Miaka 5 baada ya kifo cha mzee Moses Kulola: EAG(T) inaangamia

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,148
2,215
*WARAKA WA UAMSHO KWA WAUMINI WOTE WA KANISA LA EAGT TANZANIA*

Nawasalimu wote katika jina la Bwana wa majeshi Yesu Kristo. Ambalo kwa jina hilo, kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri ya kwamba *YESU NI BWANA*.

Neema na iwe kwenu nyote, na amani tele zitokazo kwa Mungu Baba yetu wa mbinguni, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Nikiwa mtumwa tu wa Bwana wetu Yesu Kristo, nachukua kalamu yangu ya shillingi mia mbili, namuomba Mungu anipe moyo mkuu ili niweze kuandika waraka huu kwenu ninyi waumini wenzangu wa kanisa la *EAGT*.

Kama mnavyokumbuka, leo ni tarehe 29/08/2018. Ni miaka mitano kamili sasa tokea baba yetu wa kiroho, na Askofu mkuu mwanzilishi wa kanisa letu la EAGT *Dr. Moses Samwel Kulola*, alipotwaliwa na Bwana kuishi naye huko juu mbinguni. Mtumishi huyu wa Mungu aliye hai, aliacha alama na ushuhuda wa kiwango cha juu katika kizazi hiki. Kama umewahi kusikia Roho wa Bwana yu juu ya mtu, hakika Roho Mtakatifu alitembea na kuonekana akitenda kazi katika huduma ya mzee wetu huyu. Si rahisi kusahaulika katika kizazi chetu na Taifa letu la Tanzania. Ni Zawadi Mungu alitupa kwa wakati wetu. Namkumbuka kwa mengi sana mzee wetu huyu aliyetangulia mbele ya haki. Naikumbuka injili yake isiyokuwa na chengachenga, uongozi wake, upendo wake, uvumilivu wake, na kwa mambo mengi sana ambayo kwayo, ni mfano wa kuigwa. Nakumbuka sana jinsi alivyoilinda na kuipigania imani mpaka pumzi yake ya mwisho.

Nakumbuka kuwaona watu wengi wakilia sana siku hiyo, wengine wakimshukuru Mungu na wengine wakibaki midomo wazi wasijue nini cha kusema au cha kufanya kwa wakati huo.

Katika ibada ya kuaga mwili wa mzee wetu huyu katika viwanja vya kanisa la EAGT Temeke, nashuhudia watu wengi wakiwa wamefurika kila pembe ya uwanja huo. Wachungaji, Maaskofu na viongozi wa dini mbalimbali walikusanyika katika kumuaga shujaa huyu wa injili hapa Tanzania. Hakika umati wa watu ni mwingi sana, na kila mgeni anayepita, lazima atauliza huyu mtu alikuwa nani!!?? Shuhuda zinazotolewa hapo, zinakuonyesha kuwa hakika Bishop Moses Kulola, alitembea na Mungu na alijitoa maisha yake yote kumtumikia katika kutumika shambani mwa Bwana. Hotuba mbalimbali zinatolewa na viongozi wa kadi mbalimbali, akiwemo mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa wakati huo alikuwa Dr. Mohamed Gharib Bilal. Ahadi nyingi na nzito zinatolewa na viongozi hawa. Kwanza kwa mjane wa marehemu bibi *Elizabeth Kulola*, familia nzima, na pia ahadi zinatolewa kwa kanisa la EAGT kuwa lisihofu na ya kuwa mambo yataendelea vizuri kama mzee alivyoacha.

