Japo mara nyingi marehemu husifiwa hata pale ambapo hakufanya vizuri LAKINI kwa Kighoma Malima yatosha kusema kuwa tutamkumbuka kwa maisha ya unafiki tangu ujana wake. Formal education aliyoipata ilikuwa STD IV, kwa unafiki alijiweka karibu sana na Wamisionari hata wakadanganyika kuwa alikuwa mfuasi wao kuliko waumini wao wa wakati ule. Wakamwendeleza mpaka kufikia kumlipia masomo yake ya Chuo Kikuu. Kwa kuendeleza unafiki wake, kwa dhamira maalum, aliamua kumwoa mwanamke mkristo, na Jumapili zote akawa akienda kanisani, na akajifanya mwumini mkubwa wa Mwalimu katika falsafa ya 'serikali haina dini'. Alipoingia Mwinyi akapewa wizara ya Elimu, huko akatangaza kuwa idadi ya wakristo waliosoma inatosha, sasa ni wakati wa kuwasomesha waislam - aliyasema hayo akiamini kuwa atapata uungwaji mkono wa jamii ya kiislam na Rais Mwinyi. Akatenga sehemu ya ofisi za wizara kuwa sehemu ya kuswalia (msikiti). Alipostaafu mkurugenzi wa wizara ya elimu, na msaidizi wake kufariki, alienda msikitini na kusema kuwa, 'kuna mkurugenzi pale mkristo amestaafu, akaniletea taarifa hiyo, nikasema sawa, nikamweka kwenye nafasi hiyo muislam mmoja safi ambaye watu walikuwa wamemkalia; kisha msaidizi akafariki, nikasema naam, na hapo nikamweka muislam mwingine. hatimaye nikaondolewa kupelekwa wizara ya fedha, sikusikitika kwa vile nilikuwa nimefanikisha malengo yangu'.
Akiwa waziri wa fedha, ndipo serikali ilipofilisika kwa namna ambayo haijawahi kutokea, pesa ya misaada iliporwa na kuwekwa kwenye akaunti zake mpaka kufikia mashirika yote ya kimataifa na mataifa ya Ulaya na Amerika kusimamisha misaada yote kwa Tanzania. Baada ya kuvurunda kwa namna ya ajabu, Mwinyi hakuwa na chaguo zaidi ya kumfukuza kazi, aliambiwa ajiuzulu saa 3 asubuhi, na saa 4 asubuhi siku hiyo hiyo ilitangazwa kuwa Rais ameridhia. Baada ya hapo akaanza kwenda misikitini akitangaza kuwa Mwinyi amemwondoa kwa sababu ya kuwatetea waislam. Akajiunga na Chama cha NRA, na akiwa Tabora msikitini akatangaza kuwa angegombea Urais. JK, alipochukua nafasi ya Uwaziri wa Fedha, kama namna mojawapo ya kurudisha imani kwa jamii ya kimataifa alizifunga akaunti zote za nje za Kighoma Malima. Kighoma Malima alipoenda Uingereza kuchukua fedha kwaajili ya kuendeshea kituo chake cha redio kilichokuwa kikihamasisha siasa za kidini, akaambiwa kuwa serikali ya Tanzania imeomba kufungwa kwa akaunti zake za benki nchini Uingereza, siku hiyo hiyo, usiku, Mkuu wa Maisha na pumzi yetu, ambaye ukuu wake hauhojiwi, aliichukua roho ya kiumbe wake.
Tunamwombea kwa Muumba wetu, amrehemu kadiri ya mapenzi yake.