Miaka 5 baada ya kifo cha mzee Moses Kulola: EAG(T) inaangamia

1. EAGT ya Mosses Kulola ilisema Bikira Maria ni Bahasha tuu na hafai kuheshimiwa Kama wafanyavyo wakatoliki. Iweje unataka mke wake aheshimiwe?

2. EAGT ya Mosses Kulola ilisema wakatoliki wanamwabudu PAPA iweje mnataka yeye aenziwe si waumini watasema anaabudiwa?

3. EAGT ya Mosses Kulola ilisema kanisa Katoliki ni "njia ile pana iendayo kuzimu" (kwa sababu ta watu wengi kuelekea humo kufanta ibada) huku ikijitapa kuwa yenyewe ni "njia ile nyembamba iendayo uzimani" (vile walikuwa na Nyumba ndogo za ibada na waumini wachache).

Sasa hapo si EAGT unga LTD ikijaa Mwinjilist ataona imekuwa njia pana. Happy hata mtoa mada utaona kuwa EAGT ishakuwa "njia pana iendayo kuzimu".

Mrudi Kanisa Katoliki.
 
Matatizo hasa ya EAGT yalianzia hapa.

1/Kumjenga mtu badala ya kujenga taasisi. Waumini wengi wa EAGT wao ni Kolola, Kulola, Kuloka tu. Wapo EAGT kwa sababu ya kulola. Sasa Kulola na wapambe wake wameshatangulia mbele ya haki, kinachofuata ni kusambaratika maana kila mtu sasa ni kambale.

2/Mbegu ya ugomvi na mivutano walianza kuipanda wakati wanajitoa TAG. Ile dhambi itaendelea kuwatafuna vizazi na vizazi. Hekima, Busara na Uvumilivu vilikosekana katika ule mgogoro, na mgogoro ukazaa EAGT. Hivyo EAGT ni matunda ya mgogoro.

3/Kuacha kufuata katiba na kuaminishwa katika hekima za mtu mmoja tu kwa kisingizio kuwa roho mtakatifu amesema naye. Ni rahisi sana kiongozi dhaifu kujificha kwenye kichaka kinachoiwa 'amepakwa mafuta'
Hii shida ipo ktk makanisa mengi yanayojiita ya kipentekoste au ya kiroho. Unakuta Mchungani hata kujenga kisima tuu kanisani mpaka afuniliwe. Wale wa chini ya Mchungani hawana kubwa la kuchangia ktk ujenzi wa taasisi zaidi ya kufuata la Mchungani wenyewe wanafuata mbeba maono tu. Ukihoji unaonekana tofauti huna roho wa Mungu au unafukuzwa kanisani.
 
1. EAGT ya Mosses Kulola ilisema Bikira Maria ni Bahasha tuu na hafai kuheshimiwa Kama wafanyavyo wakatoliki. Iweje unataka mke wake aheshimiwe?

2. EAGT ya Mosses Kulola ilisema wakatoliki wanamwabudu PAPA iweje mnataka yeye aenziwe si waumini watasema anaabudiwa?

3. EAGT ya Mosses Kulola ilisema kanisa Katoliki ni "njia ile pana iendayo kuzimu" (kwa sababu ta watu wengi kuelekea humo kufanta ibada) huku ikijitapa kuwa yenyewe ni "njia ile nyembamba iendayo uzimani" (vile walikuwa na Nyumba ndogo za ibada na waumini wachache).

Sasa hapo si EAGT unga LTD ikijaa Mwinjilist ataona imekuwa njia pana. Happy hata mtoa mada utaona kuwa EAGT ishakuwa "njia pana iendayo kuzimu".

Mrudi Kanisa Katoliki.
Pole sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madhehebu mengine ya kikristo hususani ya kipontekoste yaanze kujifunza kupitia hili. Waachane na mambo ya umungu-mtu, kufanya mambo kienyeji enyeji na kushindwa kuweka mifumo ya mali za kanisa waziwazi.