Ndugu zangu na waumini wenzangu, nimeamua kuandika waraka huu kwenu ili kuwafahamisha kuwa mambo sivyo yalivyoahidiwa au kutegemea kuwa, tokea shujaa huyu wa injili Mzee wetu ninayemkumbuka leo, *Moses Kulola*, aitwe na Bwana. Baada ya kufariki mzee, kanisa letu lilipita vizuri katika kipindi cha mpito, ambacho mzee wetu Askofu mkuu msaidizi kwa kipindi hicho, Bishop Asumwisye Mwaisabila alikuwa kiongozi wa kanisa. Mungu ambariki sana Askofu Mstaafu Mwaisabila. Hekima yake na ukomavu wake katika uongozi ambao Bwana amemjaalia, ulitupitisha salama katika kipindi hicho cha mpito kiasi kwamba tukaona mambo yote ni shwari na hakika mzee wetu *Moses Kulola*, aliacha watu. Atakayemdharau Mzee Mwaisabila, hana Mungu ndani yake. Na anatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

Matatizo yalianza baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Uongozi huu ukiongozwa na Brown Mwakipesile, Mwizarubi, PrayGod Mgonja n.k, umeleta shida kubwa sana, fedheha na aibu kubwa. Si kwa kanisa la EAGT tu lililofedheheshwa, bali mwili wa Kristo Tanzania umejeruhiwa.

Waumini wenzangu, kama mnayakumbuka maneno ya Bwana Yesu ya
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”, basi maneno hayo yamedhihirika katika uongozi huu unaoongozwa na Mwakipesile pamoja na Mwizarubi.

Tokea Mwakipesile na wenzake wachukue uongozi wa kanisa, huduma ya EAGT imerudi nyuma badala ya kusonga mbele. Waumini mmekuwa mkiambiwa kila siku kuwa kila kitu kiko sawa, sasa naomba niwafumbue macho kuwa hali sio shwari kabisa. Na hili kanisa linaweza kufutwa wakati wowote ule kama juhudi za kulinusuru kanisa hazitafanyika. Tuingie kwenye maombi makali ya kumuomba Mungu aepushie mbali jambo hili lisitokee katika macho yetu. Kanisa letu la EAGT limekuwa na wizi mkubwa sana wa mali na fedha za kanisa. Chini ya uongozi wa Mwakipesile na kundi lake, kanisa limekuwa likijihusisha na biashara ya uingizaji wa mali yakiwemo magari ambayo hayapo kanisani. Neema ya kanisa letu la EAGT ya kupata msamaha wa kodi toka serikalini, imekuwa ikitumiwa vibaya na uongozi huu wa Mwakipesile, Mwizarubi pamoja na kamati yake yote, maaskofu wa kanda, na rafiki zao na watu wao wa karibu kama Alex Simbila na wengineo. Ninasikitika kuwajulisha waumini wenzangu kuwa, baada ya jumuiya ya Waislamu ya BAKWATA kuingiza magari mengi nchini, linalofuata ni kanisa letu la EAGT. Taarifa zipo, na taarifa hizi zimefichwa sana ili watu msijue. Hamshangai kila mara tunaambiwa makanisani hali ni shwari??

EAGT kwa kipindi kifupi imeingiza magari zaidi ya 2500(elfu mbili na mia tano), na yote yamefanyiwa biashara na kundi hili ovu la viongozi. Yoyote anayejaribu kuhoji haya yote amekuwa ni adui mkubwa na amekuwa akipigwa vita sana. Wote ambao wamejitokeza hadharani kupinga ufisadi huu wa kihistoria ndani ya EAGT chini ya Mwakipesile, kama ni mchungaji amekuwa akitishwa kuwekwa ndani,(baadhi yao wameswekwa rumande hata wiki iliyopita huko Ukerewe, Mwanza kuna mchungaji aliwekwa ndani na kina Mwakipesile na kundi lake). Kama wewe ni muumini, mchungaji wako na wazee wa kanisa watapewa maelekezo ya kukufukuza kanisani kwa visingizio na visa mbalimbali.

