Miaka 50 ya umaskini Tanzania

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,516
1,865
Nikiwa nimefikisha miaka 42 ya umri tangu kuzaliwa, nikiwa nimezaliwa ktk nchi ya kimaskini kabisa, naendelea kupata tabu kuwa hali ya maisha ya mtanzania inashuka, japo kuwa mi nikiangalia hali yangu ni nzuri nikilinganisha na baba yangu japo kuwa kwa sasa ni marehemu. Lkn inabidi watanzania tujilaumu kwa kuweka madarakani wahuni ambao wameangusha uchumi wa nchi.

Pole wanajamii kwa kufikisha miaka 50 ya umaskini. Japo nimeshangaa Wizara mbalimbali zimetenga pesa nyingi za kusherehekea hiyo miaka ya umaskini!! si hizo pesa wangewalipia wadogo zetu wanao hangaika na pesa za chakula ambao wanacheleweshewa.

Tena nimepata habari kuwa wafanyakazi wa umma wamekatwa pesa bila taarifa. Hahahahaaaa nchi hii bwana.

MUNGU AWABARIKI SANA WANAJAMVI NA WKD NJEMA.
avatar32881_1.jpg
 
Kutoka ndege 11 za Air Tz mpaka 1 iliyofungwafungwa kwa mipira na inaendeshwa na wafanyakazi 300 wanaolipwa mishahara na wengine wanaajiriwa kila mwaka?

kubadili mwatex,mutex,sunguratex,urafiki na kuwa maghofu ya kufugia mende?

Kuifanya general tire kuwa ukumbi wa harusi?

Mwalimu alisema,yaacheni madini watanzania wakisoma watakuja wachimbe na wafaidi madini yao,wakihitaji barabara wachimbe madini yao,wakihitaji maji wauze madini yao,wakihitaji shule wauze madini yao,leo ukiangalia shule hamna,barabara hovyo,maji hata Geita hamna,wanachoambulia watanzania ni vumbi na mahandaki

Hakika hiki kizazi cha akina JK kimefuja na kimeiba vya kutosha lakini ipo siku tutawaita na watatajana kwa majina na watarudisha mali za zetu zote tena kwa bakora
 
Back
Top Bottom