Miaka 32 ya CCM - Upinzani wa Kweli "utatoka" CCM!

Miaka 32 ya CCM - Upinzani wa Kweli "utatoka" CCM!

Kwa mazingira ya nchi zetu za kiafrika (bila ya kuiondoa Tanzania) hali zetu za kimaisha zinafanana kwa maana hali za kiuchumi ni zilezile za nchi zinazoendelea.

Unataka sema kama hali zetu ni sawa na nchi zingine zinazoendelea basi ndio kipimo kuwa hakuna kasoro za uongozi wa CCM. Namibia, Botswana tuko sawa?


CCM ina kazi ya kuhakikisha inatimiza ilani yake uchaguzi ambayo ndiyo mkataba wa ajira yake kati yake na wananchi. Imekuwa ikifanya hivyo kwa wakati wote licha ya kukabiliwa na hali ngumu za kiuchumi zinazosababishwana mambo ambayo yako nje ya uwezo wake. Kwa mfano hali ngumu ya kiuchumi duniani hili liko nje ya uwezo wa CCM.
Hali ngumu ya uchumi duniani ilianza lini?, unataka kusema huu mtikisiko wa kiuchumi una miaka 32?.

Lakini pia wakati wakutekeleza majukumu yake makubwa ya kuendesha serikali inakumbana na matatizo ambayo kwa hakika inajitahidi kuyaweka sawa kwa manufaa ya nchi na wala siyo CCM. Kwa mfano, kitendo cha kupambana na rushwa, hatua ambazo zimechukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa hatuna budi kuipongeza serikali ili ipate nguvu zaidi ya kuongeza mapambano dhidi ya rushwa. Hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama ambao utawawezesha wananchi walau waweze kuamka na kufanya shughuli zao za kila siku bila ya bugdha.
Kuimarisha mapambano dhidi ya vifo vya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano.Kupunguza vifo vya akina mama wajawazito.Kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto wetu nk.Kazi hii ya CCM si kazi ndogo, ni kazi kubwa kabisa ambayo inafanyika kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi.


Hizo hatua ni kazi na majukumu ya Chama chochote tawala, ni lazima wafanye.

Leo ninafuraha sana kuona uhuru wa kujieleza ndani ya nchi yetu umepanuka na ni wa mfano wa kupigiwa mstari barani Afrika.

Gazeti la Mwanahalisi la Kubenea!!!???.
Taifa Huru la Mohamed Seif Khatib!!!???.

Nimefurahi kuona kuwa maneno aliyoyatoa Mh Kikwete wakati wa kuzindua bunge, kuwa atahakikisha kuwa vyama vya upinzani vinapata nafasi ya kuweza kufanya kazi vyema ndani ya kipindi cha utawala wake yametimizwa. Wabunge wa upinzani sasa hivi wana uhuru mkubwa wakufanya kazi zao bungeni kuliko wakati mwingine wowote.
Hapa sikatai, wana uhuru kiasi fulani (kiasi nikikumbuka suala kama la kufungiwa Zito).

Kazi ya CCM ya kuhakikisha vyama vya upinzani vinalelewa vyema na serikali yake nayo pia ni mfano wa kuigwa. Tuendelee kuisifu na kuikosoa CCM pale inapobidi.
Haya ndio maneno.

Mkuu,
Nia yangu si kukataza wachangiaji wengine wasieleze yale wanayoyaamini.

Mimi nimejaribu kueleza yale ambayo ninayaona ni mapungufu kwenye jamvi letu hili kuwa hatuyazungumzi.

Kama nilivyoeleza hapo awali 'ruksa' kuikosoa CCM kwani kwa kufanya hivyo mnaisadia zaidi kujirekebisha na kujua kero za wananchi ni zipi hasa.

Maoni yako nadhani wahusika wa CCM wameyaona na watayaangalia.

Tuendelee kuchangia
 
Unaona sasa!!! MANENO YA NYERERE!!! Huyu mzee ni kama MTUME wa Tanzania. Milele tutatumia maneno yake na kumtaja kila linapotokea tatizo. CCM, mhhhhh. Tulilia na CHADEMA ili hata sisi tuwe wanachama na kuhudhuria mikutano hata kama hatupo Dar, ila hadi leo wameingia mitini.

.

Wameingia mitini kivipi? Mbona CHADEMA wapo hapa? Kama unataka kujiunga tuma tu ujumbe kwenda info@chadema.net. Mbona mwenzio Mkandara alisema hapa ameomba kujiunga huko alipo na tayari ametuambia ameshajiunga?

Asha
 
Wameingia mitini kivipi? Mbona CHADEMA wapo hapa? Kama unataka kujiunga tuma tu ujumbe kwenda info@chadema.net. Mbona mwenzio Mkandara alisema hapa ameomba kujiunga huko alipo na tayari ametuambia ameshajiunga?

Asha
Hayo mazagazaga yenu ya CHADEMA myatafutie bandiko lake, hapa ni sherehe za CCM
 
Hayo mazagazaga yenu ya CHADEMA myatafutie bandiko lake, hapa ni sherehe za CCM


Kibunago, hadi huku upo? Mie nilifikiri nyie Wazenji mna-CUF yenu, inyeshe au liwake nyie mko tu huko. Hata kama CUF waanza biashara ya viungo vya Albino na ufisadi, nye aka mpo tu na Maalim wenu. Hivi hayo madevu yake hamuyaogopi?
Mbona wewe hukuanzisha bandiko lake kutushambulia kwa kuanzisha haya uyaitayo Mazagazaga? Umetuonea wivu mie na Asha na wewe umeiga!!!
 
Kuna sherehe ya kutimiza miaka 32 ya Ccm Huko Houston...Tawi la CCM marekani limefunguliwa na mwenyekitu ni J six na Katibu wake ni Zainab Janguo...so wale wale walereketwa wa CCM wanaweza kuhudhuria hiyo sherehe huko houston kwa maelezo ziaid tembelea mIchuzi blog spot....

Mwanakijiji it will not hurt if you join them...it will be a good expericne for all of us.
Umeshajiunga?
 
Umeshajiunga?

Yes nimeshajiunga na nitakuwepo huko (houston)this weekend...i think this is a great opportunity for watanzania waliokuwa marekani ili kuweza ku-contribe idea zao...
Matter of fact I am planning kwenda kugombea ubunge Tz 2010 mkoa wa njombe.
 
Naamini kwa dhati kuwa upinzani wa kweli utatoka kwa wananchi wenyewe wakichoshwa na ubabaishaji wa CCM na watakapoanza kutumia vichwa vyao katika masuala ya kisiasa.

Narudia tena kusema, ukimwona mtu yuko CCM kwa sana, basi ujue ana lake jambo.

1. Amepata nafasi ya urua humo.
2. Anavizia nafasi ya urua humo.
3. Ana mtu mwenye nafasi ya urua humo anakula naye au anajikomba ale naye.
4. Anabembeleza kitumbua chake kisiingie mchanga.

Kama wapo watu wenye uchungu wa nchi CCM, basi hao hawajai mkononi, ni wachache mno.

Ukimwona mtu anatoka CCM kwenda upinzani, basi huyo kabanwa kweli na wajanja wenzake au kasoma alama za nyakati anataka aendelee kutusanifu. Nasikitika kusema huyo atakuwa si mpinzani wa kweli bali ni "opportunist."

Habari ndio hiyo!
 
Kibunago, hadi huku upo? Mie nilifikiri nyie Wazenji mna-CUF yenu, inyeshe au liwake nyie mko tu huko. Hata kama CUF waanza biashara ya viungo vya Albino na ufisadi, nye aka mpo tu na Maalim wenu. Hivi hayo madevu yake hamuyaogopi?
Mbona wewe hukuanzisha bandiko lake kutushambulia kwa kuanzisha haya uyaitayo Mazagazaga? Umetuonea wivu mie na Asha na wewe umeiga!!!
Usio haya...ukome kuifuata futa CCM...huyo Asha keshalewa limbwata la chadema
 
Last edited:
Wakuu,habari!
Nafahamu kabisa wengi wetu humu tumesha yasikia maneno ya Mwalimu kwamba aliposema kuwa mpinzani wa kweli atatoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.Sikumbuki haya maneno Mwalimu aliyasema akiwa ana adress watu gani lakini ninachofahamu kwamba aliwahi kusema hivyo wakati wa uhai wake..Hili mimi linanitatiza.

Nikifuatilia historia wote tunafahamu kwamba Mrema Lyatonga alitoka ndani ya CCM na kuwarejeshea kadi yake ya uanachama baada ya kutokea kutkuelewana katika misimamo kama vile ile ishu ya Chavda n.k.Mrema alitoka na akawa Mpinzani tena very strong Mpinzani aliyetikisa nchi kwenye siasa za ushindani hasa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 1995 na alifanya vizuri katika kura zake za Urais ambapo mpaka sasa hakuna chama kingine chochote cha upinzani kilichoweka rekodi yake. Lakini pamoja na mafaniko hayo Mrema alididimia taratibu na hatimaye ameshapoteza mwelekeo kabisa wa kisiasa kwani kwa sasa kwa mtazamo wangu Mrema hafanyi siasa ila yupo yupo tu mradi tu bora siku ziende.

Kwa sababu hivyo basi kwa mtazamo wangu Mwalimu was wrong katika hili kwamba Mpinzani wa kweli ni lazima atoke ndani ya CCM. Mpinzani ni mpinzani tu awe ametokana ndani ya CCM ama ameibuka form now where wote wanaweza kuwa wapinzani wa kweli.
 
That was his opinion not a formula, principle or law of nature; wala sio kila alichosema kitafsirike alikosea au la, he was a man of his kind, he did what he believed and preach, he said what he was thinking and thats alone shows he was a good leader. So please stand as you, dont take anything from Nyerere as the platform or basis of argument, we live now he lived in his time!

Anyway check tena alisema 'mpinzani' au 'upinzani'????, they are bit different.

The only mistake that Mrema did was his great passion of becoming president 'alone' as Mrema,I do believe wangetoka wengi CCM we would have made another history.Though at that time it was not possible for any opposition part to win. moto ule ungeendelea kwa ajili ya kuondoa mizizi ya CCM ubongoni mwa watu basi 2000 au 2005 ndiyo tungetegemea upinzani angalau uweke 50-50 ya ushindani na CCM.

Lastly, I strongly believe that opposition leaders can emanate from anywhere and do great things; sio hawa tuliona sasa hakuna upinzani sasa naona tu is another way of giving people false hopes na kuwapa wao ajira na kurithishana vyama.

hatuna sababu ya kuwa na CCM ambayo watu wote wanajua mafisadi yet watu wote wanajua itashinda tu! halafu bado mtu bado anasema kuna upinzani!




we are all natural born leaders!!
 
That was his opinion not a formula, principle or law of nature; wala sio kila alichosema kitafsirike alikosea au la, he was a man of his kind, he did what he believed and preach, he said what he was thinking and thats alone shows he was a good leader. So please stand as you, dont take anything from Nyerere as the platform or basis of argument, we live now he lived in his time!

Anyway check tena alisema 'mpinzani' au 'upinzani'????, they are bit different.

The only mistake that Mrema did was his great passion of becoming president 'alone' as Mrema,I do believe wangetoka wengi CCM we would have made another history.Though at that time it was not possible for any opposition part to win. moto ule ungeendelea kwa ajili ya kuondoa mizizi ya CCM ubongoni mwa watu basi 2000 au 2005 ndiyo tungetegemea upinzani angalau uweke 50-50 ya ushindani na CCM.

Lastly, I strongly believe that opposition leaders can emanate from anywhere and do great things; sio hawa tuliona sasa hakuna upinzani sasa naona tu is another way of giving people false hopes na kuwapa wao ajira na kurithishana vyama.

hatuna sababu ya kuwa na CCM ambayo watu wote wanajua mafisadi yet watu wote wanajua itashinda tu! halafu bado mtu bado anasema kuna upinzani!




we are all natural born leaders!!

Asante sana kwa uchambuzi mzuri.Nakubaliana na wewe kwa karibu ote uliyoyasema isipokuwa hapo kwenye red ndio sikubaliani na wewe..it is not applicable kwa vyama vyote vipo vyama vya upinzani ambavyo ni serious vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba zao.
 
Nyerere aliongea kwa mtazamo wake na sio ndio kwamba lazima kiwe sahihi.
 
Asante sana kwa uchambuzi mzuri.Nakubaliana na wewe kwa karibu ote uliyoyasema isipokuwa hapo kwenye red ndio sikubaliani na wewe..it is not applicable kwa vyama vyote vipo vyama vya upinzani ambavyo ni serious vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba zao.

G.S when do you think opposition party can win the presidential position. Not that I dont like changes, not that I like CCM, is there any light at the end of tunnel? see how CUF has done amazing Job in Zanzibar, can we find the same in bara? why?

at least kama hata mwaka huu upinzani hautapata urais, unafikiri kwa makadirio yako, just estimate when do you think opposition party can lead this country?

