Miaka 45 ya upelelezi

Miaka 45 ya upelelezi

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,423
Reaction score
8,653
Miaka 45 ya upelelezi Part [1]

Kwa wale wapenzi watazamaji wa tamthilia ya Prison Break watakuwa wanakumbuka katika msimu wa kwanza wa tamthilia kipindi muhusika mkuu wa tamthilia, Michael Scofield, akijaribu kuwashawishi wafungwa kadhaa aliowachagua wamuunge mkono kwenye mpango wake kabambe wa kutoroka kutoka katika gereza la Fox River.

Prison_Break_S3intro.jpg

Basi, kulikuwa na mzee wa makamo aliyeitwa, Charles Westmoreland ambaye alimpa changamoto kubwa kumkubalia kujiunga na mpango huu. Watu ambao Micheal aliwachagua, kila mmoja alimteua kwa sababu maalumu kutokana na umuhimu fulani alionao ambao utahitajika katika kufanikisha tukio la kutoroka.

Mathalani alimchagua Cellmate wake, Fernando Sucre, ili aje kuwasaidia katika mpango wa kuingia nchi ya Mexico kiurahisi baada ya kutoroka. Alimchagua John Abruzzi ili aje kusaidia kupata usafiri wa ndege watokomee pindi tu wakitoroka Fox River, na wengineo wote waliojumuishwa kwenye mpango huo walikuwa na umuhimu maalumu.
.

Kujumuishwa kwa Charles Westmoreland kwenye mpango huo ni kutokana na Michael kung'amua mapema kwamba watahitaji fedha za kujikimu mara tu wakifanikiwa kutoroka na hatimaye kuingia nchini Mexico.

_Prison_Break_.jpg

Swali ni je, fedha wanapata wapi? Ndipo hapo anapoingia Charles Westmoreland, ambaye licha ya kutumia jina hili la Charles Westmoreland, Michael Scofield aliamini kuwa huyu mzee ni jambazi (D.B Cooper) aliyefanikiwa kuiteka ndege na serikali kukubali kulipa dola milioni moja ili aiachie; jambazi ambaye mpaka muda huo alikuwa bado anatafutwa na shirika la ujasusi la FBI.

jambazi pekee aliyefanikiwa kuweka historia katika nchi ya Marekani kufanya tukio la utekaji ndege kwa mafanikio na kesi kushindwa kutatuliwa na FBI kwa takribani miaka 45! Licha ya Charles Westmoreland kukataa katakata kuwa yeye siye D.B Cooper lakini Michael aliamini yeye ndiye na fedha alizofanikiwa kulipwa na serikali bado hajazitumia, ziko mahali fulani amezificha.

yerickonyerere___Bged6rOHttU___.jpg

. Baada ya majaribio kadhaa ya kumshawishi kushindikana, mwishoni kabisa Charles anakubali kuungana katika mpango wa kutoroka baada ya kugundua kuwa hatopewa fursa ya kumuona binti yake aliyekuwa anaumwa na ana karibia kufa. Na kuthibitisha hilo anamuonesha Michael noti ya fedha...... Itaendelea Part 2
 
Inaonekana story yako ni tamu kwa jinsi ulivyoianza, au labda kwakuwa nilikuwa teja wa Prison Break!!! Naomba ikiendelea unitag.
 
Miaka 45 ya upelelezi Part [1]

Kwa wale wapenzi watazamaji wa tamthilia ya Prison Break watakuwa wanakumbuka katika msimu wa kwanza wa tamthilia kipindi muhusika mkuu wa tamthilia, Michael Scofield, akijaribu kuwashawishi wafungwa kadhaa aliowachagua wamuunge mkono kwenye mpango wake kabambe wa kutoroka kutoka katika gereza la Fox River.

View attachment 719769

Basi, kulikuwa na mzee wa makamo aliyeitwa, Charles Westmoreland ambaye alimpa changamoto kubwa kumkubalia kujiunga na mpango huu. Watu ambao Micheal aliwachagua, kila mmoja alimteua kwa sababu maalumu kutokana na umuhimu fulani alionao ambao utahitajika katika kufanikisha tukio la kutoroka.

Mathalani alimchagua Cellmate wake, Fernando Sucre, ili aje kuwasaidia katika mpango wa kuingia nchi ya Mexico kiurahisi baada ya kutoroka. Alimchagua John Abruzzi ili aje kusaidia kupata usafiri wa ndege watokomee pindi tu wakitoroka Fox River, na wengineo wote waliojumuishwa kwenye mpango huo walikuwa na umuhimu maalumu.
.

Kujumuishwa kwa Charles Westmoreland kwenye mpango huo ni kutokana na Michael kung'amua mapema kwamba watahitaji fedha za kujikimu mara tu wakifanikiwa kutoroka na hatimaye kuingia nchini Mexico.

View attachment 719770

Swali ni je, fedha wanapata wapi? Ndipo hapo anapoingia Charles Westmoreland, ambaye licha ya kutumia jina hili la Charles Westmoreland, Michael Scofield aliamini kuwa huyu mzee ni jambazi (D.B Cooper) aliyefanikiwa kuiteka ndege na serikali kukubali kulipa dola milioni moja ili aiachie; jambazi ambaye mpaka muda huo alikuwa bado anatafutwa na shirika la ujasusi la FBI.

jambazi pekee aliyefanikiwa kuweka historia katika nchi ya Marekani kufanya tukio la utekaji ndege kwa mafanikio na kesi kushindwa kutatuliwa na FBI kwa takribani miaka 45! Licha ya Charles Westmoreland kukataa katakata kuwa yeye siye D.B Cooper lakini Michael aliamini yeye ndiye na fedha alizofanikiwa kulipwa na serikali bado hajazitumia, ziko mahali fulani amezificha.

View attachment 719772

. Baada ya majaribio kadhaa ya kumshawishi kushindikana, mwishoni kabisa Charles anakubali kuungana katika mpango wa kutoroka baada ya kugundua kuwa hatopewa fursa ya kumuona binti yake aliyekuwa anaumwa na ana karibia kufa. Na kuthibitisha hilo anamuonesha Michael noti ya fedha...... Itaendelea Part 2
USISAHAU KUNITAG(herufi kubwa kuonesha msisitizo)!
 
Copied and pasted from Yerico Nyerere, muwe mnatoka acknowledgements bas kwa original authors
 
haaaaaahaaaa hii story ilianzia hapa... kutoka kwa habib. A. Anga then yerico nyerere akai copy
 
Back
Top Bottom