Miaka 50 ya uhuru wa tanzania na ukweli

MR NDEE

Member
Aug 2, 2011
54
21
Ni saa chache zimesalia kufikia siku ya kumkumbuka baba wa Taifa mwl Julius Nyerere,japo si vema kumuenzi siku moja,lakini kuwepo siku hiyo ni kuonyesha kumjali ikiwa tafakuri zake zitafanyiwa kazi kila siku na muda wote vinginevyo siku hiyo haina maana. jambo hili ni muhimu ili kukimbilia maendeleo ya ukuweli yenye haki na uadilifu kwa wanyonge kwa kutumia rasilimali za wanyonge.

Mwanzon nilisita mno kuandika makala hii kwani kwa desturi za kale mkubwa hakosei wala hakosolewi. kwa desturi za kale baba hakosei wala hakosolewi ni ni laana kumuambia baba umekosea jambo kadha wa kadha , viongozi wetu baadhi wameikiumbatia mila hii potofu ya mkubwa (kiongozi) hakosei wala hakosolewi, ndio maana utamshuhudia mbunge ndani ya bunge akitoa maoni waziwazi kuwa vyombo vya habari vinavyoonesha hali mbaya za maisha kama kutoa picha za mashule na mahospitali vilivyoharibika au kuchakaa ni kudhalilisha Taifa, kuonyesha watoto wamekaa katika mjengo wa nyasi chini wanasoma ni kudhalilisha Taifa vyombo hivi vifungiwwe mara moja,. kauli hii inatoa maana hiyo ya wakubwa wako sahihi na kusema UKWELI NI MWIKO. hiii ilinikumbusha kitabu cha kivuli kinaishi ambapo mtawala Bi Kirembwe ndio aliruhusu nani aseme na aseme nini, lakini nimesonga mbele kutokana na maneno ya Shakespeare aliposema "coward die many times before their death" sito acha kusema na nikaamua kuandika*

Tukisema Tanzania kuna demokrasia tuna maanisha kuna uhuru wa kutoa maoni Mwl Julius Nyerere alipata kusema "kuna mambo mawili ya lazima katika demokrasia; ukiyakosa hayo demokrasia hakuna. la kwanza ni kwamba ni lazima mtu aweze kusema kwa uhuru kabisa na maneno ya kila mtu lazima yasikilizwe"

Tunaelekea kusheherekea miaka 50 ya uhuru, je ni kweli tunasheherekea? tunasheherekea kipi? kwa faida ipi na ya nani? Sir W Scott alipata kusema "The best part of life is not *the number of years *we live but achievement we gather to our credit. it doesnt matter if a man lives for hundred years without being able to make best use of his abilities and opportunities........"*

Hivi ni KWELI serikali kwa miaka 50 imetumia uwezo wake wa mwisho na nafasi kiukweli kufikia maendeleo? mathlani katika suala la afya hadi leo mijini na vijijini wagonjwa wanalala kitanda kimoja zaidi ya mtu mmoja, madaktari *wachache madawa hakuna kwenye vituo vya serikali unaambiwa ukanunue duka binafsi *iwejie serikali ikose binafsi wapate? viongozi wakiumwa wanakimbilia ulaya au India je wanauchungu na wanyonge na maskini? hadi leo shule hazina walim ukiuliza utambiwa kuna mpango wa dharura umeandaliwa.

mikataba mibovu na maamuzi mabaya yameliingiza Taifa letu katika umaskini wa kutupa nazo sera zisizotekelezeka zimejaa na ndugu yake sasa amezaliwa anaitwa mpango wa dharura,mfumuko wa bei naO umeongezeka utaambiwa kuna vita Libya au dola imeshuka mtikisiko wa kiuchumi Marekani au *mvua na umeme, leo hii sukari Tsh 2400 mafuta ya taa 2000 unga wa ugali 600 ukijulisha ni Tsh 5000 bado matumizi mengine inamaana kwa vitu hivyo tu kwa mwezi na laki na nusu ni mlala hoi yupi "atakayeweza" kama kauli mbiu inavyosema au amewezwa? je bado tupige makofi na tupewe kanga na tisheti tushangilie? je ni KWELI?*

Ukiyasema haya utaambiwa msiwaskilize mavuvuzela au nyie sio wazalendo je uzalendo nikutokusema kweli? Tunasema ya kwamba WALALAHOI TUNATESEKA NA TUNAENDELEA KUTESEKA MIAKA 50 YA UHURU IFIKE MWISHI WOTE TUPATE KEKI HUU NDIO UKWELI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom