Kama wewe ni mwanaume au mwanamke na umetimiza miaka 27 lakini huna hata mtoto wa kusingiziwa,na hata kutoa mimba hujawahi basi unapaswa kujichunguza huenda una matatizo ya kizazi.haiwezekani mtu anaefanya ngono hadi kufikisha umri huo hana mtoto.hilo ni tatizo maana maisha ya sasa ni mafupi sana.sasa kama hutaacha legacy basi ni hatari sana kwako.au subiri tu kuitwa babu au bibi na watoto zako..wenzako wanaacha kuzaa wewe ndio unaanza[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Kama unachosema ni sahihi basi wengi tupo pabaya kwa kweli.
Nchi za wenzetu walioendelea hua wanasema "Bila tafiti hakuna ruhusa ya kuzungumza"
Sina shaka kama hujafanya tafiti ya ulichozungumza. Shaka yangu ni moja tuu, Je, umefanya tafiti ya hicho ulichosema ????
Na je wale waliopata watoto wao wakiwa na zaidi ya miaka 27 inakuaje ??
Mh.Reginald Mengi amepata watoto mapacha akiwa na 50 yrs plus,
Ndugu zetu wa mitaani waliochelewa kupata watoto baada ya ndoa nao vipi ??
Waliooana mapema ktk ujana wao angali na miaka 24-25 tu lakini hawakupata watoto ndani ya ndoa kwa zaidi ya miaka mitatu mpaka mitano Je ??
Wasomi wengi huchelewa kuoa, wengi wao huoa na umri wa miaka 30, lakini hakuna tafiti inayooanisha mojakwamoja kati ya wasomi na ukosefu wa watoto. Je ??
Tunahitaji tafiti madhubuti kabla ya kuamini falsafa yako hii, vinginevyo tunaomba mtizamo wa kitaalamu wa wataalam wa Afya ktk hili.