Miaka hii 5 imenifanya niwajue rangi zao halisi, si wakweli

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Naam wanajukwaa,
Mzigo umeletwa tena wa kutosha ni tani kadhaa. Ni solution ya mitishamba kutoka Madagascar. Wanaiita ni dawa ya kufubaza virusi vya corona. Kwa mujibu wa maelezo yao wanasema tumepewa msaada. yaani tumepewa bure kabisa. Umewaamini?

Mimi sijaamini hata kidogo labda mpaka CAG akague ankara za pale Hazina na ile ofisi nyingine. Awamu hii kutumia rupia za wananchi kwa mambo hata ya kisangoma ni kawaida sana. Muda utasema.

Jingine ni kwamba wanasema hatuanzi kuutumia ule mzigo mpaka ufanyiwe utafiti wa kisayansi! Halafu msimamizi ni Kagundi Mwalimu wa Kiswahili! You know why? Wanalenga kuidanganya Dunia na hasa WHO kwamba hawajaanza kutumika kumbe usikute tayari watunga sheria wamepewa ili waendelee na shughuli zao wakiwa wametuluzwa Kisaikolojia.

Kama lengo lingekuwa ni kufanyia utafiti kwanza si wangeagiza lita hata 100 tu ili kubana matumizi? Za kuambiwa changanya na zako.

Mzigo umefika sasa kwanini Kabudi aendelee kuwa msemaji? Kwanini asiupeleke kwa mkemia mkuu au Chakula na dawa huko? You can fool all the people some time and some of the people all the time but you can not fool all the people all the time!

Binafsi nimeijua awamu hii vizuri mno. Kwanza wanaamini fedha za Nchi hii ni zao wanaweza kutumia vyovyote vile.

Pili wanaamini sheria,kanuni na taratibu ziliwekwa kwaajili ya watu vyama vya upinzani. Wao wanaweza wakafanya chocho popote kwa yeyote na wasiulizwe.

Hii dawa haija thibitishwa na mamlaka za tiba za kidunia.Unaanzaje kutumia mamilioni ya fedha za umma kufuata kitu fake?

Mapendekezo yangu ni kwamba kuwekwe Auditing special ya watu wote watakao pewa dawa hii ili madhara ya kitokea basi kuna watu wawajibishwe !

Pili, CAG afuatilie kuona mzigo hautumiki mpaka matokeo ya utafiti yatoke.

Nijuavyo rangi zao hawatakubali.
 
Hebu nisaidie hapa; inawezekanaje kutuma ndege kwenda Madagascar kuchukua mzigo mpaka tunaoneshwa picha ndege yetu imetua kule, then after tunaoneshwa imesharudi na mabox kadhaa ya dawa, halafu baada ya hapo tunaambiwa wanaenda kwanza kuyafanyia utafiti!.

Why our leaders nowadays are mentally so vulnerable?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu tunadanganya eti kuna ofisi ya utawala bora? Mbona viongozi wasio bora ni wengi sana na hawafanywi chochote?

PCCB wapo na wanaona Ndugai akichezea fedha za umma wapo kimyaa!:Nchi hovyo Kabisa.
Hawawezi fanya kazi bila maagizo toka juu labda tu Kama ni ya kuwashughulikia wapinzani hapo awasubiri maagizo ili kumfurahisha mkoloni
 
Hawawezi fanya kazi bila maagizo toka juu labda tu Kama ni ya kuwashughulikia wapinzani hapo awasubiri maagizo ili kumfurahisha mkoloni
Udhaifu wa ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka, utawala bora na hata PCCB ndio unafanya watu wavunje katiba.
 
Afu yule Waziri anakunywa wakati haijathitishwa, hehehe!

Kuna movie ya animation inaitwa Rango, kuna sehem Rango anaambiwa wenzie "tusinywe haya maji kwa kuwa ndio the only hope we have" hivi mfano wewe ukichukua kidogo kama hivi ukanywa, yule akachukua kama hivi akanywa haya maji si yataisha, wakati huo anaonesha yote kwa vitendo huku kashika glass na kunywa kabisa".

Alexander The Great
 
Wanasiasa wameona kitu inawachukua wameona wajichukulie yao. Hapo waziri, wabunge chamachao na jamaa yao wanakunywa kujilinda sisi walalahoi tunaambiwa ni ya utafiti?

Ingekuwa hii nchi tunajielewa tusingeruhusu uongozi wa namna hii kuendelea kukalia ofisi za umma.
 
Afu yule Waziri anakunywa wakati haijathitishwa, hehehe!

Kuna movie ya animation inaitwa Rango, kuna sehem Rango anaambiwa wenzie "tusinywe haya maji kwa kuwa ndio the only hope we have" hivi mfano wewe ukichukua kidogo kama hivi ukanywa, yule akachukua kama hivi akanywa haya maji si yataisha, wakati huo anaonesha yote kwa vitendo huku kashika glass na kunywa kabisa".

Alexander The Great
Ndio maana wazungu wanatuona bado tuna undergo biological changes hatujawa fully developed
 
Mkuu hakuna wq kuwawajibisha. Ila kabudi inasemekana wiki zlzopita alikuwa na hali tete wakamconvice mkuu wakafate dawa ya madagascar. Kumbuka madagascar iligawia nchi kadhaa hii dawa na Tz haikuwa kwenye list ya mgao. So wakatafta njia yoyote wapate ili watibu afya zao.

Cha msingi tunajua hii dawa mpaka sasa Magufuli na kabudi wameshakunywa. Ngoja tuwaone maendeleo yao.

Mimi naomba iwageuze kuwa Mabubu ndio watajuta kuwaamini masangoma. Dawa ya Loliondo iliwamaliza rafiki zangu watatu walio enda kunywa.
 
Back
Top Bottom