Sikusema kuwa hawako serious! no , I mean there is not opposition. We are swimming in the sea of false hopes dear.Unakumbuka at that time ilikuwa akina Mrema, Mtikila at least wakisimama jangwani CCM wanakosa usingizi! that time when you can hear Mtikila akakupandisha mori wa kufuata magabachori-though he was wrong. But today ,can we find the same leader who will tell us to go and fetch these mafisadi na tuwashughulikie......ukifikia muda tukasema tuna vyama serious !!!! huku hatuoni matunda yao basi haviko serious in walking the walk, but are smart in talking the talk!


tell me!
 
Nyerere was a great leading leader kwa wakati ule kwa hiyo maono yake mengi yali base kutokana na mazingira ya wakati ule kwa mfano alipoanzisha vijiji vya ujamaa alifanya vile akijua kuwa watu wakikusanyika pamoja ni rahisi kuwapa huduma lakini vilikuja kushindikana

Kwa hiyo si kila kitu alichoanzisha au kusema Nyerere lazima kifuatwe kwa vile alikuwa nyota wa wakati ule basi watu wengi walikuwa wanafuata kila anachosema lakini si kweli kwamba mpinzani wa CCM lazima atoke ndani ya CCM lakini hatuwezi pia tukapinga moja kwa moja hoja hiyo
 
kaka nadhani ungefafanua kidogo au bado ulikuwa una calculate Einstein equation E=mC^2 , nadhani unaposema upinzani utafsiri maana yake kwamba hali ya wananchi kuwa na uwezo wa kuchagua viongozi wao pasipo kuwa na limitation ya chama kimoja unajua chama tawala nacho ni chama pinzani ila kipo madarakani na wapinzani wake ni wale wanaotaka kuchukua madaraka yake


kijana einstein punguza tafiti..........................hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Miaka ya nyuma wanasiasa na hata Baba wa Taifa alitabiri kwamba upinzani wa kweli utapatikana ndani ya CCM, means kama CCM ikimeguka tu. Lakini kwa namna mambo yalivyo sasa nina imani kubwa kabisa kwamba hakuna haja hiyo tena na upinzani wa kweli umeshatimia na chama tawala kinaweweseka vibaya sana.

1. Kupoteza majimbo yaliyoko kwenye miji mikuu kwenye uchaguzi mkuu - Arusha Mjini, Ubungo, Kawe, Ilemera, Nyamagana na mengineyo - wao kuambulia majimbo mengi ya vijijini ambako mwamko ulikuwa haujafika.

2. Kushindwa kuchukuliana hatua za wazi wazi za kuadabishana ila badala yake eti kuonyana kwa ustaarabu - wenyewe wanaita kunyofoa nyama chakavu - kujivua gamba. Hiyo ni failure nyingine kisiasa.

3. Chama kukosa mvuto kwa wananchi baada ya kushindwa ku address key issues za matatizo ya wananchi - Failure nyingine mbaya sana.

4. Kupoteza dira na mwelekeo - hakijulikani kama ni chama cha kutetea wananchi au mafisadi.

5. Umoja wa Vijana ambao ndiyo key kwa ukuaji wa chama umemeguka vipande vipande - haukubaliki kwa vijana wa vyuo vikuu na hata kwa vijana wasio wasomi wa kitanzania.

Sababu hizi na zinginezo zinanifanya nitanganze rasmi kwamba HATUHITAJI CCM KUMEGUKA ili kupata upinzani wa kweli, upinzani upo tayari na CCM wakae mkao wa kuwa chama cha upinzani muda si mrefu.

Pongezi zangu za dhati kwa DR. Slaa na CHADEMA kwa ujumla kuwaamsha watanzania kutambua haki zao za msingi na kila aina ya unyonyaji iliyokuwa inafanywa na watawala chini ya uongozi wa CCM kwa muda ya miaka 30 na ushee.

Mwisho natarajia CHAMA kikuu cha upinzani kuibuka na viti NUSU au zaidi vya ubunge na kuongoza halmashauri zaidi na nusu Tanzania - come 2015.

Haya yatawezekana tu kama tutashikamana pamoja kudai katiba mpya na mambo mengine ndani yake kama Tume ya uchaguzi nk.

Watanzania PONA yetu ni kuwa na chama kikuu cha upinzani ili miswaada ikifika bungeni isipitishwe kama vile UCHAKAVU kwenye vikao vyetu yva harusi.


UPINZANI OYEEEE --- CCM GAMBA LIMETOKA? hamjajichubua?

Taifa litajengwa na wenye moyo tu.
 
nani sasa wakati sasa ni zama za walionacho kama una unageuka muhindi u know why/? utalisishwa 2
 
Unaizungumziaje kauli hii ya Baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere aliyoitoa mnamo mwaka 1994.!
 
Back
Top Bottom