Miaka michache ijayo, ibada zitakuwa kama ifuatavyo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka michache ijayo, ibada zitakuwa kama ifuatavyo.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mojoki, Sep 25, 2012.

 1. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Miaka michache ijayo, ibada zitakuwa kama ifuatavyo.
  MCHUNGAJI: Bwana asifiweeeee!
  WAUMINI: Ameeeeeeeeeni!
  MCHUNGAJI: Tafadhalini washarika sasa tuchukue iPad,
  tablet PC, simu na kindle zetu ili tufungue 1 Wakorintho
  13:13. Pia washeni bluetooth zenu ili muweze kupokea
  mahubiri. Mnaotumia facebook, twitter, BBM na Whatsapp
  mnaweza kuendelea kupokea mahubiri haya. Tafadhalini
  washarika mnaweza kutumia Wi-Fi ya kanisa kwa uhuru
  kabisa kwa kutumia nywila ya IMANI613. Haleluuuuuuuyah!
  WAUMINI: Haleluuuuyaaaaaaaah!
  MCHUNGAJI: Wapendwa washarika sasa ni wakati wa
  sadaka kwa hiyo kadri ya itakavyokupendeza kumtolea
  Mungu unaweza kutumia credit ama debit card, pia unaweza
  kutoa sadaka kwa njia ya MPesa, Tigopesa, Airtel money
  ama ZPesa kupitia namba zinazoonekana kwenye skrini.
  WAKATI WA MATANGAZO
  KATIBU WA USHARIKA: Wapendwa washarika wiki hii
  kutakuwa na mikutano ya kiroho kupigia group letu la
  Facebook. Mada kuu itakuwa uponyaji wa kiroho kwenye
  ndoa. Washarika wote mnakaribishwa kushiriki.
  Siku ya Alhamisi kutakuwa na mafundisho ya Biblia moja
  kwa moja kupitia Skype kuanzia saa moja jioni. Tafadhali
  msikose kushiriki. Pia mnaweza kuendelea kufuatilia ibada
  hii pamoja na mafundisho yote kutoka kwa mchungaji
  kupitia akaunti yake ya Twitter.
  Haleluyaaaaaah!
  WAUMINI: Ameeeeeen!


  Source, Nimeiba fb
   
 2. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Very possible chief. Great thinker!
   
 3. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mpesa, Airtel money on work through our church..

  Near by Soweto Mbeya.
   
 4. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,993
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Umesema umeiba! no, its just a reference!
   
 5. p

  pilau JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwa taarifa yako hayo mambo ya mitandao na ibada katika hali ya kisasa tayari yameshaanza katika makanisa tembelea kanisa la Winners Chapel linaloongozwa na Askofu Dr. David Oyedepo liko Banana Ukonga DSM,wachungaji na baadhi ya waumini wanatumia iPad katika kuhubiri au kusoma Biblia ibada zinarushwa moja kwa moja kupitia sitelite ambapo ibada moja inaongozwa na yeye akiwa Cananland Nigeria na anawahudumia waumini wa madhehebu hayo duniani kote kwa wakati mmoja, hayo mambo ya M -Pesa Airtel money na tiGo pesa ni jambo la kawaida katika makanisa, makanisa hayo yamefikia hatua ya kutoa usafiri wa bure kwa waumini wao kwenda na kurudi kanisani katika maeneo mbalimbali ya DSM kama Kigamboni, Mbezi, Mbagala na Tegeta, Bwana Yesu Asifiweeeeee
   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mbona hii ya kutoa sadaka kupitia mitandao ya simu ipo sasa
   
 7. Manager

  Manager JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anti, nimekukubali kwa wizi mzuri!
   
 8. a

  anin-gift Senior Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mkuu toka uji ziwa mpk now mtandaoni? ingekuwa enzi zetu ungeiadisia hii kwa kina munuo na ben au dom usiku watu wacheke kabla tilya hajapita
   
 9. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Dah we jamaa umenijuaje???, ebana eeh kumbe unaingia pia humu Brother
   
 10. K

  Kiny JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kweli mkuu dunia inakonda**.........*
   
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,311
  Likes Received: 13,019
  Trophy Points: 280
  Sayansi hahahah
   
Loading...