Baba jayaron
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 4,007
- 5,446
Ashmkum si matusi ndugu yangu una laana ya ukoo wako yaani makubwa aliyo yafanya kikwete huyaoni?? mabarabara, zahanati, michezo na burudani,kukua kwa uhusiano wa kimataifa, ukuzaji wa demokrasia vyoooote hivi unaona ni upuuzi??? unakuja unatukana watu wanaomuona Kikwete ni bora kwa wakati wake!!!!Hili suala linaniumiza sana kichwa kila napofikiri. Mwaka 2005 nlikuwa nikifanya masomo yangu udsm wakati ambao kila kona vijana walikuwa na heka heka katika harakati za kuchagua rais.
Nakumbuka sana walivyokuwa wamejawa na kimuhemuhe cha kumchagua ndugu kikwete awe rais wa tanzania. Nlikuwa nikipenda kuwauliza vijana wenzangu na wasomi wa miaka hiyo.
Kwa nini hasa walipenda kumchagua kikwete kuwa rais? Majibu waliyotoa yalichoma moyo wangu kwa kiasi kikubwa sana.nliugua na kusononeka kutokana na majibu haya.
1. Ni kijana mwenzetu
2. Huwa anaenda klabu
3. Anaingia mpirani kutizama mpira na sisi
4. Anapenda sana kula bata
Wale walitoka bush wakaenda mbali zaidi na kusema ni hendisamu.
Nliukunyata moyo kwa masikitiko,majonzi na huzuni kubwa. Yaani Dr Salim A. Salim alionekana hafai. Hakuna aliyemfikiria kwa sababu hizi? Iliumiza sana moyo wangu. Tuliyokuja kuyapata Mungu mwenyewe anajua.
Ni mwendawazimu tu ambaye atamchukia magufuli na kumpenda kikwete. Ni mwendawazimu na pia mpumbavuh. Ashakum si matusi. Unawezaje leo kumchukia magufuli ukasema unampenda kikwete?
Ilhali magufuli anatokana na kile alichofanya kikwete? Ni wangapi tunakumbuka hata wapinzani walisema sasa anatakiwa apatikane rais dikteta?maana tulishachoka na kucheka cheka na nyani tukaishia kuvuna mabua?
Mungu aliwajaalia watanzania kuwa wasahaulifu na wanafiki sana.nadhani katika afrika kma si duniani watanzania ni watu wanafiki hawajawahi kutokea.ni hawa leo wanaomtetea patel,rugemalila na manji
Lakini ni hawa miaka kadhaa iliyopita walikuwa wakisema kwa uovu watu hawa. Ni watanzania hawa hawa ambao wanasema wanamtaka membe awe rais.katika watu wote...membe? Huyu huyu aliyekuwa akiandikwa kwa kashfa nyingi humu JF?
kikwete aliharibu dhana nzima ya Urais tanzania. Akaleta Urahis. Urais ukaonekana ni kitu Rahis. Ni muda wa kutembea dunia nzima kuomba omba...na watu kweli kama watoto wamfuatavyo baba hawakuona thamani ya kazi au kusoma.
Walidumbukia kwenye utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.ikawa ajira rasmi kabisa.kwani ninani asiyefaham ajira hii ilivyotajirisha wakubwa kwa wadogo? Wenye vyeo na wasio na vyeo?
Ni kipindi ambacho kuiba mali au pesa ya umma ilikuwa ishara ya ujanja na mafanikio.na wezi wapo mpaka leo waliogawana pesa za watanzania.huku rais wao akisema akiwakamata nchi itayumba.kauli ya hovyo kupata kusemwa na mtu ambaye tumempa dhamana ya urais.
Miaka zaidi ya 10 baada ya kupitwa na janga hilo bado watanzania hatujui tunataka rais wa namna gani.wanakuja watu kusifia kuwa flani anafaa kuwa rais sababu ni mpole, hana makuu,mnyenyekevu, mtanashati n.k
Ni wazi bado vijana wengi na hta wazee ukiwauliza mnataka rais wa namna gani wasijue. Watakosa sifa au watataja tena sifa za majanga mengine ya kitaifa hapa nchini.watanzania tunasahau sana.
Pengine kwa umbumbumbu au kwa kutumika na baadhi ya watu. Na katika hili tumeweza hata kuondoa Unyeti wa taasisi ya urais.now every tom,dick and harry thinks can be a president.
Tuliona mwaka 2015 watu wa hovyo hovyo bila hofu waliamua kuchukua form za kugombea urais.katiba inaruhusu lakini hii haimaanishi sasa watudharau kiasi hiki.waamini kuwa upumbavuh tuliokuwa nao mwaka 2005 na kuendelea nao mpaka leo upo.
Tufikie hatua tuwaheshimu watanzania.msilete watu wa hovyo hovyo kuwapigia debe kutaka wawe marais wa nchi hii mama ya tanzania.
Nasisitiza tuheshimiane.kuna mjanga hayaepukiki kama mvua,ukame,njaa,tetemeko na kimbunga.lakini la kuchagua rais kilaza hilo ni la kujitafutia.tusifanye tena majaribio.
"Nakulilia tanzania, unajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo"
we jamaa usijitoe ufahamu kabisa ebu angalia maamuzi machache anayo yaamua Rais wetu na impact yake kwanza pitia ishu ya korosho, ndege, thamani ya Tsh yetu na kuanguka kwa makampuni mengi then uniambie kwa maamuzi haya Je huyu ni BORA kuliko JK???
NB: tumia akili kutafakari na si mihemko au Tumbo