Matatizo kama haya yatakuja kujitokeza hivi hivi siku Kakobe, Gwajima, Mzee wa Upako, Josephat Mwingira nk. wakipumzishwa na Mungu (Nawaombea sana kwa Mungu wazidi kuishi maisha marefu zaidi).

Sababu za msingi ni hizi hapa.
1/Waanzilishi wa madhehebu hayo wanawajenga waumini wao kuwafuata nyuma kama mikia huku wao wakiwa kama vichwa. Huu ndio umungu-mtu.

2/Kanuni na katiba za uendeshaji wa madhehebu hayo zipo kabatini tu, viongozi wanaongoza vile wanavyotaka wao. Na hakuna muumini anayeweza kuhoji. Hapo ndipo uendeshaji wa kienyeji enyeji huzuka.

3/Kanisa ni mali ya mwanzilishi wake. Mali zote kuanzia sadaka kwao huwa hazihojiwi. Ni siri ya mwanzisha kanisa. Hivyo ufujaji ni utamaduni wa kudumu kabisa.
 
Kanisa lenu limeshafitinika tangu huku chini. Kila mahala unapopita kuna vikanisa vidogo vidogo vyenye waumini wasiozidi kumi. Kanisa likikua kidogo, pepo wa mafarakano anaingia na kanisa linagawanyika. Ni nadra sana kukuta usharika wa EAGT wenye waumini mia.
Kwa hali hii, kanisa lenu haliwezi kusimama imara kwa kuwa kila mmoja yuko after personal interest.
Kila muumini ana njaa ya kufungua usharika ili aweze kukinga sadaka. Nia ya kumtumikia Kristo imepotea kila mtu yuko after personal grolification ya kuabudiwa na waumini.
Pepo la kubagua makanisa mengine ndio limeshawajaaa mwili mzima. Nyie mnapenda kujiona ni watakatifu na Wakristo wengine mnawaona kuwa ni watenda dhambi, wachafu na waliopotea. Kwa msingi huu, kanisa la Bwana haliwezi songa mbele. Kanisa lenu lina matatizo makubwa kuliko hao uliowataja kuwa ni tatizo.
Huu wako ni uongo wa kupindukia kama tu ule wa aliyeleta hapa andishi hili
 
Mkuu lini Mwizarubi ataondoka na familia yake kwenye Nyumba ya Kanisa pale Sayuni EAGT na kupisha mchungaji aishi hapo Kama yeye alivyoishi akiwa mchungaji? Au no Nyumba yake binafsi kwenye viwanja vya Kanisa? Maana mwaka was 19 huu anaishi hapo.
Nani mchungaji kiongozi wa Sayuni EAGT? Hebu tusaidie na wengine tujue!
 
Umeniboa ulipozungumzia kujengea makaburi. Sikutegemea kauli hiyo kutoka kwa mtu anayejinasibu kuwa ameokoka.
Kwa ujumla yaliyobaki yote uliyosema naona ni majungu tu. Kama wenzako wameshakuzidi ujanja huko, achana na biashara hiyo tafuta nyingine.
 
Inahitaji nguvu ya ziada kuyasema haya. Juzi nimepita maeneo fulani jiji la Mbeya nimekuta kanisa limeandikwa mjukuu wa Moses kulola. Ukweli nilifika zaidi ya mbali yaani jina la kulola linaanza kutumika kufanya utapeli hata na wanafamilia.

Simamieni hayo but ni maombi ya kufunga na kuomba tu ndiyo yanaweza kusambaratisha hao wahuni si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo maeneo ya Kiseke PPF jijini Mwanza, kuna kiubao kinaonyesha sehemu kuna Moses Kulola Day Care Centre...
 
Nani mchungaji kiongozi wa Sayuni EAGT? Hebu tusaidie na wengine tujue!
Huyo huyo Mwizarubi ndo Kila kitu. Hawa watu sijui wakoje. Wakichipukia wengine wanalazimishwa kuanzisha kwingine. Happy nadhani atabaki mwenyewe Hadi amfuate Kulola. Ubinafsi mwingi Sana.
 
Inahitaji nguvu ya ziada kuyasema haya. Juzi nimepita maeneo fulani jiji la Mbeya nimekuta kanisa limeandikwa mjukuu wa Moses kulola. Ukweli nilifika zaidi ya mbali yaani jina la kulola linaanza kutumika kufanya utapeli hata na wanafamilia.

Simamieni hayo but ni maombi ya kufunga na kuomba tu ndiyo yanaweza kusambaratisha hao wahuni si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika vizuri sana, japo sitataka kubishana na wewe kwenye sehemu ya hitimisho. Sijajua "wahuni" kwenye hitimisho lako ni akina nani. Andiko lililoletwa hapa kama post limekusudiwa kuibua hamasa ya hovyo kabisa ya kutumia miaka 5 tangu Askofu Kulola afariki kuonyesha kwamba kanisa aliloliacha limekuwa la hovyo, kwa maana ya kwamba viongozi waliopo madarakani sasa ni wa hovyo, jambo ambalo ni uongo wa wazi. Ni kweli, ndani ya kanisa la EAGT kuna wahuni ambao wanalitumia jina la Kulola kama maficho, na nina uhakika mwandishi wa "waraka huu naye ni mhuni anayetaka kutumia jina la Kulola kutekeleza uhuni."

Madai au tuhuma zilizoko kwenye andishi hilo zote hazina uthibitisho, na mbaya zaidi baadhi ya tuhuma zenyewe zimefikishwa mahakamani, halafu waliozipeleka mahakamani wakashindwa kuzithibitisha na mahakama ikazifutilia mbali. Nadhani sana wahuni hawa wameona wapeleke tuhuma hizo mitandaoni kwa kuwa wanajua kwamba huko ni wachache wanaoujua ukweli, lakini zaidi wahuni hawa wanajua kuwa viongozi wa kanisa wanaowatuhumu hawana muda wa kuja mitandaoni kujibizana nao!

Kwa takribani miaka miwili sasa, kanisa la EAGT liko katika mvutano wa kutengenezwa ambao msingi wake ni tamaa ya madaraka. Kwanza, aliyekuwa makamu wa askofu mkuu wa kanisa hilo alituhumiwa na baadaye akikiri kwenye vikao halali vya kanisa, kwamba alianguka katika dhambi iliyomwondolea sifa ya kuwa mchungaji na hivyo kuondolewa katika nafasi ya umakamu wa askofu na uchungaji wa kanisa la EAGT Bugando, jijini Mwanza. Ili kuwa wazi zaidi mchungaji huyo alianguka katika dhambi ya uzinzi, ambayo alikiri na akaeleza kuwa kwa mazingira aliyonayo ni ngumu kuepuka hiyo dhambi.

Awali, mzee huyo mwenye miaka zaidi ya 70 sasa, alikubaliana na uamuzi wa kanisa, lakini akaomba asaidiwe namna ya kuondoka kwenye kanisa la Bugando ili tukio hilo lisilete shida kwa washirika. Kikao kilichofikia maamuzi hayo kilifanyika Dodoma, hivyo waliteuliwa viongozi wawili wa kanisa ili waende huko Mwanza wakasaidie kuliweka vizuri kwa washirika jambo hilo.

Ni bahati mbaya kwamba, wakati mchungaji huyo akiwa tayari ameishafika Mwanza akapokea ushauri wa hovyo kabisa, na ambao kimsingi ndio unalitesa kanisa hilo sasa, wa kukataa kutekeleza kile ambacho kiliamriwa na yeye kukubaliana nacho kwenye kikao cha kanisa. Wale viongozi wawili waliokuwa wameteuliwa kwenda Mwanza kwa ajili ya kusimamia zoezi la mchungaji huyo kuachia uchungaji ili akabidhiwe mtumishi mwingine wakakwama kutekeleza zoezi hilo maana wakawa wameandaliwa "washirika wahuni" kuwapiga mawe.

Waliomshauri mchungaji huyo kubadilika ni kikundi cha wachungaji ambacho kimekuwa kikileta upinzani wa chini chini dhidi ya uongozi wa kanisa hilo ambao uliingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015 kupitia uchaguzi mkuu na kusimikwa Februari 2016. Upinzani unatokana na msimamo wa askofu mkuu mpya wa kanisa hilo kutangaza kuwa mwelekeo wake anataka kuona kanisa-kwa maana ya wachungaji na waumini wanaishi maisha ya utakatifu zaidi.

Ni muhimu kufahamu kwamba, EAGT kwa sasa ni taasisi kubwa mno, kwa maana ya kuwa na idadi kubwa ya makanisa na waumini, mali; nakadhalika. Kanisa sasa linamiliki jengo kubwa la gofofa tatu katika eneo la Darajani, barabara ya Nyerere, kanisa pia linamiliki shule ya sekondari Kahama,mkoani Shinyanga.

Wasioelewa ni kwamba, ndani ya kanisa la EAGT kumekuwepo na roho ya tamaa ya madaraka tangu muda mrefu, ni sawa tu kama ilivyo katika makanisa mengine pengine tofauti ni muda haujafika au na mfumo ndani ya makanisa . Hata huyo Kulola mwenyewe kabla hajafarikii mara kadhaa aliwahi kulalamikia sana roho hiyo ambayo baada ya kufariki imejidhihirisha zaidi.

Baada ya mchungaji huyo aliyefukuzwa kukaidi, aliungana na wachungaji wengine ambao ama huko nyuma waliwahi kushughulikiwa na kanisa kutokana na tuhuma kama hizo za kwake au wale wenye nia ya kuyageuza makanisa wanayoyachunga kuwa kama "ministry" [huduma] zao wajifanyie mambo kadri wanavyotaka, wakaanzisha vuguvugu la kupinga marekebisho ya Katiba ya kanisa hilo, ambayo yalitaka pamoja na mambo mengine, kuweka kipengele kinachoelekeza kwamba pale yanapotokea matatizo au kutoelewana kwa wachungaji ndani ya kanisa hilo uwepo utaratibu kwa suala husika kushughulikiwa ndani ya kanisa kwanza badala ya kulikimbiza moja kwa moja mahakanani. Kikundi hicho cha wachungaji kilipinga kipengele hicho, lakini kikashindwa baada ya wachungaji asilimia zaidi ya 90 kukubaliana na uwepo wa kipengele hicho ili kulinda ushuhuda wa kanisa.

Mkakati huo wa kupinga marekebisho ya Katiba, ulienda sanjari na mchungaji huyo aliyefukuzwa nafasi ya umakamu wa askofu mkuu kutumia vyombo vya habari kudai kuwa kuna magari 50 yameingizwa nchini kwa jina la kanisa-EAGT-lakini hayajulikani yapo wapi. Mchungaji huyo ambaye anajulikana kwa jina la John Mahene, kwa kutumia udhaifu wa vyombo vya habari alivyokuwa akivitumia, akawa anawatuhumu viongozi wakuu wa kanisa kuwa, wameingiza hayo magari ili kukwepa ushuru na kufanya biashara kujipatia fedha. Vyombo hivyo vya habari bila kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo vikawa vinaandika kwa namna ya kuwatuhumu vongozi wakuu wa kanisa, ambao nao waliamua kubaki kimya.

Mkakati huo ambao ulilenga kuwafanya wachungaji na waumini wa EAGT wajenge chuki dhidi ya viongozi wakuu wa kanisa, ulienda hatua nyingine kwa suala hilo kupelekwa mahakamani. Lilipelekwa mahakamani kupitia kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa kanisa hilo, marehemu Mchungaji John Mfuko aliyefariki dunia hivi karibuni. Hata hivyo, wakati fulani mchungaji Mfuko alipoulizwa mahakamani kama anafahamu shauri lililokuwa limefikishwa mahakamani alisema kuwa "suala lililoko mahakamani ni askofu mkuu kufukuza wachungaji."

Kuna simulizi ndefu sana kuhusiana na suala hili, lakini itoshe tu kusema kwamba, kulikuwa na hila na udanganyifu mkubwa katika kufikisha tuhuma za magari hayo mahakamani. Haikushangaza mahakama kulifutilia mbali shauri hilo kwa gharama na baadaye muda mfupi kabla ya kufikwa na mauti Mchungaji Mfuko kufanya toba kwa ajili ya jambo hilo. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya familia ambayo ilitolewa msibani.

Mwandishi wa waraka huu, wala wenzake waliomtuma [labda?] hawawezi kuthibitisha popote pale tuhuma wanazoeneza kwamba viongozi wa kanisa wameingiza magari kwa jina la EAGT na hayajulikani yalipo. Hawawezi!

Pili, waraka huo umempamba mchungaji Asumwisye Mwaisabila kuwa ni mtu mwema na anayestahili heshima. Iko hivi: Mwaisabila amekuwa msaidizi wa marehemu Kulola kwa muda mrefu. Alikuwa makamu wa askofu wa EAGT mpaka alipofariki Kulola ambapo alikaimu kama askofu mkuu kwa mujibu wa katiba. Amekaimu nafasi hiyo kwa takribani miaka miwili, lakini uchaguzi mkuu wa kupata askofu mkuu uliofanyika Septemba 2015 kura hazikutosha kabisa.

Nafasi ya makamu wa askofu katika EAGT ni "ceremonial post". Hufanyi chochote mpaka uagizwe na askofu mkuu. Kwa hiyo katika kipindi chote cha uongozi wa Kulola, Mwaisabila hakupata nafasi ya kuonyesha uwezo wa kiutendaji, hivyo miaka miwili aliyokaimu ilitumika kuonyesha uwezo wake. Wachungaji waliona na kumwelewa, hivyo hawakuona kama anastahili kuwa askofu mkuu wa kanisa la EAGT.

Ukiacha ukweli kwamba Mwaisabila hajamaliza hata darasa la saba, lakini ni miongoni mwa wachungaji wenye udhaifu mkubwa katika uongozi. Na ni uhakika kwamba pamoja na udhaifu mkubwa alionao katika uongozi, lakini mbaya zaidi ni mpenda madaraka kupita kiasi. Waliokuwepo Temeke wakati mwili wa askofu Kulola ukiagwa kabla ya kwenda kuzikwa jijini Mwanza, watakumbuka kauli aliyoitoa baada ya Askofu Zakaria Kakobe kutahadharisha wachungaji wa EAGT kuwa kifo cha Kulola kisifungue mlango wa mafarakano. Mwaisabila alitamka kuwa "mimi ndiye askofu mkuu, nimeachiwa kazi na waliokuwa wananidharau wakomee hapa hapa!"

Wakati wa uchaguzi mkuu wazee wenye heshima ndani ya kanisa walimshauri aondoe jina lake [kwa kuwa walijua atashindwa kwa aibu] lakini akagoma. Aliomba kuondoa jina kwenye duru la pili baada ya kuona wachungaji wamekosa imani naye na kumnyima kura. Tangu ashindwe Mwaisabila amekuwa na chuki ya wazi wazi dhidi ya uongozi ulioko madarakani. Aliamini kwa kuwa amekuwa msaidizi wa Kulola wa muda mrefu basi wachungaji wangemwamini.

Kikundi cha wachungaji kinachopinga viongozi wa juu, waliona udhaifu wake wa kupenda mno madaraka, hivyo wakamtangaza kuwa "askofu wao". Na sasa ndiye wanamtumia kuliumiza kanisa bila sababu za msingi. Leo ukimuuliza Mwaisabila sababu za kufanya uasi dhidi ya uongozi halali wa kanisa hawezi kukupa jibu la maana. Nimesoma mahojiano ya Katibu wa kanisa analochungaji Mwaisabila huko Mbeya, nimeiridhisha kukosa elimu na exposure kwa Mwaisabila, kumetumiwa vibaya na kikundi hicho cha wachungaji ambacho sasa kinamtumia kutesa kanisa na kuharibu image ya EAGT bila yeye kujua.

Kwenye waraka huo imeelezwa kwamba viongozi wa kanisa wamemtelekeza mjane wa askofu Kulola. Huu nao ni uongo wa mchana kweupe. Kwenye mkutano wa wachungaji uliofanyika Dodoma mwishoni mwa mwaka jana, katibu mkuu wa EAGT mchungaji Dk. Leonard Mwizarubi alilazimika kuzungumzia namna kanisa linavyomtunza bibi huyo. Na alifanya hivyo huku bibi Elizabeth Kulola akiwepo mkutanoni hapo. Tuliona na kusikia kauli ya bibi huyo. Ni jambo ambalo halihitaji maelezo mengi sana. Lakini kwa ufupi bibi huyo anapewa na kanisa posho kubwa ya shilingi milioni 5 kwa mwezi, analipiwa posho walinzi wawili shilingi laki 3 kwa mwezi, na analipiwa dereva ambaye ni mwanaye shilingi laki 5 kila mwezi.

Na yote hayo yanafanywa huku huyo bibi mwenyewe akiwa mara anaungana na wachungaji wanaopinga viongozi halali wa kanisa, mara anaungana nao tena kwa kuomba msamaha. Wachungaji wanaopinga uongozi halali wamekuwa wakimshawishi bibi huyo kuwa awe upande wao ili siku wakifanikiwa "kuupindua" uongozi halali watamboreshea maisha yake. Binafsi sitaki kuamini haraka kwamba kama viongozi wa kanisa wanampa posho hiyo watashindwaje kufanya service ya gari.

Ni ushauri wangu kwamba, badala ya kukimbilia mtandaoni kuchafua viongozi wa kanisa, mwandishi wa 'waraka ule' kama kweli anao ushahidi wa kwamba kuna magari 2500 yameingizwa nchini kwa jina la EAGT na hayajulikani yalipo, angewahi TRA maana kule atapata zawadi ya kufichua wakwepa kodi ambayo hutolewa bila usumbufu, maana hiki anachokifanya kitamchosha haraka sana kwa kuwa anajiongezea dhambi bure!

Mbarikiwe!
 
Huyo huyo Mwizarubi ndo Kila kitu. Hawa watu sijui wakoje. Wakichipukia wengine wanalazimishwa kuanzisha kwingine. Happy nadhani atabaki mwenyewe Hadi amfuate Kulola. Ubinafsi mwingi Sana.
Sasa kama Mwizarubi ndiye mchungaji kiongozi huo wito wa kwamba aondoke kwenye nyumba ya kanisa una lengo gani?
 
Umeniboa ulipozungumzia kujengea makaburi. Sikutegemea kauli hiyo kutoka kwa mtu anayejinasibu kuwa ameokoka.
Kwa ujumla yaliyobaki yote uliyosema naona ni majungu tu. Kama wenzako wameshakuzidi ujanja huko, achana na biashara hiyo tafuta nyingine.
Kwa hiyo waache kaburi lijae manyasi!
 
Walokole bwana!
Dhambi yenu kubwa ni uzinzi!
Ila mmejaa unafiki;dharau,ubaguzi,maringo,uongo na uzandiki!
Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom