The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,147
- 20,085
Leo ni "50th birthday" ya mashine za kutolea hela, ATM baada ya mashine ya kwanza Duniani kuzinduliwa tarehe 02.07.1967 nchini Uingereza.
Leo watu wa banking wakiwa wanasherehekea miaka 50 ya mashine ya kwanza ya kutolea hela kuzinduliwa na bank ya Barclays, takwimu zinaonyesha kuna mashine hizo milioni 3 duniani kote huku uingereza kukiwa na mashine 70,000 za kutolea hela huku Tanzania hazifiki hata 1,000.
Pamoja na mapinduzi ya tekinolojia katika maswala ya pesa hasa hizi online payments platforms lakini bado umuhimu wa kua na pesa taslim(cash) bado uko pale pale katika maisha ya kila siku ya watu. Hivyo mashine hizi bado zitaendelea kuwepo kwa muda mrefu.
Unaweza kujisomea zaidi hapa:
World's first ATM machine turns to gold on 50th birthday World's first ATM machine turns to gold on 50th birthday