Makao makuu ya kanisa yamewekwa rehani. Jengo ambalo kanisa inamiliki, inasemekana limeshauzwa kinyemela kwa mfanyabishara kutoka kanda ya ziwa anayejulikana kwa jina Jumanne Kishimba. Mkataba kati ya Kishimba na EAGT haueleweki eleweki, huku Kishimba akitamba kuwa ameshamilikishwa mali. Ushahidi wa mambo haya yote upo, lakini waumini wenzangu tumefichwa kwa vitisho vikali sana. Mambo ni mengi sana, sijaongelea katiba feki iliyotengenezwa na Mwakipesile na Mwizarubi na Mgonja ili iweze kuwapa nafasi ya kulitafuna kanisa kama wanavyotaka, kesi zilizoko mahakamani ni nyingi, Wachungaji kupelekana Polisi ni mara kwa mara. Kina Mwakipesile na kundi lake wameshahojiwa polisi, na kuna ushahidi wa dhahiri, hawa watu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa kila mahali. Haya yote yamekuwa yakifanikiwa chini ya udhamini wa mchungaji wa *Temeke EAGT, mchungaji Christomore Ngowi, ambaye ni mdhamini.* Mchungaji huyu amekuwa hatulii kanisani kwake, amekuwa akizunguka kila mahali Tanzania nzima kuhakikisha anazima hili sakata la wizi mzito ambao ameshirikiana na kina Mwakipesile. Amekuwa mwiba mkubwa kwa haki na maendeleo ya kanisa. Mchungaji Ngowi wa EAGT Temeke amesikika akiapa kuwa kamwe hatajitenga na kundi hili la waovu. Ukiona hivyo, lazima anafaidika sana na ubadhirifu huu. Wamekuwa wakinunua vyombo vya habari ili kuandika habari zilizopotoshwa, kwa lengo kubwa la kutuhadaa sisi waumini. Kwa mfano gazeti la MWANZO. Nawashauri msinunue gazeti hili. Kununua gazeti hili ni kufanikisha malengo ya kishetani.

Nashawishika kwa asilimia mia moja kuwa, watumishi wa Mungu wamebaki wachache. Nawakumbuka wazee wetu waliotutangulia katika imani na walioacha alama ya utumishi uliotukuka. Walikuwepo kwa uchache wao kina Calist Masalu, Mzee Mwamwenda, Mzee John Mfuko na wengine wengi sana. Hawakutaka mali za dunia hii, kila kilichopatikana kilifanya kazi ya Mungu kwa uamunifu wa hali ya juu. Je, tumekosea wapi? Nani atatuvusha hapa?

Tunapokumbuka siku hii ambayo shujaa wa injili alitwaliwa na Bwana miaka mitano iliyopita. Waumini wote kwa ujumla wetu, tuikumbuke familia ya Askofu Moses Kulola katika maombi. Kundi la Mwakipesile na wenzake wanataka kuiangamiza hii familia. Mama mjane wa mzee wetu Moses Kulola hana heshima tena kama aliyokuwa nayo zamani. Je hii si laana? Hawajui anakula nini, wala hawajui ameamkaje au anaishi vipi. Mama huyu pamoja na Mzee walizunguka nchi nzima kwa miaka mingi wakiihubiri injili. Maisha yao yote waliyatoa kwa Bwana. Wengi wetu ni mashahidi. Leo huyu mama hana hata bajaji ya kutembelea au hata anapotaka kwenda kwenye kanisa la karibu kwa ajili ya ibada, amekuwa akitembea kwa miguu au kuomba omba msaada wa usafiri. Amekuwa omba omba mama yetu. Tokea gari lake aliloachiwa na mzee kuharibika, viongozi wakuu wa kanisa wamegoma kutoa pesa za matengenezo. Leo miaka mitano tokea kifo cha mzee, hata kaburi la aliyekuwa askofu mkuu wetu ni aibu tupu. Wameshindwa hata kulijenga. Mama Kulola alijichanga changa kuliweka katika hali nzuri, lakini viongozi wameshindwa kumsapoti. Ninapoyaona haya, nakumbuka maneno mzee wetu alikuwa akipenda kuyasema. “Je, mwana wa adamu akirudi, ataikuta ile imani?”

Mwisho, ninawaomba waumini wenzangu popote tulipo, tumlilie Mungu kwa ajili ya kanisa la Bwana. Tupaze sauti zetu mbele za Mungu, ili kundi hili ovu la hawa viongozi kina Mwakipesile, Mwizarubi, Mgonja na wengineo, bila kumsahau mdhamini aliyekimbilia mihuri ya kanisa baada ya mzee Mfuko kuitwa na Bwana, Christomore Ngowi, Bwana wa majeshi akashughulike nao. Mchungaji Ngowi amesahau kuwa anachofanya ni uvunjifu wa sheria, huku yeye mwenyewe akiwa ni mstaafu wa jeshi la polisi Tanzania. Sambaza ujumbe huu kwa kila muumini ili ajue yanayofanyika kanisani. Tuungane kuwakataa hawa waovu wanaojifanya kondoo kumbe ni mbwa mwitu. Kama Bwana alishughulika na Farao aliyekuwa na moyo mgumu kama jiwe, hatashindwa kushughulika na hawa wanyang’anyi na wapenda madaraka waliojivalisha majina ya uaskofu. Kuna baadhi ya washirika wenzetu hasa wachanga katika imani baada ya kusikia uovu huu wameamua kurudi nyuma, na wengine kurudi kwenye dini zao za zamani. Maana hawaoni tena thamani ya wokovu kwa vile kama wale waliopaswa kuonyesha njia, ndio wanaoongoza kwa uovu wa hali ya juu namna hii.

Na hawa maaskofu watakapojitokeza na kukana hili andiko, nitasambaza vielelezo vyote kwenu waumini wenzangu.

Kifupi, tunaongozwa na kundi lililojawa na roho chafu. Wote kwa pamoja tuombe kuwaangamiza hawa watu na nia zao mbovu. Neno la Mungu aliye hai likapate kusimama.

Tunapokumbuka siku hii ya tarehe 29/08, tuliombee kanisa la Bwana linaloelekea kuzama baharini, kila mmoja wetu ajiulize, amefanya nini au atafanya nini kuzuia huu uovu? Kalamu yangu ya shilingi mia mbili inaelekea kuisha wino. Nimeandika mengi kidogo na poleni sana kwa kuwachosha. Yapo mengi zaidi ya hayo niliyoyataja. Tuanze na haya kwa leo. Kumbuka, Mungu hakutupa roho ya woga. Tuamke toke usingizini, tuwahoji hawa viongozi wetu wanaotupeleka kubaya.

Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Pendo la Mungu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Tudumu katika kukesha na maombi. *Bwana yu karibu.*

Mshirika mwamunifu wa EAGT.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mtumishi wa Mungu Moses Kolola (R.I.P) nilihudhuria mkutano wake wa injili 1993 Monduli,Alikuwa na upako wa ajabu.
Hayo mengine jadilianeni mpate suluhu huko nakanisani kwenu.Huku umekuja mbali,Mungu anakuona.
 
Kanisa lenu limeshafitinika tangu huku chini. Kila mahala unapopita kuna vikanisa vidogo vidogo vyenye waumini wasiozidi kumi. Kanisa likikua kidogo, pepo wa mafarakano anaingia na kanisa linagawanyika. Ni nadra sana kukuta usharika wa EAGT wenye waumini mia.
Kwa hali hii, kanisa lenu haliwezi kusimama imara kwa kuwa kila mmoja yuko after personal interest.
Kila muumini ana njaa ya kufungua usharika ili aweze kukinga sadaka. Nia ya kumtumikia Kristo imepotea kila mtu yuko after personal grolification ya kuabudiwa na waumini.
Pepo la kubagua makanisa mengine ndio limeshawajaaa mwili mzima. Nyie mnapenda kujiona ni watakatifu na Wakristo wengine mnawaona kuwa ni watenda dhambi, wachafu na waliopotea. Kwa msingi huu, kanisa la Bwana haliwezi songa mbele. Kanisa lenu lina matatizo makubwa kuliko hao uliowataja kuwa ni tatizo.
 
Mimi mambo ya dini hapana, Yesu anasema tujifunze kwake,. Na Yesu hakuwa na dini na wala sio mkristo.. Yesu ni Mwana wa Mungu na ni Mungu kamili bali hakuanzisha ukristo..
Ndomaana unamkuta mkristo anaitwa John,au Michael,ila ni mtenda dhambi wa kawaida tu..
Mwana wa Mungu hatendi dhambi kamwe,ila wakristo wengi tu mtaani ni walevi wazinzi,na wachafu wa kila Aina,. Ila mwana wa Mungu hatendi dhambi kamwe..
I'm a child of God..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*WARAKA WA UAMSHO KWA WAUMINI WOTE WA KANISA LA EAGT TANZANIA*

Nawasalimu wote katika jina la Bwana wa majeshi Yesu Kristo. Ambalo kwa jina hilo, kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri ya kwamba *YESU NI BWANA*.

Neema na iwe kwenu nyote, na amani tele zitokazo kwa Mungu Baba yetu wa mbinguni, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Nikiwa mtumwa tu wa Bwana wetu Yesu Kristo, nachukua kalamu yangu ya shillingi mia mbili, namuomba Mungu anipe moyo mkuu ili niweze kuandika waraka huu kwenu ninyi waumini wenzangu wa kanisa la *EAGT*.

Kama mnavyokumbuka, leo ni tarehe 29/08/2018. Ni miaka mitano kamili sasa tokea baba yetu wa kiroho, na Askofu mkuu mwanzilishi wa kanisa letu la EAGT *Dr. Moses Samwel Kulola*, alipotwaliwa na Bwana kuishi naye huko juu mbinguni. Mtumishi huyu wa Mungu aliye hai, aliacha alama na ushuhuda wa kiwango cha juu katika kizazi hiki. Kama umewahi kusikia Roho wa Bwana yu juu ya mtu, hakika Roho Mtakatifu alitembea na kuonekana akitenda kazi katika huduma ya mzee wetu huyu. Si rahisi kusahaulika katika kizazi chetu na Taifa letu la Tanzania. Ni Zawadi Mungu alitupa kwa wakati wetu. Namkumbuka kwa mengi sana mzee wetu huyu aliyetangulia mbele ya haki. Naikumbuka injili yake isiyokuwa na chengachenga, uongozi wake, upendo wake, uvumilivu wake, na kwa mambo mengi sana ambayo kwayo, ni mfano wa kuigwa. Nakumbuka sana jinsi alivyoilinda na kuipigania imani mpaka pumzi yake ya mwisho.

Nakumbuka kuwaona watu wengi wakilia sana siku hiyo, wengine wakimshukuru Mungu na wengine wakibaki midomo wazi wasijue nini cha kusema au cha kufanya kwa wakati huo.

Katika ibada ya kuaga mwili wa mzee wetu huyu katika viwanja vya kanisa la EAGT Temeke, nashuhudia watu wengi wakiwa wamefurika kila pembe ya uwanja huo. Wachungaji, Maaskofu na viongozi wa dini mbalimbali walikusanyika katika kumuaga shujaa huyu wa injili hapa Tanzania. Hakika umati wa watu ni mwingi sana, na kila mgeni anayepita, lazima atauliza huyu mtu alikuwa nani!!?? Shuhuda zinazotolewa hapo, zinakuonyesha kuwa hakika Bishop Moses Kulola, alitembea na Mungu na alijitoa maisha yake yote kumtumikia katika kutumika shambani mwa Bwana. Hotuba mbalimbali zinatolewa na viongozi wa kadi mbalimbali, akiwemo mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa wakati huo alikuwa Dr. Mohamed Gharib Bilal. Ahadi nyingi na nzito zinatolewa na viongozi hawa. Kwanza kwa mjane wa marehemu bibi *Elizabeth Kulola*, familia nzima, na pia ahadi zinatolewa kwa kanisa la EAGT kuwa lisihofu na ya kuwa mambo yataendelea vizuri kama mzee alivyoacha.

