Miaka 50 baada ya uhuru. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 baada ya uhuru.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jaguar, Oct 5, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna mzungu mmoja namjua kwa jina la Mark anamiliki hekari mia kadhaa za ardhi mitaa ya kijiji cha Ifunda.Kwa kifupi huyu bwana anawanyanyasa sana wanakijiji wanaoishi maeneo yanayozunguka mashamba yake.Siku moja nilikuwa nikipata lunch baada ya kazi pale Ifunda ndipo nikashuhudia akina mama kadhaa wamekamatwa na walinzi wa kimasai wa huyu mzungu.Kosa la akina mama hawa lilikuwa ni kutafuta uyoga na kuokoteza kuni ndani ya eneo la huyu mzungu.Kwa kosa hilo,walipelekwa kituo kidogo cha polisi ifunda na kuchapwa bakora kadhaa na kuonywa wasirudie tena.Walinzi hawa wa kimasai inasemekana wamekuwa wakiwakamata watoto wadogo wanaojaribu kuvua vijisamaki katika kijito kinachokatiza eneo la huyu mzungu na kuwapiga sana.Kama haitoshi,watoto hawa hulazimishwa kuwatafuna hao samaki waliowavua wakiwa wabichi vivyo hivyo.Mbaya zaidi inasemekana J.K ni swahiba wa karibu wa huyu mzungu na mara kadhaa amekuwa akimtembelea kisirisiri huko shambani.Inanisikitisha,anyway nakutakia maandalizi mema ya sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa taifa letu.
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,136
  Likes Received: 6,631
  Trophy Points: 280
  wanafunzi wa tz.jpg

  wanasheherekea miaka 50 ya uhuru.  shule za igunga.jpg
   
Loading...