Miaka 5 katika NDOA!

Kweli ni jambo la kumshukuru Mungu kufikisha miaka mitano ya ndoa maana nyingine huvunjika miezi michache tu. Nikupe moyo kuwa miaka mitano ya mwanzo wa ndoa ni hatua kubwa, miaka kumi ni matumaini makubwa ...... na kuendelea hadi jubilee ya miaka 25!!! Hapo ni ushindi mkubwa sana na baada ya hapo ni kuwa ndoa ya kuigwa!! Bravo man!
 
mkuu hongera sana ni kweli ndoa ndio msingi wa familia bora kwani ndio mwanzo wa maadili yote ukishaharika tu unazaa mmomonyoko wa maadili
 
pole sana na ongereni sana si mchezo kuna mshikaji wangu kaoa juzi tu;lakini hana ata mda mambo si mambo
 
Hongera MJ, kama ulivyosema miaka mitano ni michache lakini ni mingi sana ndani ya ndoa! Kila la heri na nawatakia wewe na familia yako annivesary njema na pasaka njema huko 'idodomia'.
 
Hongera sana mkuu. Mungu awajalie kila lililo na heri na wingi wa baraka. Tuko pamoja.
 
mimi na siku nne legally having my baby with me lkn nimeishi nae miaka sita illegally....
 
mimi na siku nne legally having my baby with me lkn nimeishi nae miaka sita illegally....
 
Hongera sana Mkuu! Mbarikiwe zaidi mfike miaka 50 mkiwa pamoja na mnapendana kama wachumba.
 
Hongera Mkuu kufikisha miaka mitano.kumbe upo ndoani mi nilifikiri.......

Mpwa nimerudi ; ulifikiri nini? Ah zile kuleeeeeeeee ni chai chai tu usihofu mpwa Ni ko ndani ya himaya na leo ndo narudi rasmi dimbani maana honeymoon iliunganishwa na safari za kikazi!
 
Wana JF!

Namshukuru Mungu kwa kutujaalia uzima na afya njema! Sifa na Utukufu ni vyake yeye!
Namshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee mwanetu Junior hapo kwenye avatar! Mungu mlinde na umpe uhai hata naye aje asherehekee kama mimi leo!

Wapendwa wana JF napenda kuwashirikisha kuwa ifikapo tarehe 4 April 2010 mimi na shemeji/wifi yenu tutatimiza miaka 5 ya kuishi kama Mke na mume!

Miaka 5 sio mingi ni kweli lakini pia ni mingi katika maisha ya ndoa; Wangapi hawajafika? na siwafichi it was not a smooth ride always! Ila kwa msaada wa Mungu tumepita katika milima na mabonde na leo hii kwa ushujaa tunafurahi kuwa tulivuka na tutavuka yajayo mbele yetu kwa msaada wake yeye atutiaye nguvu! Jina la Bwana Yesu libarikiwe!

Naomba nichukue nafasi hii pia kuwaombeni kila mtu kwa imani yake; Jamani tuziombee ndoa zetu na tuwaombee wanandoa wote; NDOA ndio msingi wa Familia zetu; kuanguka kwake ni anguko la Familia na mmomonyoko wa society yetu! Familia imara zitaleta Watanzania imara wa baadaye na wenye uwezo wa kuijenga nchi yao!

Kwa nini ninaituma leo hii; Nitakuwa mapumziko kuanzia kesho kwangu mimi hii ni Double celebration ; Pasaka na Miaka 5 ya ndoa!

Nawapenda nyote

Mungu awabariki!
Hongera sana kwa kutimiza miaka 17 ya ndoa (kama bado mpo pamoja)
 
Back
Top Bottom