Ndugu zangu na waumini wenzangu, nimeamua kuandika waraka huu kwenu ili kuwafahamisha kuwa mambo sivyo yalivyoahidiwa au kutegemea kuwa, tokea shujaa huyu wa injili Mzee wetu ninayemkumbuka leo, *Moses Kulola*, aitwe na Bwana. Baada ya kufariki mzee, kanisa letu lilipita vizuri katika kipindi cha mpito, ambacho mzee wetu Askofu mkuu msaidizi kwa kipindi hicho, Bishop Asumwisye Mwaisabila alikuwa kiongozi wa kanisa. Mungu ambariki sana Askofu Mstaafu Mwaisabila. Hekima yake na ukomavu wake katika uongozi ambao Bwana amemjaalia, ulitupitisha salama katika kipindi hicho cha mpito kiasi kwamba tukaona mambo yote ni shwari na hakika mzee wetu *Moses Kulola*, aliacha watu. Atakayemdharau Mzee Mwaisabila, hana Mungu ndani yake. Na anatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

Matatizo yalianza baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Uongozi huu ukiongozwa na Brown Mwakipesile, Mwizarubi, PrayGod Mgonja n.k, umeleta shida kubwa sana, fedheha na aibu kubwa. Si kwa kanisa la EAGT tu lililofedheheshwa, bali mwili wa Kristo Tanzania umejeruhiwa.

Waumini wenzangu, kama mnayakumbuka maneno ya Bwana Yesu ya
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”, basi maneno hayo yamedhihirika katika uongozi huu unaoongozwa na Mwakipesile pamoja na Mwizarubi.

Tokea Mwakipesile na wenzake wachukue uongozi wa kanisa, huduma ya EAGT imerudi nyuma badala ya kusonga mbele. Waumini mmekuwa mkiambiwa kila siku kuwa kila kitu kiko sawa, sasa naomba niwafumbue macho kuwa hali sio shwari kabisa. Na hili kanisa linaweza kufutwa wakati wowote ule kama juhudi za kulinusuru kanisa hazitafanyika. Tuingie kwenye maombi makali ya kumuomba Mungu aepushie mbali jambo hili lisitokee katika macho yetu. Kanisa letu la EAGT limekuwa na wizi mkubwa sana wa mali na fedha za kanisa. Chini ya uongozi wa Mwakipesile na kundi lake, kanisa limekuwa likijihusisha na biashara ya uingizaji wa mali yakiwemo magari ambayo hayapo kanisani. Neema ya kanisa letu la EAGT ya kupata msamaha wa kodi toka serikalini, imekuwa ikitumiwa vibaya na uongozi huu wa Mwakipesile, Mwizarubi pamoja na kamati yake yote, maaskofu wa kanda, na rafiki zao na watu wao wa karibu kama Alex Simbila na wengineo. Ninasikitika kuwajulisha waumini wenzangu kuwa, baada ya jumuiya ya Waislamu ya BAKWATA kuingiza magari mengi nchini, linalofuata ni kanisa letu la EAGT. Taarifa zipo, na taarifa hizi zimefichwa sana ili watu msijue. Hamshangai kila mara tunaambiwa makanisani hali ni shwari??

EAGT kwa kipindi kifupi imeingiza magari zaidi ya 2500(elfu mbili na mia tano), na yote yamefanyiwa biashara na kundi hili ovu la viongozi. Yoyote anayejaribu kuhoji haya yote amekuwa ni adui mkubwa na amekuwa akipigwa vita sana. Wote ambao wamejitokeza hadharani kupinga ufisadi huu wa kihistoria ndani ya EAGT chini ya Mwakipesile, kama ni mchungaji amekuwa akitishwa kuwekwa ndani,(baadhi yao wameswekwa rumande hata wiki iliyopita huko Ukerewe, Mwanza kuna mchungaji aliwekwa ndani na kina Mwakipesile na kundi lake). Kama wewe ni muumini, mchungaji wako na wazee wa kanisa watapewa maelekezo ya kukufukuza kanisani kwa visingizio na visa mbalimbali.

Makao makuu ya kanisa yamewekwa rehani. Jengo ambalo kanisa inamiliki, inasemekana limeshauzwa kinyemela kwa mfanyabishara kutoka kanda ya ziwa anayejulikana kwa jina Jumanne Kishimba. Mkataba kati ya Kishimba na EAGT haueleweki eleweki, huku Kishimba akitamba kuwa ameshamilikishwa mali. Ushahidi wa mambo haya yote upo, lakini waumini wenzangu tumefichwa kwa vitisho vikali sana. Mambo ni mengi sana, sijaongelea katiba feki iliyotengenezwa na Mwakipesile na Mwizarubi na Mgonja ili iweze kuwapa nafasi ya kulitafuna kanisa kama wanavyotaka, kesi zilizoko mahakamani ni nyingi, Wachungaji kupelekana Polisi ni mara kwa mara. Kina Mwakipesile na kundi lake wameshahojiwa polisi, na kuna ushahidi wa dhahiri, hawa watu wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa kila mahali. Haya yote yamekuwa yakifanikiwa chini ya udhamini wa mchungaji wa *Temeke EAGT, mchungaji Christomore Ngowi, ambaye ni mdhamini.* Mchungaji huyu amekuwa hatulii kanisani kwake, amekuwa akizunguka kila mahali Tanzania nzima kuhakikisha anazima hili sakata la wizi mzito ambao ameshirikiana na kina Mwakipesile. Amekuwa mwiba mkubwa kwa haki na maendeleo ya kanisa. Mchungaji Ngowi wa EAGT Temeke amesikika akiapa kuwa kamwe hatajitenga na kundi hili la waovu. Ukiona hivyo, lazima anafaidika sana na ubadhirifu huu. Wamekuwa wakinunua vyombo vya habari ili kuandika habari zilizopotoshwa, kwa lengo kubwa la kutuhadaa sisi waumini. Kwa mfano gazeti la MWANZO. Nawashauri msinunue gazeti hili. Kununua gazeti hili ni kufanikisha malengo ya kishetani.

Nashawishika kwa asilimia mia moja kuwa, watumishi wa Mungu wamebaki wachache. Nawakumbuka wazee wetu waliotutangulia katika imani na walioacha alama ya utumishi uliotukuka. Walikuwepo kwa uchache wao kina Calist Masalu, Mzee Mwamwenda, Mzee John Mfuko na wengine wengi sana. Hawakutaka mali za dunia hii, kila kilichopatikana kilifanya kazi ya Mungu kwa uamunifu wa hali ya juu. Je, tumekosea wapi? Nani atatuvusha hapa?

Tunapokumbuka siku hii ambayo shujaa wa injili alitwaliwa na Bwana miaka mitano iliyopita. Waumini wote kwa ujumla wetu, tuikumbuke familia ya Askofu Moses Kulola katika maombi. Kundi la Mwakipesile na wenzake wanataka kuiangamiza hii familia. Mama mjane wa mzee wetu Moses Kulola hana heshima tena kama aliyokuwa nayo zamani. Je hii si laana? Hawajui anakula nini, wala hawajui ameamkaje au anaishi vipi. Mama huyu pamoja na Mzee walizunguka nchi nzima kwa miaka mingi wakiihubiri injili. Maisha yao yote waliyatoa kwa Bwana. Wengi wetu ni mashahidi. Leo huyu mama hana hata bajaji ya kutembelea au hata anapotaka kwenda kwenye kanisa la karibu kwa ajili ya ibada, amekuwa akitembea kwa miguu au kuomba omba msaada wa usafiri. Amekuwa omba omba mama yetu. Tokea gari lake aliloachiwa na mzee kuharibika, viongozi wakuu wa kanisa wamegoma kutoa pesa za matengenezo. Leo miaka mitano tokea kifo cha mzee, hata kaburi la aliyekuwa askofu mkuu wetu ni aibu tupu. Wameshindwa hata kulijenga. Mama Kulola alijichanga changa kuliweka katika hali nzuri, lakini viongozi wameshindwa kumsapoti. Ninapoyaona haya, nakumbuka maneno mzee wetu alikuwa akipenda kuyasema. “Je, mwana wa adamu akirudi, ataikuta ile imani?”

Mwisho, ninawaomba waumini wenzangu popote tulipo, tumlilie Mungu kwa ajili ya kanisa la Bwana. Tupaze sauti zetu mbele za Mungu, ili kundi hili ovu la hawa viongozi kina Mwakipesile, Mwizarubi, Mgonja na wengineo, bila kumsahau mdhamini aliyekimbilia mihuri ya kanisa baada ya mzee Mfuko kuitwa na Bwana, Christomore Ngowi, Bwana wa majeshi akashughulike nao. Mchungaji Ngowi amesahau kuwa anachofanya ni uvunjifu wa sheria, huku yeye mwenyewe akiwa ni mstaafu wa jeshi la polisi Tanzania. Sambaza ujumbe huu kwa kila muumini ili ajue yanayofanyika kanisani. Tuungane kuwakataa hawa waovu wanaojifanya kondoo kumbe ni mbwa mwitu. Kama Bwana alishughulika na Farao aliyekuwa na moyo mgumu kama jiwe, hatashindwa kushughulika na hawa wanyang’anyi na wapenda madaraka waliojivalisha majina ya uaskofu. Kuna baadhi ya washirika wenzetu hasa wachanga katika imani baada ya kusikia uovu huu wameamua kurudi nyuma, na wengine kurudi kwenye dini zao za zamani. Maana hawaoni tena thamani ya wokovu kwa vile kama wale waliopaswa kuonyesha njia, ndio wanaoongoza kwa uovu wa hali ya juu namna hii.

Na hawa maaskofu watakapojitokeza na kukana hili andiko, nitasambaza vielelezo vyote kwenu waumini wenzangu.

Kifupi, tunaongozwa na kundi lililojawa na roho chafu. Wote kwa pamoja tuombe kuwaangamiza hawa watu na nia zao mbovu. Neno la Mungu aliye hai likapate kusimama.

Tunapokumbuka siku hii ya tarehe 29/08, tuliombee kanisa la Bwana linaloelekea kuzama baharini, kila mmoja wetu ajiulize, amefanya nini au atafanya nini kuzuia huu uovu? Kalamu yangu ya shilingi mia mbili inaelekea kuisha wino. Nimeandika mengi kidogo na poleni sana kwa kuwachosha. Yapo mengi zaidi ya hayo niliyoyataja. Tuanze na haya kwa leo. Kumbuka, Mungu hakutupa roho ya woga. Tuamke toke usingizini, tuwahoji hawa viongozi wetu wanaotupeleka kubaya.

Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Pendo la Mungu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. Tudumu katika kukesha na maombi. *Bwana yu karibu.*

Mshirika mwamunifu wa EAGT.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukitazama anayofanya mwanadamu huwezi songa mbele katika imani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutathibitisha vipi hayo ni ya kweli?
Je wewe siyo miongoni mwa waliokosa nafasi za uongozi baada ya mzee?
unasema tuwaombee waangamizwe? We ni mtu wa kiroho kweli! badala ya kuomba rehema unataka waangamie?
kwenye mtandao utapa suluhu?
Unachafua kanisa kwenye mitandao kwa maslahi binafsi?
avatar yenyewe inatia maisha kama kweli umeokoka.
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom