madawa ya kulevya, Uzembe katika utumishi wa umma.

JPM kaja nae kutekeleza yale ambayo aliona kwake ni mapungufu ya Awamu ya Nne. Kajitahidi kupambana na Rushwa, Madawa ya kulevya, Uzembe katika utumishi wa umma, Matumizi ya hovyo ya serikali. Katika kutimiza haya changamoto mpya imezaliwa, kushuka kwa mzunguko wa fedha na biashara mtaani. Lakini kubwa zaidi style yake ya uendeshaji nchi inakinzana na hitaji la sekta binafsi na mfumo mzima wa mzunguko wa biashara. Pia tusisahau, kutoka katika mfumo wa serikali uliopita kuja mfumo mpya, ni lazima hali ya kiuchumi iyumbe. Malalamiko ya awamu hii kwa wananchi ni hela hakuna mtaani. Kama serikali ya watu ni lazima ichukue hatua za 'kiuchumi' na si za 'kiserikali'..

Bado naamini kwa vigezo vingi JPM ni bora zaidi kuliko JK, ila ili amalize utawala wake na kuacha legacy, afanye haya:

1. Katiba ya wananchi. Katiba itayoweka misingi thabiti ya utawala wa sheria na kujenga taasisi imara za kiserikali na kiuchumi.

2. Masikilizano na sekta binafsi. Zipo hatua ambazo serikali hii inazichukua si za 'kibiashara' kabisa. Katika mazingira ambayo mzunguko wa fedha ni mdogo, serikali inapaswa ilenge kukusanya kidogo wa wengi kuliko kingi kwa wachache. Hata hao wachache watashindwa kuendesha biashara.

3. Miradi mikubwa ya serikali. Serikali inapaswa kuangalia namna bora zaidi ya utekelezaji wa miradi mikubwa. Utumiaji wa fedha za serikali inafanya serikali kutoil, kuongeza deni la taifa, na kuathiri mzunguko wa fedha kwenye biashara mtaani.

4. Kubana matumizi. Kubana matumizi ni jambo jema. Lakini kukipitiliza kuna athiriki sekta binafsi ambao hasa ndio wanaopeleka hela mtaani na kuongeza mzunguko wa fedha na kuchochea biashara ndogo ndogo.

5. Imani ya serikali kwa sekta binafsi. Hili linaweza endana na kubana matumizi. Serikali kuzipa taaisis za serikali miradi mbalimbali inaathiri sana mzunguko wa fedha mtaani. Mathalani unapoipa JKT mradi kama wa Ukuta wa mererani badala ya kampuni fulani unaathiri sekta binafsi. Serikali ifike mahala ifikirie hata kuzikopesha kampuni binafsi katika miradi fulani fulani.

Muhimu serikali ifanye kazi kwa kuaminiana na sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama msomi ulipaswa usome thread uielewe. Hii thread imemzungumzia kikwete. Wewe unaona amelinganishwa na nani? Kwa nini umeanzisha thread ambayo haipo? Mbona ipo wazi kabisa kuwa nmezungumzia utawala wa kikwete. Wewe unataka nimlinganishe na nani? Wakati mimi sijawaza mlinganisha na mtu.

Kama msomi nilitegemea kuona ukilinganisha kulingana na mafanikio yao wakiwa viongozi kisiasa, kijamii na kiuchumi ingawa ni mapema mno hasa ukizingatia Magufuli ndio kwanza anamalizia awamu yake ya kwanza. Ninachoona hapa ni kulinganisha maneno na matendo yao ambayo pia ulipaswa kuangalia yana tija gani kwa mwananchi
 
Kwa nini usinywe maji kwanza ukatuliza munkari? Nyie watu kwa nini mnakuwa na ghadhabu zisizo na sababu?

Hebu soma taratibu then nioneshe nimemlinganisha kikwete na nani. Maana mimi nmesoma tena na tena. Nikaona nimpe mtoto wangu wa darasa la pili naye asome.😁😁😁 Kanambia kuwa hajaona kama nmelinganisha watu hapa.

So please if you want to use some terms like"comparative analysis " kuonesha unajua jua... Find appropriate environment.😁😁😁 Nuoneshe nimemlinganisha kikwete na nani.
Sio kwamba najua jua, najua. Usijifanye unajua rhetoric, hujui. Kuna vitu vinakuwa ni 'implied' hauhitaji kusema unalinganisha ili tujue unalinganisha! Soma tena hayo ma paras uliyoandika.
 
😁😁😁 yu think yu know.then lemme treat yu that way.mimi sijui... Unaifaham socratic irony?just google.

Just in plain sight. Amezungumziwa kikwete.Never compared "him" with Dr. Magufuli. Utakachoamua kuamini amua... Sitokulazimisha.but nakushauri tuliza akili.soma kwa utulivu.kunywa juice,maziwa au maji... You will finally understand.😁😁😁

Sio kwamba najua jua, najua. Usijifanye unajua rhetoric, hujui. Kuna vitu vinakuwa ni 'implied' hauhitaji kusema unalinganisha ili tujue unalinganisha! Soma tena hayo ma paras uliyoandika.
 
Kwa heshima na taadhima nitapingangana na mawazo yako mpaka siku ya kiama. Kwangu mimi hakuna rais aliyeharibu nchi kama Kikwete. Chini ya Kikwete wavivu na mafisadi walitamba na ndiyo waliokuwa wanaamua nchi iendeshwe namna gani! Ofisi za umma wafanyakazi walikuwa na kiburi na hawakuwa na woga wowote. Sehemu nyeti kama bandarini na airport shughuli zilikuwa zinaendeshwa kama watu wako chooni. Ukiangalia ''barabara'' unazosema zilijengwa ni za hovyo kweli kweli. Hazina viwango. Barabara za mijini hazina sehemu ya waenda kwa miguu, ni nyembamba na pembeni kuna mitaro mikubwa inayohatarisha usalama wa watembea kwa miguu. Lami nayo imeparazwa parazwa na nyingi zimeshabomoka. Kwa kifupi miradi mingi iliyotekelezwa kipindi hicho ilikuwa inafanyika ili tu watu wapige fedha. Magufuli anafanya vizuri sana ila tu ugumu anaokutana nao unatokana na mazoea ya yetu ya nyuma ya kupenda kuishi kwa ujanja janja bila kufanya kazi.

JK kama binadamu wengine alikuwa na mapungufu yake kama JK, lakini kiutendaji naiona nia yake ilikuwa njema kwa Taifa hili.
NAOMBA UNISOME HATUA KWA HATUA.
.
Binafsi nimetembea Tanzania mikoa yote kuanzia Bukoba mpaka Mtwara kupitia njia mbalimbali na wilaya nyingi nimetembea pia, huko nyuma kufika bukoba au musoma ilikuwa lazima upite Kenya, lakini kupitia barabara hizi zlizojengwa chini ya kiwango tunapita ndani ya tanzania kufika karibia mikoa yote angalau kwa wakati muafaka.. Kutokea Singida Manyoni unaweza kupasua itigi ukafika Kigoma usiku bila kulala njiani, Kutokea Dodoma unaweza kufika Iringa na Mbeya kwa wakati kupitia mtera, kutokea tunduma unaweza kufika Rukwa na ukipenda unaweza kwenda mpanda kupitia kibaoni kwa Pinda, kutokea Songea unaweza kufika masasi na mtwara kupitia tunduru, unaweza sasa ukatoka Singida ukafika Arusha kupitia Babati, Unaweza kutoka Shinyanga ukapita tinde, kahama ukafika Bukoba, Unaweza kutoka Mwanza ukapita Geita ukafika Bukoba, Unaweza sasa kutoka Musoma ukafika sirari border kwa wakati, Unaweza toka Tanga ukafika Horohoro border ya Tanzania na Kenya upande wa Mombasa, Unaweza sasa kufika Msumbiji kupitia daraja la umoja pale mtambaa waswala ukitokea Mtwara, Mbeya Chunya mpaka Tukuyu kutokea Mbeya unaweza kupita sasa, Unaweza kufika Namanga kutokea Arusha bila shida kwa sasa, Kigoma wanafahamu kilichofanyika pale Maragarasi, BARABARA HIZI ZOTE NIMEPITA NAKUONA KWA MACHO YANGU NA ZIMEJENGWA AWAMU YA NNE JAPOKUWA KUNA VIPANDE VIDOGO HUWA VINAKARABATIWA KWA MAANA YA UBORA ULIOSEMA, LAKINI KUNAPITIKA NA TUNAFIKA. Ndio awamu pekee tuliyoanza kushuhudia barabara za mijini zikijengwa kwa kasi Mwanza, Arusha, Dar, na Mbeya.

Binafsi najua na nimewahi kufika na kuona kilichotokea pale MADIMBA PLANT MTWARA ( mtambo wa kuchakata gas kutoka baharini), nafahamu na kuona mradi wa bomba la gas 600KM kutoka Mtwara kufika Dar. Nafahamu pia awamu ya nne ndio pekee imeweza kuzarisha MW nyingi za umeme kuliko awamu tatu zote za nyuma ukiunganisha, Awamu ya Tatu ya BEN ndio awamu palipoanzia figisu za kukodisha mitambo ya umeme na si kuwaza kumiliki mitambo yetu refer SONGAS, IPTL nk, Awamu ya nne ndio pekee iliweza kuanza kuijengea TANESCO uwezo wa kumiliki mitambo ya gas ya kuzarisha umeme, 100MW UBUNGO POWER PLANT, 75MW TEGETA POWER PLANT, 60MW HOF plant Mwanza, 20MW Mtwara power plant, na viplant vingine vidogovidogo ambavyo intotal tuliweza kuwa na zaidi ya 600MW na mwisho JK anaondoka akaacha KINYEREZI IN CONSTRUCTION.
HILI LIFUATILIE VIZURI NA KWA UNDANI KWENYE WEBSITE YA TANESCO UONE NI MITAMBO GANI TANESCO WANAMILIKI NA ILIKUJA AWAMU GANI.
Ni awamu hii pia ya JK ndipo REA ilianza na nyumba za udongo vijijini zikaanza kupata umeme. MENGINE KWENYE UMEME YAFUATILIE UTAJUA MENGI.

MLOGANZILA HOSPITAL PALE DAR, BENJAMINI MKAPA HOSPITAL PALE DOM, JK HEART INSTITUTE PALE MUHIMBILI Hizi zote ni hospitali kubwa zilizojengwa awamu ya nne wakati huko nyuma kuanzia awamu ya tatu na ya pili hatukuona ujenzi wa hospitali kama hizi bila shaka hata awamu ya kwanza nyingi tulirithi za mkoloni.

Upande wa Elimu pia utaona ni awamu ambayo iliweza kuongeza idadi ya wanafunzi secondary mpaka vyuo vikuu kwa kuviongezea uwezo vyuo kudahili wanafunzi wengi, na hapa ndipo ikajengwa UDOM na shule za kata nyingi, Ni awamu ambayo ilitoa hamasa kwa vijana wengi kwenda kusoma ndani na nje ya nchi nahisi pia awamu hii ndio Degree na Diploma ziliongezeka na kuwa nyingi kupita kiasi.

Upande wa biashara hili halihitaji maelezo mengi kila mtu hapa ni shahidi, Ujaribu pia kufanya uchunguzi kwenye mashirika ya ndege kama Ethiopian airlines na Emirates upate records za watanzania waliokuwa wakisafiri kibiashara kwenda nchi mbalimbali, Maana Ethiopian airlines ilifika kipindi nusu ya abiria kwenye ndege kwenda Guanzhou wanaongea kiswahili.

UKWELI ULIOWAZI PASIPO NA UNAFIKI HUWEZI HATA KIDOGO KUMLINGANISHA JK na awamu mbili zilizomtangulia, JPM tutamhukumu baada ya miaka kumi na yeye.
 
Hapa wala si mambo ya kuhukumu kiongozi baada ya kumaliza muda wake..mambo yote yako wazi kwa nini utathmini baada ya miaka 10 wakati miaka hii 3 tu imefunika miaka 10 ya yule aliyetangulia??? Kwanza habari ya REA aliyebuni kuleta huo mpango ni Mkapa, hizo barabara unazosema hata kama ni nyingi vyovyote vile..kama zinajengwa chini ya kiwango ni sawa na bure..na hilo ndilo linaondoa sifa zote nzr za seikali awamu ya 4, hakuna umakini, wizi na ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na utegemezi wa kiwango cha juu..huwezi jenga nchi na mentality attitude za hivi..SAHAU! unasema TANESCO kujengewa uwezo kumiliki vyanzo vya kufua nishati..unaelewa unachosema kweli, kipindi waziri wa nishati karamagi anasafiri na mihuri kwenda london kuuza rasilimali na kufunga mikataba ya wizi ndiyo kujengea uwezo TANESCO??? Kilichotokea mambo ya richmond ndiyo kujengea uwezo TANESCO??? madeni yote ya TANESCO uliza yalikuwa makubwa awamu gani??? watu wanatengeneza uhaba wa umeme makusudi ili wauzie serikali umeme, maji yanatumiwa vibaya mtera na kidatu ili watu wauzie serikali umeme...na kiongozi mkuu yupo hana habari kabisa juu ya hujuma km hizi!! Hizo hospitali umetaja ndiyo kipaumbele kuboresha sekta ya afya??? unajenga JKHI wakati wamama wanajifungulia watoto chini sakafuni, kama siyo laana hiyo ni nini?? au wanalazwa mzungu wa nne ndio sawa hivyo?? mwenzake wa sasa vituo vya afya zaidi ya 300 vipya vinajengwa vikiwa na huduma zote za msingi hasa za mama na mtoto, na hayo ndiyo yanahitajika kuinua sekta ya afya nchi kama hii..Hiyo elimu unayosema unajenga UDOM nani atafika UDOM km huku chini kuko ovyo???shule karibu zote za sekondari za serikali zilikuwa hoi bin taabani kimiundo mbinu..majengo yalikuwa yamechakaa, mabweni yanavuja, library zilikuwa zmebaki jina tu..unajenga vyuo unaacha kule wanatokea wafike huko juu??kipaumbele gani cha namna hiyo kama si bora kufanya ili ionekane angalau tumefanya!! sasa hivi ndani ya miaka hii 3 shule zote za sekondari za serikali zimefanyiwa ukarabati mkubwa majengo yamerudi kuwa mapya tena ili watoto wasome kwenye mazingira yanayostahili elimu kutolewa..Lakini mbaya zaidi kujenga tabia ya wizi, uzembe, kutowajibika, ulalamishi na utegemezi..kweli utajenga taifa imara lenye watu wa tabia za hivi..angeendelea kidogo tu nchi ingerudi utumwani tena! si lazima uwe kama ule wa enzi kabla ya uhuru lakini utumwa mamboleo..nchi inaongozwa na kundi dogo la watu wanaoishi ughaibuni! unasifu safari za watu kwenda china unaelewa maana yake?? unageuza nchi yako kuwa BAZAAR COUNTRY halafu unaona umepiga hatua?? huo si ni ujuha..Mwisho..pamoja na safari zote hizo ndani ya miaka 10 unaweza kuonyesha, viwanda au uwekezaji wowote hasa kwenye sekta zinazoajiri watu wengi nchini, kilimo au hata utalii ulifanyika kama zao la safari hizo..ukitaja hata miradi 3 tu, yote niliyoandika nayafuta!!!
 
Back
Top Bottom