Miaka 50,ya uhuru Tanganyika,Waalimu pekee ndo wanastahili utumishi uliotukuka

TASLIMU

Senior Member
May 6, 2011
144
21
Pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi,lakini wanatoa wahitimu,chekechea mpaka chuo.
2.wanajeshi nao wanajitahidi
3.wauguzi na madaktar
Walioboronga miaka 50
1.wanasiasa(wanashibisha matumbo yao)
2.wanasheria&mahakama(mikataba mingi ya kinyonyagi,wapo kimaslai)
 
:A S embarassed: Waalimu kweli wanastahili sifa. Japo kila kukicha wanatishiwa kupigwa virungu kama wakiandamana, lakini bado wanaifanya kazi yao kwa moyo. Hawa wanasiasa hawana lolote zaidi ya kujali matumbo yao na familia zao.
 
Waalimu nao wameshachakachuliwa tu na mfumo m'bovu. Hawana motisha na wanakazania tuition na kuuza vitini vya kufundishia! Huyu mgonjwa wa kufa, akiweza dawa hawezi uji! Kha!
 
Hata waalimu wanaangalia maslahi yao siku hizi na sio ya wanafunzi. Wanaona kama hamna anaewajali wao nao hawana haja ya kujali.
 
Ila bado wanapiga mzigo pamoja mazingira,nyie nyote humu JF mmefundishwa na waalimu,na watu wanaojua kusoma na kuandika,ila walimu pekee ndo wanaishi maisha magumu!Waalimu MgomoWetu ni mwezi huu january 2011,GOMENI
 
Hapa Tanzania, serikali ilikwishaapa kuwa walimu siyo viumbe wenye stahili ya kupata maisha bora, daima dawamu.
"Kama walimu mnataka maslahi bora, acheni kazi hii mkatafute kwingine--Hawa Ghasiya:shock:
 
Wengi wanaenda kusoma MBA,siasa
 
Hapa Tanzania, serikali ilikwishaapa kuwa walimu siyo viumbe wenye stahili ya kupata maisha bora, daima dawamu.
"Kama walimu mnataka maslahi bora, acheni kazi hii mkatafute kwingine--Hawa Ghasiya:shock:
Mungu wangu wamekula........... wameshiba......... wakavimbiwa.......... sasa wameanza kulewa...... Mungu yupo na atakuwepo 2015:focus:
 
Tatizo hawaijui shida ya walimu hawa kwani watoto wao hawasomi shule hizo ama wako nje ya nchi au wasoma shule za ''international ".. Wanataka kuzalisha jamii ya wajinga ili waendelee kukaa madarakani milele... Ole wao
 
Mwezi wa mgomo ndo huu,kwa waalimu,waache bla bla!wakaze wafungue mwaka,kwa mgumu
 
Mwezi wa mgomo ndo huu,kwa waalimu,waache bla bla!wakaze wafungue mwaka,kwa mgomo
 
Back
Top Bottom